TUNAENDELEA WAKUU MAMBO YALIKUA MENGI KUNA DHARULA NYINGINE HAZIELEZEKI
Ebu tuiangalie hii methylphenidate ina fanana na cocaine katika namna ipi,
Kwanza kabisa hii methylphenidate na cocaine mfanano wake unaanzia kwenye chemical properties.
Ukiacha ufanano huo wa kikemikali, methylphenidate na cocaine zote huchochea uzalishwaji wa homoni zinazojulikana kama dopamine.
Kazi ya hii homoni ya dopamine ni kumfanya mtu ajisikie raha, kwaiyo ukiona ukifanya jambo au ukila kitu Fulani unahisi raha basi jua tu kama ukiwa kwenye jambo hilo kuna uzalishwaji mwingi wa dopamine ndio maana unakupelekea au unasikia raha.
Mara nyingi dopamine huzalishwa kwenye mambo kadhaa kama vile sex (wakati wa kufanya mapenzi), chakula apa ukiwa unakula chakula kizuri unachokipenda. Lakini pia wakati wa kusikiliza Muziki mzuri unaoupenda au hata kamali pia,
Apa kwenye kamali kwa wale wazee wa kuweka mikeka kama siku hujabeti unakosa amani kabisa lakini ukiweka mkeka nafsi inapoa inatakata broh!!!! hiyo ni kazi ya dopamine na ndio maana wataalamu wanasema kamali ni ulevi pia kama ulevi mwingine.
Kuhusu kiasi cha dopamine inayozalishwa wakati wa kushiriki ngono (sex) inasemekana haifikii kile kiasi cha dopamine kinachozalishwa baada ya kutumia unga (madawa ya kulevya). Kwa mantiki hii raha ya kuvuta madawa ni zaidi ya mbili au mara tatu ya raha ya kufanya ngono, hivyo teja au mtumiaji wa madawa anapata raha zaidi kuliko mtu anaefanya ngono.
Hhhhhmmm ni ukweli ugumu sana kuukubali lakini trust me, ndio maana mtumiaji wa dawa za kulevya si rahisi kuacha ata mkipambana vipi kwani kwa raha anayopata kule hakuna sehemu anaweza akafidia starehe ile.
Kazi kwako sasa ifikirie raha ya kula tunda alafu unaambiwa haifikii raha ya kuvuta unga, usione baadhi ya watu maarufu wameshindwa kutoka kwenye kifungo cha madawa ni kwasababu hakuna kitu kingine kinachoweza kumpa raha itakayofanana na unga.
Wakati we unakaa vijiweni unabishana tu kuwa hakuna kitu kitamu kama asali na pussy, watoto mjini wala ngada wanakuchora wanakuona mshamba hujui kitu.
Tusitoke sana nje ya mada nilikua najaribu kuelezea mfanano uliopo kati ya methylphenidate na cocaine tuendelee na upande mwengine.
Utofauti uliopo kati ya methylphenidate na cocaine au madawa mengine ya kulevya kama heroin hizi ni kwamba zenyewe hutengeneza kitu kimoja maarufu kama arosto.
Mara nyingi tunawasikia mateja wakilalamika kuhusu arosto, je! Hii arosto ni nini na mtu hujisikiaje akiwa kwenye arosto na afanye nini kuiondoa arosto.
Sasa ni hivi kadili mtumiaji anavyoendelea kutumia cocaine zaidi ndivyo hivyohivyo pia mwili huitaji cocaine zaidi ili kuendelea kuzalisha dopamine ya level ile ile ambayo humfanya ajiskie raha isiyo kifani.
Na ikitokea mwili umekosa cocaine hapo ndipo unakutana na neno arosto, mtumiaji hupitia wakati mgumu sana kwani mwili na akili kwa pamoja vinapambana kwa kutumia energy nyingi ili kujirudisha kwenye hali ile ya raha.
Kuna mfano mmoja niliwahi kupewa tatizo una lugha mbaya,
Imagine umemuandaa mtu kwenye kula tunda na umeanza tu zile in and out, alafu unatoa mashine unavaa unaondoka, asee apo binti atakupiga ata na stuli kama ipo karibu.
Hiki anacho feel binti wakati huo yaani alikua kwenye raha ya ajabu alafu from no where raha zinapotea lazima ata ghazibika sana. Sasa kwa mateja ile graph ya levels ya dopamine huwa juu akishatumia unga lakini ndani ya muda mfupi sana graph inashuka.
Sasa basi arosto ni ule mchakato wa ndani ya mwili wa kupambana kurudisha graph juu bila ya kuwa na cocaine, apa mwili hutumia energy kubwa na mwili ukifeli kurudisha graph juu kinachofata ni maumivu.
Mtumiaji hupatwa na shida nyingi zikiwemo maumivu ya viungo, kichwa kusikia baridi kali mapigo ya moyo na presha kuwa juu na wengine hupatwa na maumivu makali ya tumbo kukosa hamu ya kula na ata kutapika pia.
Katika point hii sasa ndio teja ata pambana kwa namna yoyote kupata tena unga ili ahakikishe anarudi kwenye zile raha na akifikia hatua hii tayari amekua mtumwa na hana future tena kwani kila atakachokua ana fanya ni kwa ajili ya kupata unga.
Usione kuna baadhi ya watu maarufu wamezama huko na hawawezi kutoka ukawaona wajinga na hawana akili hapana kosa lao la kwanza ilikua ni kujaribu. Jinsi ya kutoka huko sio rahisi inahitajika nguvu kubwa ya kimatibabu na nguvu ya kiroho pia ili uweze kutoka kwenye utumwa huo wa madawa ya kulevya.
Kuna siku nitagusia vita inayoendelea kati ya mabepali wa duniani na monopolization ya biashara ya cocaine na heroin, kuna namna ata vile vita vinavyoendelea huko Afghanistan ni miongoni mwa mipango ya mabepali katika interest za biashara zao.
Zile shida anazopitia mtumiaji wa cocaine wakati wa arosto mara nyingi japo sio kwa watu wote hupitia changamoto hiyohiyo baada ya matumizi ya methylphenidate.
Yaani ukitoka kutumia methylphenidate probably utapitia mambo yafuatayo kama sio yote basi Baadhi,
- kichefuchefu au ata kutapika
- usingizi kukosa hamu ya kula
- maumivu ya kichwa n.k
Unatakiwa kujua kuwa methylphenidate ni dawa halali na imehalalishwa na mamlaka zote za dawa na chakula duniani, lakini tukiwa kwa upande mwingine yaani huku kwenye unga nadhani kila mtu anajua balaa lake ikitokewa umakutwa ata na gram moja nini kinakupata.
Turudi kwenye simulizi tusichoke,
Baada ya kuijua dawa hii ya methylphenidate nilijiuliza ina maana fatemeh ni mgonjwa na ndio maana anatumia methylphenidate, kama ni kweli mgonjwa mbona sijawahi kuona dalili yoyote ya ugonjwa huo kwake.
Kuna muda maisha ya fatemeh yalikua yananiumiza kichwa kiasi kwamba siutaka ata kuyafikiria, nilimuuliza shahzad vipi kuhusu future ya mjukuu wake yaani baada ya hapo akiwa anaendelea na dawa hizo haiwezi kuleta shida ukubwani akishakua mtu mzima.
Shahzad alijibu hakuna tabu yoyote tena kwakua ameanza tiba tokea akiwa na miaka sita na ukilinganisha tatizo lenyewe sio la kimaumbile na saikolojia ataweza kuishi vizuri na kufanya kazi vizuri bila kuleta changamoto zozote.
Kibongobongo sidhani kama watoto wenye shida hizi hujulikana mapema na kupewa tiba, kama hawajulikani na hawapewi tiba basi makazini mwetu tuna wafanya kazi wenzetu ambao nao pia ni wahanga wa ADHD lakini bila wao kujua.
MIMI: hhhmmm sasa mzee shahzad mjukuu wako anaweza kufanya shughuli zipi za kitaaluma ambazo hazita leta shida kwenye changamoto aliyonayo.
Shahzad alicheka sana akauliza kwani mimi mpaka muda huo nimeona changamoto gani kwa mjukuu wake huyo.
Kiukweli sikua nimeona changamoto yoyote ile zaidi ya kumuona yupo kawaida, ila shahzad aliongezea kitu kutokana na swali langu nililouliza kuhusu shughuli anazoweza kufanya mjukuu wake apo baadae.
Shahzad alisema wengi wa watu wenye changamoto hiyo ya ADHD hujishughulisha na ujasilia mali, wengine wengi akiwa na mfano wa nchi hiyo ya Iran na kwingineko hutumika kama computer programmers huku waliobaki unudumu kwenye viwanda au sector zinazohitaji creativity.
Kwa nchi ya Iran kulingana na tafiti zilizofanywa na taasisi iliyojulikana kama psychosocial health Research institute, waliwahi kuchapisha au kutoa makala iliyo toa taarifa za tatizo hilo la ADHD ( attention deficit hyperactivity disorder) kwa nch hiyo.
Makala hii ilitaja kuwa kuanzia mwaka 1990 mpaka kufikia mwaka 2014 idadi ya watoto na watu wazima waliozaliwa na tatizo la ADHD walikadiliwa kufikia 33,000 ( therathini na tatu elfu).
Unaweza kuona ni idadi kubwa kiasi gani kwa nchi kama Iran kuwa na watu wenye shida hiyo hivyo ADHD haikuwa changamoto mpya miongoni mwa raia wa Iran.
Tukirudi kwa fatemeh sasa, niliona ni busara kwenda kumuuliza yeye mwenyewe kuhusu matumizi ya dawa hizo kwani mpaka wakati huo alishakuwa muwazi kwenye baadhi ya mambo yanayohusu maisha yake.
Lakini pia wakati huo huo nilikumbuka zile moment tukiwa haullaga namna gani alikua anapata shida kuhusiana na jambo ambalo javier aliliita ni arosto ya fish scale Cocaine aliyokuwa akipewa na Catarina.
Lakini binafsi nikiwa haullaga sikuwahi kumshuhudia kwa macho yangu aki sniff kwani alikua akienda kwenye jengo la pili pembeni ya maabara ambapo lilikua linatumika kufungashia mzigo pindi unapokamilika.
Shahzad alinitahadharisha niache kuendelea kuuliza maswala ya methylphenidate kwani kwa siku hiyo yeye hakutakiwa kuwepo hapo kwa muda mrefu kwani ataondoka.
Na aliniomba tukimaliza pale tufuatane kama nitakubaliana nae ili akanikutanishe na baadhi ya watu ambao anafikiria watakua na msaada kwa namna moja ama nyingine juu ya jambo letu.
Sikutaka kujibu moja kwa moja kwani niikumbuka kauli au masharti ya fatemeh kwamba sikutakiwa kwenda popote pale bila idhini yake wala siku takiwa kukutana na yeyeto bila idhini yake.
Lakini nilimuambia shahzad kwamba tutaenda wote kwakua ameshatangulia kusema watu tutaokutana nao watakua na msaada kwenye project yetu.