Baada ya kuamka asubuhi ile nakusoma ile message niliwaza nafikaje Lima, ila kwakua nilikua Ndani ya nyumba ile ya aparecida niliamini kuna utaratibu utakuwa umeandaliwa kwa ajili yangu.
Baada ya kujifanyia usafi wa asubuhi niliona nguo mpya zimewekwa pembeni ya kabati lililokua ndani ya chumba hicho. Niliamini zile nguo zilikua pale kwa ajili yangu, Hivyo nilizivaa zilezile nikaachana na overoll niliyopewa kule mgodini.
Nilikua nimebadilika kiukweli baada ya kuvaa zile nguo mpya nilizozikuta asubuhi ile ndani ya chumba hicho. Ilikua ni jeans classic sana moja ya rangi ya blue iliyopauka na t-shirt nyeupe,
nilikua Smart sana kimuonekano kwa siku hiyo, hivyo nilikua na faraja sana baada ya kujiangalia kwenye kioo kilichokua ndani ya chumba kile.
Nikiwa chumbani namalizia malizia kujiandaa kuna sauti za watu wawili niliziskia nje ya nyumba ile. Bila Shaka ilikua ni sauti ya aparecida na kijana wa kiume ambae sikumjua kabisa.
Nilipotoka ndani ya chumba kile nilimkuta aparecida akiwa amekaa kwenye sebule na kijana ambaye mpaka wakati huo sikuweza kumfahamu.
APARECIDA: good morning mustapha
( Habari za asubuhi mustapha)
Aparecida alinisalimia kwa bashasha sana ni kama alikua ananisubiri niamke kwa hamu sana. Wakati anaongea na mimi alikua na sura ya furaha sana kama kuna habari nzuri alitarajia kuiskia kwenye midomo yangu.
Huku akiwa na sigara mdomoni kwa kutumia kingereza cha hovyo sana na kisichoeleweka alijaribu kunitambulisha kwa kijana yule niliyemkuta sebuleni.
Dhumuni lake nilishalijua hivyo na mimi nilijitambulisha kwa kijana yule ambae kwa bahati nzuri alikua anaongea kingereza.
MIMI: hi..!!! This is mustapha, nice to meet you broh.
( Habari, mimi ni mustapha nafurahi kukutana na wewe)
I'm Damião, nice to meet you too
( Mi naitwa Damião nimefurahi sana kukuona)
Jamaa alikua anaitwa Damião, alikua ana mwili Fulani hivi wa uzembe uzembe japo hakua mnene sana lakini naweza sema kuna maisha Fulani hivi amekulia yale ya msosi wa draft.
Kiufupi alionekana kama kijani mmoja hivi ambae hajui shida kabisa mpaka kufikia umri huo.
Kwa pamoja tulikaa mezani kwa ajili ya breakfast, huku aparecida alikua bize kuandaa mapochopocho ya kufungua kinywa asubuhi hiyo.
APARECIDA: Damião, meet fatemeh's boyfriend. He seems to be very lucky man.
( Damião kutana na boyfriend wa fatemeh, jamaa anaonekana kua mwenye bahati sana)
Damião aliniangalia kwa kunitamani sana kwani alionekana kutokuamini kama ni kweli nilikua boyfriend wa fatemeh.
Ile taarifa ya aparecida kuhusu mimi na fatemeh sikutaka kuipinga haraka haraka kwani sikujua alikua na nia gani au alikua na ushahidi gani.
Aparecida alisema ata yeye amefurahi kuniona kwani hakutarajia kwa siku za hivi karibuni kumuona msichana huyo akiwa na boyfriend.
Alidai amekaa na fatemeh miaka 2 eneo hilo, lakini miaka hiyo yote miwili msichana yule hakuonyesha dalili yoyote ya kuwa na mahusiano.
Fatemeh hapo awali wakati ndio anafika kwenye mji huo hakupenda kabisa kuchanganyika na wanaume wala hakutaka kabisa mazoea na wanaume.
Tabia hii ilisababishwa na mazingira yale ya kiislamu aliyolelewa kwenye kituo kilichoitwa nursery imam Ali Huko mjini Tehran.
Ilionekana wazi kabisa kitendo cha Manuela au fatemeh jina jingine, kukubali kulala chumba kimoja na mimi ilikua ni sababu iliyomuanisha aparecida kua tulikua wapenzi.
Hivyo aparecida aliendelea kusema kwamba mimi nitakua na kitu cha pekee sana kilichomvutia binti huyo. Nilitamani kuwauliza background ya fatemeh (Manuela) ilikuaje akafika hapo na nini alikua akifanya akiwa hapo.
Ila niliamua kukaa kimya kwani niliamini kwenye stories zinazoendelea hapo ningeweza kupata lolote lililohusu background ya fatemeh (Manuela).
DAMIÃO: Did you meet in the mine?
( Mulikutana mgodini?)
Damião aliuliza kama mimi na fatemeh tulikutana mgodini, hapo nilijiongeza kwakua nilikua nimefika hapo jana yake nikiwa na overoll za mgodi nikasema ni kweli tulikutana mgodini.
Kwa maelezo yaliyokua yanaendelea pale niligundua fatemeh ( Manuela) alifika hapo mara ya kwanza akiwa kama mtaalam ambae anaenda kuhudumu kwenye ule mgodi. Japo sikujua alienda kwenye mgodi huo kwa taaluma ipi iliyompeleka mgodini hapo.
DAMIÃO: so broh!! You are as Strong as fatemeh
( Kwaiyo ndugu yangu na wewe unanguvu kama fatemeh alivyo)
MIMI: what you mean
( Una maanisha Nini?)
Hapa Damião alinichanganya kidogo kwani aliuliza kama na mimi nina nguvu kama fatemeh ( Manuela) ila nilishindwa nimjibu nini.
DAMIÃO: usiniambie kama hujui una date na mtu ambaye alipitia mafunzo ya ninjutsu.
Damião aliendelea kunichanganya zaidi baada ya kuniletea msamiati mpya wa ninjutsu ambao sikuwahi kuusikia hapo kabla.
Damião alidai kwamba aligundua fatemeh alikua na uwezo binafsi kwenye self defense pale ambapo wakiwa bado wageni kabisa mgodini. Apa aliniambia walianza wote kazi pale mgodini lakini yeye aliwahi kuondoka kwa ajili ya masomo na mda huo alikua akisoma.
Fatemeh Akiwa bado mgeni mgodini aliwahi kushikwa tako na gringo mmoja hivi ambae baada ya hapo alijutia maamuzi yake.
Kwa maelezo ya Damião ni kwamba huyo gringo hadi leo shingo yake haijanyooka kutokana na pigo la ajabu alilolipata kutoka kwa fatemeh (Manuela).
Hapo niliamua kumwambia Damião kuwa sikua na habari yoyote ya kuhusu uwezo wa kimapigano wa fatemeh.
Damião alicheka sana huku akinisisitza nimepotea njia yaani sitakiwi kumtibua ata kidogo binti huyo kwani hakuwa mtu wa kawaida kabisa.
Aliendelea kusema kwa jinsi anavyoniona nilivyo mtoto wa mama basi sio swala kubwa kabisa kwa fatemeh kunivunja shingo kwani sitompa challenge yoyote endapo ata aamua kunishughulikia.
Nilianza kuhisi kama kuna uhalisia wa maneno yale niliyoyasikia kutoka kwa Damião. Nilikumbuka siku ya kwanza ambapo Manuela (fatemeh) alinipa ahadi tukutane pale kwenye ngazi za magogo chini ya maabara.
Ile siku kuna namna alinivuta sikuelewa nimefikaje pembeni ya barabara kwenye kichaka, lakini pia aliweza kunifikia karibu na kunigusa bila mimi kuhisi kama kuna mtu nyuma yangu.
Jambo lingine lilikua ni uwezo wake mkubwa wa kutembea umbali mrefu bila kuchoka na jinsi alivyokua anajiamini akiwa porini.
Kwa hayo mazingira niliamini ni kweli Manuela (fatemeh) anaweza kuwa na kitu cha zaida kwenye maisha yake especially mambo yanayohusu jeshi au mapigano yoyote.
Damião aliendelea kunipa stories kidogo anazozijua kuhusu fatemeh, japo alidai haijui ata nusu ya story ya maisha ya fatemeh ila kuna namna anaweza kuelezea ni nini anakijua kuhusu binti huyo.
Alidai fatemeh aliwahi kupitia mafunzo maalum yaliyoitwa ninjutsu, Ninjutsu (mara nyingi huitwa Ninpō) hii ilikua mbinu ya upiganaji iliyotumika kwenye martial arts za wajapani.
Hivyo basi hapa alidai fatemeh alikua ni ninja wa kike yaani KUNOICHI. ilionekana kama dogo (Damião) alikua ananitisha kwamba kama ni kweli nilikua nakula yule mchumba basi niache haraka sana.
Apa ilibidi nimuulize Damião ina maana fatemeh alisafiri mpaka Japan kwa ajili ya mafunzo hayo ya kunoichi.
Kwa mujibu wa Damião ni kwamba mafunzo hayo aliyapatia hukohuko Iran nje kidogo ya jiji la Tehran kuliitwa jughin.
Damião alifuatilia taarifa hizo kwani na yeye alitamani kujua mapigano hayo ya ninjutsu kwani muonekano wake ulimfanya kudhaulika sana.
hivyo akaelekezwa kwa master aliyeitwa faraji kwani ndiye alimpika fatemeh mpaka kufikia hapo alipo.
Katika kujifunza mbinu hizi za ninjutsu mavazi yake hu favor wanawake tena hasa wale wanafata shari'a rules. Kwani mwanafunzi hufunika sehemu kubwa ya mwili wake hii ndio ilifanya wanawake wengi wa Iran kujifunza sanaa hii ya ninjutsu.
PICHA YA MFANO WA WANAWAKE WAKIWA KWENYE MAFUNZO HAYO YA NINJUTSU
(PDF)
Baada ya story chache zilizomuhusu fatemeh na vitisho vya hapa na pale. Damião alinihasa nichangamke kwenye msosi kwani tunasafari ndefu ya kuelekea Lima.
Alidai girlfriend wangu alitangulia huko mapema kwa ajili ya kufanya utaratibu wa safari yetu. Hivyo basi alimu assign Damião anifikishe huko lima ili ikiwezekana kesho yake tuanze safari.
Kiukweli sikuona logic ya kuniacha usiku ule na yeye kuelekea mwenyewe huko lima. Hivyo basi bila kupoteza muda nilichangamkia ile breakfast sikutaka kupoteza muda tena.
Hapo at least nilianza kuona matumaini ya kurudi tena bongo kuendelea na struggle nyingine za maisha. Sikuwaza mikwala ya mzee massawe zaidi niliwaza kumueleza nini kimenikuta na kumuomba msamaha anirudishe shule.
Kwa wakati huo nilianza kukusanya taarifa taratibu zilizo muhusu fatemeh.
0623329512 Whatsapp ni AF TATU kupata muendelezo wa pdf
Sent from my ZTE T1002 using
JamiiForums mobile app