Mugabonihela
JF-Expert Member
- Dec 12, 2022
- 306
- 1,784
- Thread starter
- #1,081
Tunaendelea wazee wa kazi,
Ramani niliyopewa na Shahzad ilikua na visiwa vingi vidogo vidogo japo na vikubwa vilikuwepo pia ndani yake.
Kwa mujibu wa ramani hiyo ili kufika rapta nilitakiwa kwanza kabisa kufika kisiwa kimoja ambacho kilikuwa ni miongoni mwa visiwa vikubwa kwenye ramani ile.
Naam bila shaka kisiwa kile ndio eneo kilipo kisiwa cha mafia kwa sasa kwenye bahari hii yetu ya Indi. Hivyo basi Shahzad alidai safari yangu itaanzia pwani ya Dar es salaam na kisha nitatimkia mafia.
kwanini nitaanzia pwani ya Dar es salaam, ni kwa sababu kwenye ramani ile kuna eneo pia liliwekwa alama iliyoonyesha kuna maeneo kwenye pwani ya Dar es salaam kuna vitu vya msingi ndani yake.
Shahzad alidai yeye wakati anakuja bongo alitarget rapta peke yake na sio sehemu nyingine. Na hivyo basi baada ya kuwa amesharudi kwao ndipo akagundua kwenye ramani ile kuna maeneo mengine yaliwekwa alama za kuonyesha uwepo wa mali.
Kwa bahati mbaya sana yeye hakudili au hakujihusisha na maeneo hayo, yeye aliwekeza nguvu zote akili pamoja na pesa kwenye mji mmoja tu ulioitwa rapta.
Hivyo basi alisisitiza pia kama kuna uwezekano tupitie Kwanza pwani ya Dar es salaam ili kutafuta eneo hilo ambalo lipo miongoni mwa maeneo yaliyowekewa alama na ndugu zake.
Maelezo mengi yaliyohusu alama zile kwenye ramani yaliandikwa kwa lugha ya kwao hivyo ilikua ngumu kuitafsiri. Lakini Shahzad alisema kwa uwepo wa uyo bwana mwingine kazi haitakua ngumu kwa upande wangu.
Kiukweli sikua tayari kusikia story za uwepo wa huyo mtu mwingine aliyekuwa anatajwa na Shahzad kwenye misheni yangu.
Ila nilishindwa kukataa papo hapo nilikua nasubiri tumalize kila kitu ndipo nitafute gia ya kumkataa huyo chalii yake.
MIMI: mzee mbona hii ramani ina visiwa vingi namna hii.
SHAHZAD: hahahahah ahaha kumbe bado hujatembea pwani ya Tanganyika wewe, we mzanzibari wa wapi ndugu yangu.
Hiyo ramani ni ya pwani yote ya Africa mashariki kuanzia somalia mpaka mwanzoni mwa Mozambique.
Nikwambie tu mjukuu wangu kuwa bahari ina mambo mengi kiasi kwamba ata wanaojiita wataalamu wana kubali hawaijui bahari kabisa.
Na kama wanaijua basi kwenye asilimia 100 wao ujuzi wao hauwezi kufikia ata asilimia 7 kwa wanachojua kuhusu bahari.
Shahzad alionekana kuijua sana bahari au niseme tu alionekana kuwa na taarifa nyingi zinazohusu bahari hususani ile bahari ya sham.
Lakini aliendelea kusema kwenye bahari zote kunavimbwanga lakini Atlantic na Indian ocean hizi zimezidi vituko.
Apa shahzad alisema kwakua ndio ninaanza kucheza na bahari basi hana haja ya kuniambia mengi kwani kwa anavyoniona anahisi nitaogopa na kutokuendelea na misheni.
Ila alisema watu nitakao washirikisha nihakikishe nachukua wazoefu wanaoyajua maji ya bahari na viumbe wengine waliomo ndani yake.
Kuna muda alisema ndani ya bahari hususani bahari ya Atlantic na bahari ya Indi. kuna sehemu ata sheria za physics hazifanyi kabisa kabisa, yaani hakuna cha relativity, quantum mechanics wala sijui ujinga gani.
Yaani hayo maeneo hayazitambui sheria za wafizikia kabisa kabisa na ndio maana mpaka leo wataalamu watakueleza mengi kuhusu anga pekee na sio bahari.
Kwa mujibu wa shahzad alisema kwakua nimetaka kujihusisha na bahari basi hakuna namna nitaacha kuzihusisha roho zisizoonekana kwenye ulimwengu huu wakawaida isipokua baharini pekee.
Kwakua Shahzad alikua ameanza kuielezea bahari hususani bahari ya Indi na Atlantic nilimuuliza kama amewahi kusafiri njia zote hizo ambazo yeye amedai ni hatari sana yaani Atlantic na Indi.
Alisema amepita njia zote hizo enzi za ujana wake wakati bado anapambana kabla ata ya kuoa marehemu mke wake.
Nilimuuliza mzee kuhusu eneo linaloitwa Bermuda triangle huko baharini, lakini kwa majibu yake alisema hajawahi kukutana na eneo hilo kwenye maisha yake ya bahari.
Kuna story nyingi zinadai Bermuda triangle ni eneo huko kwenye bahari ya Atlantic, eneo hilo mara nyingi linaaminika kumeza meli na ndege zote zinazokatisha kwenye pembe tatu hizo za bahari ya Atlantic.
Ila shahzad yeye anasema hakuwahi kukutana na eneo hilo kwenye maisha yake ya safari za Atlantic. Na mimi nilimuuliza hivyo makusudi kwani sio mara moja nimekua nikisikia story zinazohusu eneo hilo.
Ila Shahzad kuna kitu alikisema,
Alisema kwenye hizi bahari mbili kuna sehemu za hatari sana ambazo kuzitambua kunahitaji msaada wa roho nyingine.
Na apa ndipo unapokuja umuhimu wa pete ile aliyonionyesha sikuile wakati anatoa zile artifacts.
Alisema hujawahi kusikia kuna vitu au watu wanapotea baharini na hawaonekani tena kwenye ulimwengu wetu huu wa nyama.
Alisema sehemu hizo bwana ndio zilezile ambazo ata sheria za physics hazifanyi kazi, yaani kila kinachosogelea hapo huvutwa na hakiwezi kutoka tena.
Kiuhalisia ni kwamba hakuna kinachoonekana kwenye eneo hilo ata mwanga wenyewe hauonekani ahahahah hahahha.
Yaani kwa lugha rahisi ata mwanga ukienda hapo haurudi, waliosoma soma physics si mnajua kuwa ili uweze kukiona kitu basi ni lazima mwanga uwe unatoka kwenye hicho kitu.
Sasa basi kwenye maeneo hayo ata mwanga ukienda hautoki, utaona nini eti? Mzee alidai kila kitu husimama kikifika apo mpaka muda husimama eti, yaani kuna uwezekano ukiingia umo usizeeka karne karne
Kwa mantiki hiyo sisi tuliosoma physics maana yake eneo hilo escape velocity ni infinity.
OTEA NI WAPI HAPO. hahah haha
Binafsi nilihisi hiyo ndio Bermuda triangle yenyewe lakini mzee aliikataa Bermuda akasema hajui kuhusu hiyo kitu hivyo hataki kuwa muongo.
Alichokijua yeye ni hicho alichonieleza na kama nitajikita baharini na nitakua na msaada wa nishati za roho alizozisema basi nitaona alichoniambia.
Nilianza kuhisi kama mzee ananitengenezea mazingira ya kuingia kwenye ulimwengu wa giza usioonekana.
Kuna jambo lingine aliliongea kuhusu bahari ya Indi, alisema tunajua pacific ndio bahari kubwa na yenye kina kirefu kisha inafuata Atlantic kama sikosei, lakini sasa bahari ya Indi pamoja na kua ni ya tatu ndani yake imehifadhi mambo mengi sana.
Alidai nitayaona nikianza kuzamia kwenda huko, apa alisema kuzamia baharini ni ulevi mkubwa sana yaan endapo nikianza tu basi nitatumia muda mwingi kwenye maisha yangu kuwa chini ya bahari.
Alisema usishangae watu wanatoka nchi moja kwenda nchi nyingine kwa lengo la shughuli hiyo ya uzamiaji tu.
Apa alisema bahari hii ya Indi ndani yake kulikua na mabara,
Hhhhhmmm sikumuelewa
Mzee alidai hii bahari tunayoiona kuanzia coco beach kuja DP WORLD kurasini na kisha ikasambaa kwingineko duniani. Eti Bwana Ndani yake kuna mabara yaliyomezwa wakati Dunia inakatika vipande vipande ili kutengeneza haya mabara ya sasa.
Yaani kuna muda Shahzad niliona ananipanga kabisa ila nikawa namvumilia kwa kua ni mtu mzima sana siwezi kumpinga waziwazi.
Sasa kwa logic ya Shahzad ni kwamba kuna mapande makubwa ya ardhi ambayo yapo baharini na yalikatika kwa zaidi ya miaka billion 3.5 iliyopita.
Kama alichokua anakisema mzee ni cha kweli basi mzee kichwa chake kimehifadhi mengi mno.
Hakika siku hiyo mzee alinipa mengi japo mengi hayo yalikua na vitisho ndani yake na kuna muda nilihisi nisichukue pete yake kwani inaweza kuwa na mabalaa zaidi.
Au naweza kuivaa alafu nikifika deep sea jamaa wajue mi mwenzao maana ata huyu shahzad nilishanza kupoteza imani nae.
Baada ya story nyingi nakua ameshanikabidhi ramani rasmi alisema tunaweza kwenda msikitini kwakua muda umefika.
Lakini kabla hatujaenda huko alisisitiza kua ramani ile kama sitoifanyia chochote yaani kama misheni ikishindikana basi nitairudisha pale mwaka wowote Kwani familia yake tayari imeshanitambua.
Alidai yeye tayari yupo maji ya jioni naweza kuanza safari nisifike ata airport ya Dar es salaam nikasikia amekwisha kuaga Dunia.
Siunajua tena wazee ambao umri umeenda sana wanavyopenda kujitabiria kifo.
Shahzad alisema tukifika msikitini na kurudi nyumbani basi yule bwana aliyeongea nae kuhusu kufuatana na mimi ata kua tayari ameshafika nyumbani apo.