TUNAENDELEA
Baada ya kuona nimemuacha fatemeh njia panda kutokana na lile swala la kumtajia jina la Tala, niliona kama nimemuongezea mawazo ya kumfanya aendelee kutafakari. Na sio hilo tu ata baada ya kumwambia kuwa javier hakuhusika na kifo cha Gatkuoth pia lilimfanya atafakari upya swala hilo.
Niliamua kumuacha peke yake na mimi nikaelekea kwenye room yangu kwa ajili ya kupumzika sikutaka kumsumbua kabisa kwa siku hiyo.
Kabla sijalala nilitafakari sana kuhusu swala la mzee shahzad, nilitamani nimalizane nalo mapema ili nirudi tena bongo kujaribu bahati yangu kuona kama naweza kupata Chochote.
Na pia nilitamani sana kukutana na watu ambao aliwasema kuwa wangenisaidia kwenye project hiyo lakini shida ilikua masharti ya fatemeh ambae hakutaka nikutane na watu wa aina yoyote pasipo idhini yake.
Baada ya mawazo ya hapa na pale nilifikia conclusion kwamba nisubiri fatemeh apitiwe na usingizi kisha nishuke basement nikaongee na Mohamed.
Sababu ya kwenda basement kwanza kabisa ni kumuuliza Mohamed kama ni kweli yeye alikuwepo kule clinic ya moyo nilipoenda na shahzad.
Kama ni kweli ni yeye, je! Na yeye ni mgonjwa au alikua ananifuatilia mimi kwenye mizunguko yangu na kama alikua ananifuatilia basi ni wazi atakua anamjua huyo Tala ambae kwa mujibu wa ujumbe ule nilitakiwa kuwa namsikiliza sana na nisipuuze kile alichokuwa ananiambia.
Basi bwana baada ya masaa kama mawili hivi niliamini fatemeh hawezi kuendelea kuwa macho kwani nilimuacha na mawazo mengi sana baada ya kumpa stories za javier na kile ki memo kilichoandikwa Tala.
Nilishuka na kuelekea basement kwa kutumia lift, jengo lile lilikua kimya zaidi mida ya usiku mnene kama ule. japo mara nyingi jengo hilo lipo kimya lakini kwa mida ya usiku ukimya ule huongezeka maradufu.
Nikiwa basement eneo ambalo nilitegemea kumkuta Mohamed kama alivyosema siku ile kwamba nikiwa na changamoto yoyote naweza kumkuta mahali apo.
Haikua hivyo kabisa kwani nilimkuta bwana mmoja mnene sana lakini alionekana kuwa lindo mida ile, na alipo niona tu aliniuliza kama niihitaji kukutana na Mohamed.
Sikujua ni kitu gani kilimfanya ajue ninataka kuonana na mohamed usiku huo. Lakini bila kuongea maneno mengi alinielekeza sehemu ambayo naweza kuonana na mohamed.
Aliniambia ili kumpata Bwana huyo Mohamed niende floor ya juu kabisa yaani floor ya mwisho ya jengo lile huko ndiko naweza kumkuta Mohamed. Kwakua nilisha dhamiria kuonana na mohamed basi nilianza safari ya kuelekea mahala nilipo elekezwa.
Haikuchukua muda mrefu kabisa kufika huko kwa sababu ya uwepo wa lifti ndani ya jengo lile. Nilipofika maeneo yale nilisikia sauti ya mtu akinikaribisha na bila shaka alikua ni Mohamed mwenyewe.
Lile eneo kwakule juu ya jengo lile kulikua na plain kabisa yaani hakukua na chochote na sikujua Mohamed alikua anafanya nini kule.
Mohamed alinikaribisha kwa maneno mawili tu huku akisema anatumaini nimeanda kule au nimemfuata maeneo ya huko kwakua kuna changamoto nimekumbana nayo.
Alisisitiza tu changamoto hiyo isiye ya mapenzi wala isiye inayohusu pesa. Na kwa kujiamini kabisa nilimwambia hivyo alivyovitaja haviwezi kuwa tatizo kwangu kwani vyote ninavyo.
Kuhusu mwanamke ninae binti mzuri ambae yeye mwenyewe alinishuhudia siku ile tukiwa tunadendeka ndani ya gari, na kuhusu pesa mwanadada huyo anazo za kutosha ata kumlipa yeye na kibarua chake cha ulinzi wa jengo lile.
Ni kama Mohamed kuna jambo alitaka kuliongea kuhusu ile kauli yangu ya kua nina mpenzi lakini nilimuona anasita kuitamka.
MOHAMED: What has brought you to me?
( Nini kimekuleta kwangu)
Kwa kujiamini kuliko pitiliza nilimkazia sura Mohamed huku nikumuuliza swali moja tu.
MIMI: I want to know why you're investigating me so much? I last saw you in the mosque yesterday
( Nataka nijue kwanini unanichunguza sana nilikuona msikitini jana)
MOHAMED: hhaahh ahaha hahah I'm glad to see you in that look,
( Nimefurahi kukuona kwenye muonekano huo)
Apa Mohamed alimaanisha amefurahi kuniona nikiwa serious lakini pia nikiwa najiamini na maneno yangu ya uongo.
Lakini pia alisema hakutarajia kama kuna muda nakua vile alijua mimi ni yuleyule wa kupelekeshwa na fatemeh kwenye kila kitu.
Ila alisisitiza jambo moja, alidai fatemeh ni kiumbe Smart sana kuliko navyofikiria hivyo hakuna jambo naweza kufanya nikamficha yeye eti asijue nitakua najidanganya.
Mohamed aliomba nieleze jambo lililonipeleka huko mapema sana ili ikiwezekana nirudi nyumbani haraka.
Jambo la kwanza nilishamueleza tayari japo hakunipa majibu ya kuridhisha kwanini alionekana kunifuatilia siku ya jana lakini kwa majibu yake yalionyesha hakua na muda huo kabisa.
Jambo la pili nilimueleza kama ataweza kunisaidia kufika kwenye kituo kilichoitwa nursery imam Ali. Nilimueleza kama nina shida ya kufika apo nionane na yeyote ambae alikua na muda mrefu kituoni apo.
Jibu la Mohamed lilikatisha tamaa kabisa, Mohamed alidai natakiwa kufuatilia mambo ya msingi na maana na yanayonihusu.
Apa alidai natakiwa kujua kwanza kwenye maisha yangu natafuta nini, nikisha kwisha kulijua hilo sasa nikomae na kutafuta kile chenye manufaa na sio ku dili na Mambo yasiyo na maana kwenye maisha yangu.
Sikuelewa kama Mohamed alijua ninataka kufika kituoni kwa dhumuni lipi,
Lakini kikubwa nilichoambulia kukisikia kutoka kwa Mohamed ni maneno magumu na ya vitisho.
Mohamed alisema kuna waliojifanya wana moyo kama wangu siku za nyuma kidogo, japo hakusema moyo kama wangu kivipi.
Alidai waliojifanya wana moyo kama wangu waliishia kufa kifo kibaya na kuzikwa kama mizoga baada ya miili yao kukaa zaidi ya siku mbili na kugundulika kama walishakufa.
Kuna muda nilihisi maneno yale kama yanamlenga Gatkuoth kwani kwa story za Javier ni kwamba mwili wa Gatkuoth ulikua na zaidi ya siku moja toka kufariki kwake na mpaka kugundulika kama alishaaga Dunia.
MIMI: Do you mean the death of Gatkuoth?
( Unamaanisha kifo cha Gatkuoth)
MOHAMED: No, I mean the death of someone who resembles you everything
( Hapana, namaanisha kifo cha mtu aliyefanana na wewe kilakitu)
Hakukua na haja ya kuumiza kichwa sana kwani kwa sentensi hiyo ni wazi kabisa mimi ndie nilikua nikifanana na Gatkuoth kila kitu.
Mohamed alimalizia kusema kuwa nina nguvu na nina akili timamu tofauti na yule aliyemuona mara ya kwanza hivyo basi nachopaswa kufanya ni kutumia akili zangu pamoja na nguvu zangu ili kutoka kwenye mtego ambao nimekua nikijiingiza kila siku.
Alidai kupitia mtego ule naweza kujiingiza kwenye matatizo makubwa sana ambayo yatanigharimu kuanzia mimi, ukoo wangu wote na mbaya zaidi ata kwa nchi yangu ambayo ni changa sana kwenye mambo yale.
Apa niliwaza jambo moja, kwani Mohamed alikua ni mlinzi tu pale kwenye lile jengo je aliwezaje kujua habari za kifo cha Gatkuoth.
Niliamua kujiondokea japo nilifika hapo kwa mbwembwe nyingi lakini kwa namna nilivyoondoka niliondoka kwa upole sana kwani maneno ya Mohamed ni wazi yalidhoofisha.
Haikunichukua muda mrefu kutoka floor ya mwisho juu kabisa ya jengo Mpaka kufika kwenye floor iliyokua na apartments ambayo ilikua inatumiwa na fatemeh.
Kitu cha kufurahisha baada ya kuingia ndani nilimkuta fatemeh akiwa amekaa kwenye kiti as if alikua ananisubiri kwa hamu sana nitoke kwenye ile safari yangu ya usiku usiku.
Baada ya kumkuta fatemeh kwenye pozi lile niliishiwa nguvu kabisa huku nikiwaza namuongopea kwa namna gani ili anielewe.
Kwa maneno machache sana fatemeh aliniomba kwa kua nimeshindwa kuwa muelewa basi kesho itakua siku ya mwisho kwenda kwa shahzad. Hivyo nachotakiwa kufanya ni kumueleza shahzad ukweli kwamba muda wa mimi kuendelea kuwepo Tehran umeisha natakiwa kurudi bongo.
Fatemeh alisema ameamua kufikia muafaka huo kwa kua ni heri nusu Shari kuliko shari kamili. Hivyo hatonipa nafasi ya kuongea lolote zaidi ya mimi kwenda kupumzika nikiwa najua kua kesho shahzad anatakiwa kumaliza program zote.
Alimalizia kwa kusema kama shahzad atasema hizo program zilizobaki zitatuchukua zaidi ya siku moja basi ata mlipia nauli na kilakitu ili tu nifuatane nae tuje wote bongo.
Fatemeh alisema kumbe javier alikua yupo sahihi sana kupitia matusi yale na maneno yote machafu kwangu. Ata yeye tayari alisha thibitisha kuwa kuna namna nina walakini kwenye uelewa wangu.
MIMI: But I didn't get out in search of women
( Lakini sikutoka nje kwa ajili ya wanawake)
FATEMEH: i don't give a f***
( Hainihusu na sijali)
Kwa mara ya pili ndani ya siku moja niijiona kabisa nimemkera binti huyu kwa viwango vya juu sana.
Kabla sijaingia kwenye chumba kile ninacholala nilijaribu kumueleza tena kama nilienda kukutana na mlinzi wa jengo lile ambae alijitambulisha kwangu kwa jina la Mohamed.
Kwa mujibu wa fatemeh alinijibu kwamba ndani ya jengo lile nisijisumbue kwa lolote Kwani sio mlinzi pekee ata mfagiaji wa mule alikua ni mtumishi wa idara ya MOIS.
Hivyo basi kwa majibu yale tu nikagundua hata Mohamed ni walewale machalii wa MOIS, na nilithibitisha hilo pia baada ya kukumbuka maneno ya Mohamed juu ya kifo cha mtu aliyefanana na mimi.
Nilibaki na swala moja kichwani, ilikuaje ndani ya idara moja watumishi wapishane taarifa. Yaani kwanini Mohamed ajue kuhusu kifo cha Gatkuoth wakati huohuo fatemeh ambae ndio alikua kwenye eneo husika asijue chochote kuhusu kifo cha Gatkuoth.
Lakini pia kwa namna nilivyokaa apo na fatemeh ilionekana wazi treatment ya fatemeh ni ya tofauti kabisa na wale wengine kwenye jengo hilo. Fatemeh aliwekwa under intensive care yaani kila alichofanya kiliratibiwa na watu ambao hatukuweza kuwajua je!! Huyu fatemeh ana nini hasa.