SEHEMU YA 04
Ras alikua anatumia nguvu kubwa kunishawishi kitu kilichofanya niamini kuna namna yeye atanufaika baada ya Mimi kuungana na McKenzie kwenye safari hiyo. Kwa maelezo ya Ras, kazi nitakayoenda kuifanya huko itakua ni kazi ya mkataba. hivyo nikiamaliza mkataba nitaweza kuludi tena bongo kuendelea na maisha yangu. Kwa Mara ya kwanza Ras aliniita jina langu MASSAWE huku akisisitiza kwamba nikiludi nitapata mrembo mwingine tena mzuri zaidi ya Merry kwani aliamini nilikua nampenda sana Merry.
Kutokana na ukweli kwamba toka nifike dar es salaam nilikua namtegemea Ras Kwa kila kitu sikuona haja ya kukataa kwani endapo ningemkatalia kuna uwezekano mkubwa asingeendelea kufanya shughuli zake na Mimi.
Kichwani nilikua najiambia kwamba nikiludi nitakuja kumfanyia mambo makubwa sana baba yangu na mama yangu. Mpaka wakati huo sikua na mawasiliano yoyote na familia yangu na sikua najua kama wananitafuta au wanaamini bado nipo shule. Maisha yangu yote yakusoma sikuwahi kutembelewa na mzazi ata siku moja nikiwa boarding school, hivyo niliamini mzee massawe hana taarifa yoyote kunihusu Mimi.
Nilimwambia Ras kama nipo tayari kwa safari lakini kwa sharti moja, endapo kuna baya lolote litanipata basi aitafute familia yangu. Nilimpa full physical address ya kuweza kumfikisha nyumbani Incase likitokea jambo lolote ambalo litahusu familia yangu.
Kiukweli ilikua ni safari ya nje ya nchi ambayo sikuifurahia wala sikuitarajia nilishangaa furaha aliyokua nayo Ras. Jioni ya siku hiyo tulitoka na kuelekea maeneo ya sinza ambako tulikula na kunywa, baadae tulielekea mitaa ya posta baada ya kukutana na wasichana wawili miongoni mwa wale ambao walikuwepo jana yake kwenye ile Houseparty kule kijichi.
Nililetewa yuleyule ambae alinipitisha rough road jana yake nilitamani kumkataa lakini ilionekana Ras aliongea nao mapema hivyo walijiandaa kwa ajili yetu.
Ugeni wa jiji ulinifanya niisiijue sehemu hiyo ni wapi zaidi ya kukalili kwamba tulikua posta lakini ilikua ni casino.
Ndani tulimkuta McKenzie nilianza kuhisi uwepo wake maeneo ya karibu kutokana na kaharufu ka cologne, baada ya kutulia na kumwangalia vizuri niligundua McKenzie ni zaidi ya baharia. Ras aliniambia hawa jamaa meli yao inapotia nanga bandarini hua wanapewa vibali vya dharula na wanatoka kufanya mambo yao ikiwepo shopping za misosi kama wana shortage ya chakula especially matunda.
Lakini pia kuna services kama kutoa uchafu wa vyakula na uchafu mwingine sio hilo tu pia wanafanya usafi kwenye vyumba vya engine na mengine mengi. Shipping agents ndio wanaratibu kila kitu na shughuli zote hizi hufanywa wakati meli inaendelea kupakua na kupakia container.
Wakati huu McKenzie alinipokea kwa furaha sana na hii ilionyesha tayar alikwisha wasiliana na Ras kuhusu maamuzi yangu. Baada ya kusalimiana na McKenzie nilitambulishwa kwa bwana mmoja mwenye asili ya kiarabu aliyekua amevaa suti aliyomkaa vizuri sana. Bwana huyu alijitambulisha kwa jina la ally, alikua mnene kiasi lakini sio muongeaji kabisa.
Kwa maelezo ya McKenzie, Ally ndio atahusika moja kwa moja na safari yangu. kwani kuanzia mchana wa siku hiyo alikua ananiandalia document zote na vibali muhimu kwa ajili ya safari yangu. Huyu Ally alionekana kuwa na connection kubwa sana lakini pia alikua na kiswahili safi kimenyooka vizuri.
Tulibadilishana namba za simu huku bwana Ally akisema kesho atanitafuta mapema kwa ajili ya maelekezo ya ziada kwenye safari yangu. Kisha ally na Ras waliondoka huku Ras akisisitiza kama hatoludi basi nisijali yule binti niliyekua naye atafanya mpango tutaludi home. Wakati huu Ras alinipa kadi ya bank kwa ajili ya shopping nikiwa nahisi kuna kitu cha kununua ili nijiandae na safari.
Kiukweli sikufurahia kuendelea kukaa pale casino kwani nilijiona watofauti sana na wale waliokuwepo pale hivyo nilimwambia binti tuondoke tuelekee sehemu ambayo nitapata maduka nifanye manunuzi.
Tulitoka posta kuelekea sehemu moja inaitwa morroco kisha tulikunja kulia na kupark sehemu inaitwa shoppers plaza. Binti aliniambia hapo naweza nanunua chochote hivyo tunaweza shuka, yeye alielekea juu akaingia duka limeandikwa touch SPA akaniacha pale nje nikitafakari nianzie wapi.
Sikuingia tena shopping zaidi niliamua kutoka nje kabisa ili kunyoosha miguu kwani nimetumia usafiri wa gari kwa siku nyingi mfululizo. Wakati natembea tembea mitaa ile niliskia mziki kwa mbali kidogo, siunajua watoto wa chuga kwa hip-hop kuna namna nilivutiwa na huo mziki.
Nilisogea mpaka kwenye geti moja na baada ya kuuliza niliambiwa hapo ni msasani club na humo ndani hua kuna shows za watu wanaopenda mziki huo. Nilipoteza mda mwingi eneo hilo kwa kuangalia vijana wakifanya battle na mengine mengi nilifurahi pia kuwaona wasanii kama nikki mbishi, one the incredible na wengine wengi.
Ila kiukweli sikua na amani ya moyo japo nilipoteza mawazo kidogo nikiwa eneo hilo. Niliamua kuludi eneo tulilopark gari ili kumchukua yule binti tuondoke nikapumzike sikuona haja ya kununua chochote. Baada ya kufika eneo lile sikumuona yule binti ikabidi niende lile duka aliloingia, nilikuta akiwa amemaliza huduma zake anajiandaa kuondoka.
Ndani ya lile duka sikuelewa ilikua saloon au kitu gani?? Lakini pia nilikuta mfilipino wa kike akiwa amevalia sare kama mmoja ya watoa huduma ndani ya eneo lile. Walinikaribisha kwa huduma ya massage na huduma nyingine kama kunyolewa nywele sehemu za siri na mengine mengi ila nilihisi wananizingua sikutarajia kama kunaweza kua na huduma ya hivyo kwenye ulimwengu huu.
Tulianza safari ya kuludi kijichi, lakini kutokana na sehemu tuliyokuwepo nilishindwa kutambua kijichi itakua upande gani hivyo yule binti ndie alikua dereva kutokana na uzoefu wake wa jiji.
Tukiwa njiani nilivunja ukimya na kuanza kumuuliza binti baadhi ya maswali kama jina lake na mahali penye anatoka. Anajishughulisha na nini ndani ya jiji hilo.
Alikua anaitwa mage, mwanafunzi ustawi wa jamii, mzaliwa wa dar es salaam na anaishi kimara. Alitabasamu kidogo akasema yeye ni mchaga mwenzangu, alijua mi ni mchaga kutokana na muonekano wangu pamoja na jina.
Ebwana eeeh tulianza kuponda kichaga japo yeye hakua vizuri kabisa ila alijitahidi ukilinganisha wa wengine. Ukaribu wetu ndani ya nusu saa uliongezeka mara dufu mpaka tunafika home tulikua kama wapenzi waliokutana zaidi ya miaka saba iliyopita.
Na usiku huo at least nili enjoy kwani tulipiga show kama wapenzi na sio mtu na mteja wake kama ilivyokua hapo awali.
Asubuhi simu ya kwanza ilikua ni ya ally akinielekeza niende kurasini kuchukua baadhi ya documents zilizokwisha kamilika. Na kwa maelezo ya ally ni kwamba jina ninalotumia kuanzia siku hiyo ni MUSTAPHA ABDUL-QADR MAKUNGU. Hivyo yoyote nitakae kutana nae nimwambie naitwa mustapha na maelezo mengine nitapewa baadae.
Nilimueleza mage kila kitu kuhusu wapi natakiwa kwenda Wakati huo lakini pia nilimueleza majina yangu mapya. Alicheka sana na akawa wakwanza kuniita mustapha, tulienda kurasini nikachukua document zote kisha tukaelekea mwenge kwenye ghetto la mage.
Nilishinda uko siku nzima, nilikula chakula kizuri na tuliongea mambo mengi sana na mage lakini kubwa ilikua ni kumsisitiza kama hana sababu ya msingi ya kufanya shughuli za umalaya aache mara moja.
Ras na mage ndio walinisindikiza siku ya safari yangu mpaka airport huku Ras akitumia uzoefu wake kwenye baadhi ya mambo. mfano kwenye kukaguliwa nyaraka sikua naelewa chochote ila yeye ndio alikua mbele kuhakikisha hakuna sehemu na kwama. Nilijikuta namkumbuka sana mama yangu, nilijiona ni mzambi na msaliti kwa wazazi wangu lakini sikua na namna zaidi ya kuongoza kwenye eneo la kusubiria ndege.
Alituchukua kama masaa matano (5) na dakika 27 kwa Emirates airlines kufika Dubai................
TUKUTANE BAADAE