Mugabonihela
JF-Expert Member
- Dec 12, 2022
- 306
- 1,784
- Thread starter
- #121
Nikiwa kwenye usingizi mzito niliamshwa kwa
Kukanyagwa na safety boots maeneo ya mgongoni. Na safari hii tuliamshwa wote kwa pamoja na kupewa gloves tuvae na Kisha tukashikishwa vile vyuma (spammer) kwa ajili ya Lile zoezi la kukaza zile long bars na short bars.
Wakati huu mvua ilikua inanyesha kubwa mno na
Baridi lilikua kali sana, machozi yalinitoka baada ya
Kukumbuka maisha ya nyumbani especially baada
Ya kumkumbuka mama yangu kipenzi. Nilijiambia
Endapo nitafanikiwa kuponyoka eneo hilo, ningerudi Nyumbani Mara moja na nisinge jaribu tena ujinga ule.
Tuliendelea na zoezi la kukaza vyuma vilivyokua
Vimeshikiria kontena hizo. Lakini wakati huu kazi
Ilikua ngumu kutokana na hali ya bahari kuchafuka
Mvua na mawimbi makubwa. Meli ilikua inayumba kiasi kwamba mtu asingeweza kusimama straight lazima angedondoka tu. Ilikua ni mara yangu ya kwanza kushuhudia tukio mla aina hiyo.
Long-bar moja ilikua na urefu wa Zaidi ya futi15
Huku uzito wake ukiwa ni Zaidi ya kilo30's sasa
Kuinyanyua hii kufika urefu wa kontena mbili au tatu juu halikua swala dogo.Wengi waliishia kuzitupa Baharini kwa kuzidiwa na uzito wake wengine Zikiwapiga kichwani na kuumia vibaya.
Wengi waliumia kwakua hawakua na vitendea kazi
Rasmi kwa shughuli hiyo kama safety boots na kofia ngumu ( helmets).
Kwa mabaharia wenyewe walikua wamevalia full
PPE (personal protective equipment) yan walikua na Kofia ngumu, safety boots, safety belts Kwa baadhi Na overoll zenye reflector.
Kiukweli chuma cha meli ni kigumu tofauti na vyuma Vya kawaida tulivyo vizoea, nilipiigwa mguu wa kulia Chini ya goti nilijikuta nimekaa chini huku machozi Nikishindwa kabisa kuyazuia.
Baridi lilikua kali sana lakini mvua pia ilikua ikinyesha Cha ajabu kila mmoja wetu alitokwa na jasho kwa Zoezi lile. Nilikua mwepesi kwenye kuelewa Maelekezo yote, mfano ilikukaza vile vyuma tulikua Tunazungusha clockwise na kulegeza ilikuani Anticlockwise.
Kilichonishangaza kwenye meli ile ambacho nadhani Ni utaratibu wa meli zote, kulikua kuna daktari, askari na pia kulikua na mafundi wa umeme, mechanic na Taaluma nyingine nyingi.
Hivyo wale walioumia walipatiwa matibabu na
mtaalam wa afya alisisitiza tupewe vitendea kazi na tuwe kwenye full PPE.
Aiseee!!!! Siku ukiwa maeneo ya felly unaenda
Kigamboni na ukaona meli ya konten aina ingia kwa kusindikizwa na zile tag ndogo. Waheshimu sana Wale jamaa mule ndani ya zile meli wanafanyakazi Ngumu sana wanapokua deep
Sea.
Ubize ulikua wa hali ya juu kwa usiku ule, na hapo
Ndio niliona kazi ya zile radiocall ambazo niliwaona Nazo wale mabaharia tuliowafata kigamboni na Kwenda nao kijichi. Kwani kwa ukubwa wa meli ile Ilikua ngumu kuwasiliana kwa njia ya kawaida bali Radiocalls..
Baadae alitoka captain ambae alitoa amri kwa wote Ambao tulikua hatusiki na lashing (kazi ya kufunga na kufungua meli) tuache mara moja. Wale mabaharia waliokua wanatutumikisha walionekana Kuwa wapole sana, kwa haraka nikagundua captain Ni mtu anae ogopeka sana kwenye mambo yale ya Usafiri wa bahari.
Tuliludi kukaa eneo tulilopangiwa tokea mwanzo
Tunaingia ndani ya meli hiyo na wengi tulishukuru
Ujio wa captain yule kwani zoezi lile lilikua ni vita ya kupambana na dhoruba la baharini..
Tukiwa tumepumzika bwana mmoja alitupa story za Mambo ya bahari kwani alionekana kuwa mzoefu Japo kingereza chake kilikua kigumu kueleweka. Lakini point kubwa alikua anajaribu kutuelezwa Nguvu ya captain kwenye usafiri wa baharini.
Kwa maelezo yake ni kwamba captain ndio kiongozi Mkuu ndani ya meli, na mnapokua ndani ya meli Mabaharia hawaruhusiwi kusafiri na wanawake Isipokua captain anaweza akasafiri na familia yake. Ila mabaharia wa kawaida hawatakiwi kuwa na Wanawake na ndio maana wanapotia nanga popote Huwaza wanawake, hii hutokana na ukweli kwamba Wanasafiri umbali mrefu bila kuwaona kabisa wadada.
Alienda mbali Zaidi kwa kusema meli nyingi za karne Hii ya 21 unakuta ndani ya ile crew yao kunakua na Ma gay ata wawili. Hawa huwa ni chakula kwa wenzao, Na mabaharia wengi kazi zao hua ni za mikataba mifupi mifupi na popote pale mkataba utakapoishia basi utashuka kwenye chombo kisha watapanda wengine.
Story zilikua nyingi tulicheka kwa pamoja japo wengi Tulionekana kucheka kicheko cha uchungu
Uliosababishwa either na fatiki au mawazo ya kule
tunapoelekea.
Nikiwa ndani ya blanket nilikumbuka matukio mengi Ya ajabu niliyowahi kuyafanya kuanzia MAKOKO SEMINARY, KIZUKA SEKONDARI na kisha SENGEREMA SECONDARY. Niliamini hayo ndio yalikua malipo yangu kwa uhuni niliowahi kuufanya ambao Haukua na tija wala faida yoyote.
Nilimkumbuka Merry toka siku tunakutana maeneo Ya sengerema na kisha kumbukumbu ilinipeleka Mpaka siku tuna agana stand ya msamvu morogoro. Kisha masaa kadhaa mbele kupata taarifa ya kifo chake.
Niliingiza Mkono Mfukoni Na Kutoa Hereni zake
Ambazo aliziacha siku ile room tukiwa kwa ras, niliamini ile ilikua ni kumbukumbu tosha niliyoachiwa na merry ( kwa sasa hereni hizo anazivaa mke wangu japo sikuwahi kumpa uhalisia wa hereni hizo, hua anashangaa tu kwanini ni hereni flani local and cheap ila nazipenda sana)
kwa kipindi hiki nilitamani Second chance ya kuishi na wazazi wangu ili niwaonyeshe ni kwa namna gani nimebadilika.
Kiukweli kwa wakati huo nilikua naiangalia dunia
Kwa jicho linguine kabisa. Usiombe uwe kwenye
Situation kama hii kwani hutoona maana ya kuzaliwa kabisa.
Mpaka wakati huo sikuona tena thamani ya maisha yangu, nilimkumbuka mzee massawe ambae Mara Nyingi alikua mkali lakini bado kwa ukali wake Hakuacha kunilipia ada akisisitiza nisome.
Nilimkumbuka mama ambae alijitahidi kuhakikisha
Napata chakula hasa wakati ninapochelewa kurudi
Nyumbani huku mzee massawe akiacha taarifa
Nisipewe chakula niende nikale nilipovutia bangi
Zangu.
Nilikuja Kustuka Baada Ya Sauti Niliyoiskia kwambali ikiita "kunta! Kunta! Kunta! Hey little boy from Africa, good morning?"
Ilikua ni rafudhi ya kimexico hapo niligundua alikua
Ni yule Mzee mwenye pama. Ilikua ni asubuhi lakini Hatukuweza kuliona jua sijui ilikua ni mawingu au Bado hakuja pambazuka vizuri. Ile ya dhoruba la usiku hali ilikua imetulia Lile dhoruba la usiku lilipotea kabisa huwezi amini Kama usiku huo hatuku pumzika kwa kupambana na Upepo mkali.
Baada ya kuwa kumekucha vizuri walichukuliwa
Baadhi yetu kuelekea sehemu ambayo nadhani ndio Kulikua na jiko. Jamaa wale waliludi na chakula, Ilikua ni mikate pamoja na mapande makubwa ya samaki.I likua ngumu kutambua alikua ni samaki gani kwani yalikuani mapande makubwa usingeweza kuona ata miba ya samaki yule.
Tukiendelea na chai alikuja Miguel katika namna
Kama ana tuhesabu, hapo mwanzo tulikua 14 lakini Ata mimi nilistuka baada ya kuona tupo 12 pekee.
Miguel aliuliza wenzetu walipo lakini hakukua na
Mwenye majibu.
Ni yule jamaa ambae usiku alikua anatupa story za Mabaharia na maisha ya baharini kwa ujumla ndio Sikumuona wakati huo. Alionekana kuwa mzoefu Kidogo kwenye mambo ya bahari, nilimshuhudia Miguel akija na askaria mbao hapo mwanzo Sikufanikiwa kuwaona na sikujua askari hao walikua Wapi muda wote.
Nikawaida sana meli hizi za mizigo kutembea na
Askari ndani yake tena makomando kabisa kwani
Miaka hii kumekua na wimbi kubwa la shughuli za
kiharamia. Hasa kwa meli zinazokuja ukanda wetu huu wa Pwani ya Africa mashariki pia zina desturi hiyo. Kwani pwani ya somaria mpaka Mombasa inasifika pia kwa uwepo wa wazee wa kazi Yaani pilates.
Ndio maana meli inapotia nanga tu kwenye Bandari Ya dar es salaam utaona gari ya jeshi ya navy kigamboni itaenda kwenye meli husika.
Story zinasema jamaa wanaendaga kuchukua silaha za Askari ambao wanakuwepo kwenye meli hiyo.
Baada ya kushuka askari kwenye meli zinazoingia
Bandari ya dar es salaam anaefata anakua ni daktari Kwa ajili ya kuangalia afya za mabaharia na mwisho Kabisa ni afisa wa uhamiaji.
Nimetoa maelezo haya ilituone kwanini ndani ya
Meli hizi unakuta kuna makomando ndani yake.
Miguel alikuja na askari wale ambao walikua na
Mbwa watatu walioshiba lakini cha ajabu tokea
Tunapanda meli hiyo hatukusikia mlio au mbwa
akibweka. Ila baada ya mbwa wale kuja eneo ulilopo walianza kubweka huku wakiwa wameshikiliwa kwenye kamba.
Baada ya muda mbwa wale waliachiwa nakuanza kuzunguka Meli nzima especially maeneo yaliyokua yamejificha. Ilionekana wale mbwa ile ndio ilikua kazi yao yaan Kutafuta watu ambao walidhaniwa kuwa ni wazamiaji.
Hazikupita dakika 10 wale askari walikuja wakiwa
Wame wakamata jamaa wawili ambao Hatukuwafahamu kwa majina lakini mmoja wao
Alikua ni yule aliyekua anatupas tory usiku.
Miguel alitoa bastola kiunoni na kumshuti mmoja
Wao kifuani kisha ikatoka amri atupwe ndani ya maji.
Hapa sasa nilianza kuiona sura halisi ya Miguel
Alikua kijana mdogo lakini katili sana.
Mwingine aliyebaki alivunjwa mikono kuanzia maeneo ya Begani kwa vyuma vinavyojulikana kama twist lock na Kisha kutupwa baharini pia. Huyu yeye alitupwa mzima lakini mikono ilivunjwa so alikua ni wakufa tu kwani asingeweza kujitetea kwa namna yoyote.
Miguel: ofcourse I want to show you how cruel I am.
Aliongea maneno hayo tu na kuondoka bila kugeuka Nyuma huku akionekana amekasilika sana kwa Kitendo cha jamaa wale kujaribu kumtoroka.
Jambo lile lilituacha midomo wazi kwani
Hatukutegemea kama angefikia huko kwenye
kuuana. Kulikuana kimya cha takribani dakika 20,
watu wakionekana kutafakari kitendo kile kwani bila shaka wote tulijua tunapoenda ni kweli hakuna
Amani na tunaenda kufanya kazi ngumu.
Lakini hatukufikiri kama ata sisi hatuna thamani
Kiasi hicho. Mzee wangu wa ki Mexican alitoa pakiti Ya sigara iliyoandikwa CARIBE ambayo ilionekana ni sigara pendwa Sana kwa nchi za American ya kusini hususani Colombia, Peru, Chile na kwa uchache sana Cuba. Inazalishwa na COLTABACO huku piece moja ikifikia urefu wa Mpaka 82mm.
Alitoa pakiti hiyo akajaribu kuchungulia kama kuna
Chochote kimebaki hatimae alikuta sigara moja
Akaitoa na kisha kuiwasha. Alivuta kidogo na kunipa,
Sikua mtumiaji wa sigara lakini sikuona sababu ya
Kukataa kuvuta nilivuta kidogo na kumpatia jilani
Yangu mwingine. Sigara ile ilitembea kwa pafu moja mpaka pafu mbili Kwa kila mtu kati yetu wote 12 kisha ikamfikia tena Mzee yule m Mexicana. Ilipofika kwake alisimama Katikati yetu, kisha kwa lugha nisiyo itambua Aliongeamaneno ambayo baada ya kutafsiriwa hii Ndio ilikua maana yake.
"Tulikua 14 na sasa tupo12, sababu ya kupungua
Kwetu ni vifo ambavyo naweza sema wenzetu Wamejitakia . Sasa sigara hii imetuunganisha kuwa Kitu kimoja, hakuna asiyejua kuwa tunapoenda kuna Hari mbaya kuliko hapa. Labda kwa upande wa kunta Ye ni kipofu kabisa, kwa kumuona tu anahisi Tunapoenda ni sehem ya kupumzika na kushusha Shida zake. Kwa umri wangu huu nawaomba Tusijaribu kufanya lolote linalohusu kukimbia kwa Kufanya hivyo tutaisha, Miguel nimemjua miaka Mingi yeye ni Zaidi ya baba yake.
Likini kwa pamoja tuungane kumfariji kunta kinte
Kwani umri wake bado mdogo sana asipoteze Energy nyingi kwenye kulia usiku kucha bado ana Nafasi kubwa.
Alimaliza kwa kusema atakua mkali Kwa yoyote atakae onyesha kukata tamaa, kwani Mpaka wanaenda huko walisha kata tamaa ya Maisha ya mtaani hivyo ni Zaidi ya dhambi kukataTamaa mara mbili.
Wengi walimsikiliza kwa utulivu sana lakini kwa Upande wangu maneno yale yalinikumbusha mzee massawe ambae Mara nyingi nikiwa katika umri Mdogo aliniita mwanajeshi wake.
KWA AMBAO WATATAKA KUISOMA KWA HARAKA ZAIDI WA MUONE 0623329512 Whatsapp