Utajiri wa Magofu ya Rapta

Utajiri wa Magofu ya Rapta

Juu ya maturubai hayo makubwa yalianikwa majani mabichi, yaani kama ambavyo tunaanika mahindi au mazao mengine ndivyo ambavyo hawa jamaa walianika majani hayo.
Wote kwa pamoja tulikusanyika chini ya banda moja kubwa la mbao lililo funikwa na turubai kwa juu. Tukiwa hapa sasa nilimuona baba yake na Miguel akija eneo tulilo fikia.

Kwa mbali tuliona watu, watu walionekana kuwa wanatokea mashambani na walikua na mizigo mgongoni.

Mizigo ile ilikua ni aina ya viroba vikubwa, walielekea eneo lile la uwanja na kushusha mizigo ile na kisha kuendelea kuisambaza eneo zima.

Wote tuliowasili siku ile tulionekana kuwa wageni wa kile kilichokua kinaendelea eneo lile. Na yoyote angetambua hilo kwa namna ambavyo tulikua bize kushangaa shughuli hizo.

Daniel alikuja tena eneo hilo akiwa vijana wanne waliokua wamebeba maboxi makubwa lakini hayakua mazito kabisa kwa kuyaangalia tu.

Vijana wale walionekana wamechoka sana kwa kuwaangalia, suruali zoa hazikua na mikanda hawana mashati wakati huo wenye mashati mengi yalikua yametoboka au kuchanika kabisa.

Idadi kubwa ya wafanyakazi waliokua pale walikua ni weupe kwa muonekano. Na weusi niliowaona walikua na weusi ule wa design ya half-caste.

Kiukweli kila aliyekua eneo hilo alikua amechoka sana isipokua nafuu ilikua kwa viongozi ambao nao walionekana ni addicted pia kwenye matumizi ya unga.

Jamaa wale waliokua wamebeba maboxi walifika na kuacha chini maboxi kisha wakatokomea mashambani.

Niligundua eneo hilo halikua na utaratibu wa kusalimiana hovyohovyo. Utaongea na Mtu kama kuna sababu ya msingi la sivyo fanya majukumu yako mengine.

Hakukua na nafasi ya kupiga soga hovyohovyo muda mwingi waliutumia mashambani.

Kulikua na ulevi wa kipundukia pia, tulipofika hapo kulikua na kila dalili ya kuwepo kwa kila aina ya pombe.

Kwa muonekano wa wafanyakazi wale sikutaka kuamini kama wanalipwa kabisa. Mbaya zaidi walikuwepo mabinti ambao ilikua ngumu kujua kama ni wasichana au wazee.
Kama tunavyojua America ya kusini ilivyojaaliwa warembo lakini sio kwa warembo wale waliokua hoi wasingenivutia ata iweje.

Akati nipo kwenye mawazo ya kuwafikiria mabinti wale kwamba wasingenivutia kumbe kila mmoja wetu aliwaza hivyo.

Daniel aligundua hilo na akatukanusha kwa kusema pale ni kama bar au club, wakati unaingia bar utaona wanawake wote wabaya na hawatakuvutia. Lakini ukiwa kwenye bia ya sita au ya saba utaona walewale mabinti wameanza kuwa warembo.

Hivyo ata sisi baada ya mwezi tutaanza kuwa sumbua kwa kutaka kuchakata mbususu zao. Lakini Daniel alitukumbusha kuwa eneo hilo lina maambukizi makubwa ya ukimwi na waliouleta ni haohao tunao waona mabinti wabaya.

Na wengi walioupatia ukimwi hapo hawapo tayari kuondoka eneo hilo na watafia hapo na kuzikwa hapohapo.

Wakati tunaanza safari kule Cabo de la vela, hawa wafanyakazi wenzangu niliwaona wamechoka sana na ni kama watu wasio na matumaini ya kuishi. Lakini baada ya kufika hapa niliwaona kama watu wenye afya na nguvu zaidi.

Nilidhibitisha hili baada ya mkulima mmoja kupita na mwenzake huku wakiambiana kua wanaona nguvu mpya imeingia.

Baba yake na Miguel alisimama mbele yetu na kuanza kusoma majina, lakini kabla hajaanza,
BABA MIGUEL: mustapha!! I thought you dead at sea.
( Mustapha nilijua umefia baharini)

MIMI: no Dad I am still alive
( Hapana baba, Bado nipo hai)
BABA MIGUEL: shut the https://jamii.app/JFUserGuide up, I'm not your dady
(Funga bakuri lako mi sio baba ako)
Wenzangu walicheka sana waliamini naanza kujipendekeza ili nisipitie ule msoto unaoonekana unaendelea eneo lile.

Baba Miguel aliamini mimi ni miongoni mwa wale waliotoroka kwa kua nilionekana kutoridhika kuwepo eneo lile.

Hapa tuligundua kuwa Miguel alitoa taarifa baada ya kuwaua jamaa wale waliokua wanajaribu kumtoroka.

Kila aliepita eneo lile alikua ana niangalia sana mimi kuliko wale wenzangu.

Baba Miguel aliendelea kuita majina kwa kutumia list yake ili kuhakikisha hakuna mtu yoyote alietoroka. Na ilikua ukiitwa jina unasogea mbele na kupewa blanket pamoja na gumboots.

Wote tulipewa vitu hivyo na zoezi liliishia pale, kulichofuata ni kuonyeshwa eneo ambalo tutalitumia kwa ajili ya kulala.
 
BABA MIGUEL: shut the JamiiForums' Community Engagement Guidelines | Mwongozo wa Ushiriki kwenye Mijadala up, I'm not your dady
(Funga bakuri lako mi sio baba ako)
Wenzangu walicheka sana waliamini naanza kujipendekeza ili nisipitie ule msoto unaoonekana unaendelea eneo lile.

Baba Miguel aliamini mimi ni miongoni mwa wale waliotoroka kwa kua nilionekana kutoridhika kuwepo eneo lile.

Hapa tuligundua kuwa Miguel alitoa taarifa baada ya kuwaua jamaa wale waliokua wanajaribu kumtoroka.

Kila aliepita eneo lile alikua ana niangalia sana mimi kuliko wale wenzangu.

Baba Miguel aliendelea kuita majina kwa kutumia list yake ili kuhakikisha hakuna mtu yoyote alietoroka. Na ilikua ukiitwa jina unasogea mbele na kupewa blanket pamoja na gumboots.

Wote tulipewa vitu hivyo na zoezi liliishia pale, kulichofuata ni kuonyeshwa eneo ambalo tutalitumia kwa ajili ya kulala.
Mkuu nitag na mm🤩
 
Ndani ya camp hiyo ya mashambani nilipewa room namba 18 ambayo ilikua juu kwenye kibanda cha gharofo moja ya mbao. Room ile ilikua karibu kabisa na uwanja ule uliotumika katika kuanika majani yale ya coca.

Nilipoingia ndani ya room ile kulikua na vitanda viwili vyenye magodolo ya sufi. Kitanda kimoja kilikua upande wa kulia huku kingine kikiwa upande wa kushoto. Kile cha upande wa kushoto kilionekana dhahiri kuna mtu yupo anatumia kitanda hicho kwani kilikua na blanket na kitabu (Bible) upande wa kichwani yaani kwenye mto.

Kulikua na pillowcase iliyotumika kama begi sababu ndani yake kulikua na nguo. Kwa haraka niligundua anaye lala hapo ni dhahiri alikua at least na hofu ya mungu.

Niliweka blanket langu juu ya kitanda cha pili ambacho kilionekana kua wazi kisha nikaweka na zile gumboots kwa chini. Niliamua kujilaza ili kuhakikisha naondoa ule uchovu wa safari yangu ya kutoka dar es salaam mpaka dubai kisha Colombia hatimae hapo Peru.

Apa unachotakiwa kujua ni kwamba zao la coca kwa nchi za America ya kusini wanali treat kama zao la biashara. Na nchi hii ya Peru ndio inaaminika kuwa ndio nchi inayoongoza kwa uzalishaji wa zao hili.

Kwa nchi ya Peru, Kilimo cha zao hili kimegawanyika sehemu mbili, yaani kuna kile kilimo cha halali na kile kilimo ambacho si cha halali ( licit and illicit cultivation).

Kilimo cha halali ni kile kinachofanywa na wakulima ambao wapo kihalali na wamesajiliwa na chama cha ushirika cha National Coca Monopoly (ENACO).
National Coca Monopoly chama hiki hufanya biashara na wakulima waliosajiliwa kisheria. Wao hununua na kuuza coca kutoka kwa wakulima hususani wale wakulima wadogo wadogo.

Mchakato huu wa kununua na kuuza kutoka kwa wakulima wadogo wadogo hufanywa either domestically ( ndani ya nchi) au nje ya nchi ( export).

Kwa matumizi ya ndani mara nyingi wanatumia kwa kutafuna tu kama vile tulivyoona kwa Daniel wakati tupo ndani ya helicopter kutokea kisiwani. Au wengine hutengeneza chai maarufu kama herbal tea kwa matumizi ya kawaida ya kila siku.

Lakini linapokuja swala la exports ( kuuza nje ya nchi) mara nyingi huuzwa kwa makampuni yanayo tengeneza vinywaji (soft drinks), flavoring au hata kwa pharmaceuticals.

Apa kwenye soft drinks tupaache tusije kuharibu biashara za watu, lakini unachotakiwa kujua ni kwamba coca plant ni highly addictive stimulant. Unakuta mtu akikosa kinywaji fulani cha kawaida tu anakosa amani siku nzima au atakitafuta popote, hahahahah that's coca plant broh.

Apa kwenye licit cultivation au wale wakulima halali waliosajiliwa kisheria wengi wanapatikana jimbo moja linaitwa Cuzco ambapo zaidi hekari 18,000 zimesajiliwa kihalali kabisa ndio maana pale mwanzo nilisema hili ni zao la biashara kwa nchi hizi za America ya kusini.

Kuna familia nyingi sana zinaendesha maisha kwa kilimo hiki cha coca, kwa upande wa wakulima wadogo wadogo wengi hutumia family labour kwenye michakato yote kuanzia kupanda mpaka ile hatua ya kuanika ili kupata the dried coca leaf.

Kwa upande wa pili yaani illicit cultivation ( kilimo ambacho si halali) hawa ndio wale mabwana ambao wapo wanaendelea na kilimo lakini hawapo kisheria au sheria haiwatambui kabisa.

Na hawa ndio wanamashamba makubwa sana lakini yapo maeneo ambayo hayafikiki kirahisi na wanatumia gharama kubwa kuyaendesha mashamba hayo. Kutoka kwenye mashamba haya ndio zinatengenezwa products kama cocaine na wamiliki wa mashamba haya hua ni mabilionea wakubwa.

Mara nyingi mashamba haya ambayo ni illicit au sio halali yanapatikana sehemu kama (UHV) upper haullaga Valley kaskazini mwa nchi hiyo ya Peru kwenye majimbo kama San Martin, huanaco na ucayali.

Lakini pia mashamba hayo yanapatikana sehemu za bonde linaloitwa La Convencion na Lares ndani ya jimbo la Cuzco, jimbo la Huanta na La Mar kando ya Rio Apurimac jimbo la Ayachucho.

Ukiacha maeneo hayo kuna maeneo kama ya Puno na Pasco yenyewe wanalima lakini sio kiviiile.

Hapa eneo la upper haullaga Valley udongo wake upo well drained na una iron ya kutosha sana jambo hili linapelekea maeneo haya kua potential kwenye uzalishaji wa zao hili la coca.

Maeneo mengine ambayo yanalima sana coca America ya kusini ni Bolivia na Colombia, sina habari nyingi sana kuhusu Colombia na Bolivia kwani sikubahatika kabisa kujishughulisha na shughuli hizi nikiwa uko.

KWA PDF ZA HARAKA ZIKIWA NA PICHA TUMUONE 0623329512 kupitia whatapp tusimpigie simu namba ipo whatapp (malipo ya PDF ni 2000 kwa simulizi yote)
 
Eneo hili la camp kulikua na shughuli nyingi zinaendelea huku wafanyakazi wamegawanywa kulingana na majukumu yao.

Kuna baadhi walikua mashambani huku baadhi wakiwa upande ule wa processing, hawa wa processing ndio walikua jikoni sasa maana huu upande wao ndio umehusisha taaluma au utaalamu mkubwa.

Kimsingi eneo hili lilikua kimya sana kilichosikika ni shughuli za watu pekee na sio kelele nyingine zozote.

Niliamshwa na bwana mmoja aliyekua amekaa kitanda cha pembeni yangu, bila shaka bwana huyu ndie alikua anayelala kitanda hicho. Alikua mwanaume wa makamo mwenye asili ya ki-Asia aliyekua na nywele nyingi zilizotimka na ndevu zilizokosa matunzo kabisa.

Kwa haraka haraka ningeamua kupekua nywele zile nisingekosa chawa, bwana huyu alikua mpole sana nilipomuona tu nilifurahi kupata jilani wa design hiyo. Kwani nilipomlinganisha na wale niliowaona nje hapo huyu alionekana kua amestaarabika sana.

Aliongea kwa upole sana,

"Hey teen time for food"
(Muda wa chakula dogo)

MIMI: thanks!! This is mustapha, what should I call you please
(Asante!! Naitwa mustapha, naweza kukuita nani)

" This is Javier, go and take the meal"

Bwana yule alisema anaitwa Javier, na alinisisitiza nikachukue chakula kuonyesha hataki maongezi zaidi.

Nilitoka nje kuchukua chakula lakini sikukielewa kabisa kile chakula kuanzia ingredients mpaka radha ya chakula ilinishinda kabisa hivyo sikuchukua muda nililudi ndani kuendelea na usingizi wangu.

JAVIER: why is it so fast???

Rafudhi na kingereza cha Javier kilinipa shida sana kumuelewa, lakini mwisho wa siku tulikua tunaelewana.

Alishangaa kwanini nimeludi mapema,

MIMI: I don't like the food
(Sijakipenda chakula)

JAVIER: so you don't use cocaine
( Kwaiyo wewe hutumii cocaine)

MIMI: yes I don't
(Ndio situmii)

JAVIER: I'm very sory Young Man from Africa, here coca is a food ingredients.
(Pole sana kijana, hapa kwetu cocaine ni kiungo cha chakula)

Wapishi wa maeneo haya especially eneo hili la kambi tuliyofikia hutumia coca leaf au majani ya coca kutengeneza chakula Mfano:
Vitu kama chocolate, ice-cream, na cakes lakini vyakula kama pasta, tamales na hata tempura inayotumia unga wa majani ya coca.

Baadae tutaelezana Mambo baadhi kuhusu vyakula hivyo apo vinavyotengezwa kwa coca leaf, hili sio jambo geni kwani kuna Cake pia hutengenezwa kwa majani ya bangi, na zenyewe nitakuja kuzielezea.

Aliniangalia kwa makini sana kisha akauliza" how did you get here"

Kabla sijamjibu swali lake aliondoka na kuniacha ndani mule peke yangu, kwa maelezo ya Javier niliamini wale wafanyakazi wote ni kama watumwa wa madawa. Hivyo kwa kupewa chakula kile iliwatosha sana kupunguza alosto walizotengenezewa na mabepari wale wamiliki wa mashamba hayo ya coca.

Nikiwa nimejilaza kitandani naangalia juu ya paa la Banda lile la gharofa moja iliyotengenezwa kwa mbao. Niliona baadhi ya vitu vikiwa vimening'inia juu ya mbao zilizoshikiria paa hilo.

Niliona baadhi ya nguo za ndani mablanket makubwa mawili yaliyochoka sana. Kwa uwepo wa vitu vile niligundua vilimilikiwa na mtu ambaye alikua analala kitanda hicho.

Nilisubiri Javier aludi ili niweze kumuuliza habari za mtu huyo, je!!! Alifanikiwa kutoka eneo hilo au ilikuwaje?

Zilipita dakika 10 mbele nilimuona Javier akiingia na chakula, kilikua ni chakula maarufu sana kwa ukanda ule wa Peru. Chakula kiliitwa CEVICHE kilikua na taste nzuri sana na mchanganyiko wa vitu vingi lakini kwa haraka niligundua uwepo wa samaki aliepikwa kwa ustadi wa hali ya juu.

Nilikishambulia chakula kile kwa speed ambayo hata yeye mwenyewe alishangaa, kiukweli nilitumia mda mwingi au ulipita mda mrefu sijala chakula chenye taste nzuri kama hiyo.

Nilikua na maswali mengi kichwani, ni kwa namna gani alipata chakula kile ambacho kilionekana exceptional na unique sana kwa maeneo yale.

Niliishia kwa kujiambia kichwani kwamba inawezekana jamaa amebebwa na ukongwe wake wa kuwepo pale.

Niliamini hivyo kwani ata kipindi ni boarding schools especially hizi za serikali inawezekana siku hiyo ratiba ya shule inasema tutakula dona maharage lakini kuna baadhi unakuta wanapiga wali.

Hivyo nilihitimisha kwa kuamini bwana Javier anabebwa na ukongwe wa kuwepo hapo mda mrefu.

Wakati nakula msosi ule nilimuuliza, swali bwana Javier.

MIMI: Javier, where is your food
( Chakula chako kikowapi wapi Javier)

Javier aliniangalia kisha akaludisha macho kwenye kitabu chake.
JAVIER: You think what you eat is yours.
Daaaaah!!! Nilijiona mjinga sana, kwani chakula kile ilionyesha wazi ilikua ni share yake hivyo aliileta pale ilitule wote lakini mimi nilifakamia kama changu.

Hivyo kwa siku ya kwanza tu tayari nimeonyesha character ya uchoyo kwa room mate.

Nilisogea na chakula kile kikiwa kimebaki kidogo hadi kwenye kitanda chake ili tule pamoja sasa. Lakini Javier aliendelea kuwa busy na kitabu anachosoma, zaidi aliongea tena maneno yenye ukweli unaoumiza sana.

JAVIER: you seem to regret your behavior, it's not your fault young man. Africans are bred for greed, that's why they don't make any of developments for centuries.

( Inaonekana kama unajuta, ila usijali sio kosa lako. waafrika wengi mmekuzwa katika uchoyo)

Kiukweli sikua na namna ya kuipinga kauli ile kwani kila kitu kilikua wazi. Aliendelea kwa kwa kuniambia kama kitanda hicho nilicholala kilikua kinatumika na kijana mmoja wa kiafrika kutokea Western Bahr el Ghazal ( south Sudan).

Aliendelea kwa kusema tunafanana sana tabia na yule kijana, waafrika wote ni selfish!! Ndio maana ata viongozi wanapochaguliwa tu, cha kwanza kabisa wanawaza matumbo yao, familia zao na kisha kabila au mkoa anapotoka.

Mpaka wapiga kura wenyewe wanathubutu kumcheka au kumshangaa kiongozi ambaye atamaliza muda wake madarakani bila kufanya lolote kwao.

Hapo nilikumbuka jambo moja tulilowahi kulizungumzia hapo nyuma kwamba watu wanamshangaa Nyerere kwa uzalendo uliompelekea mpaka sasa ridhiwani hafanani na makongolo.

Nilijihisi mwenye hatia sana siku ile kwa maneno yale japo yalikua na ukweli usiopingika.

JAVIER: what country do you come from in Africa
(Unatokea nchi gani afrika)
MIMI: Tanzania

JAVIER: my grandfather used to live there around 1950's
Baada ya hapo aliahidi kunipa stories za Babu yake huyo ambae kwa haraka tu aliishi mkoa wa Lindi (nditi). Ametunza address hizo akiwa anaamini kuna siku na yeye ataludi huko.
 
Back
Top Bottom