TUENDELEE WAPENDWA
Wakati ninyanyuka nikimfuata mzee shahzad kwa ajili ya kuelekea msikitini kuna namna fatemeh aliniangalia. Na mimi nilipomuangalia usoni alinikonyeza huku akinizomea nadhani alimaanisha niende nikapambane na hali yangu huko msikitini.
Fatemeh alijua sikuwa muislam wala nilikua sijui ata waislamu wanasali vipi hivyo ile ilikua ni ishara kwamba nikawe makini wasinistukie.
Unajua eneo kama hukuwahi kuingia na unahisi kuna miiko yake lazima kuna namna ya uoga itakuingia. Na kiukweli nisingeweza kusema mimi sio muislam ingezua maswali mengine mengi kwa mzee yule.
Lakini pia baada ya kumuona ana chembechembe za udini ningesema sio muislam lazima mambo yangekua magumu upande wa ushirikiano.
Hivyo basi nilisimama kinyonge huku fatemeh akinicheka na kunizomea, for sure fatemeh alianza kunizoea sana na ata mimi nisiwe muongo nilishamzoea sana.
Tulishuka taratibu mimi na shahzad wakati huu fatemeh alibaki ndani ya maktaba ile yeye sikuona akijishughulisha na kwenda msikitini.
Lakini ata hivyo shahzad aliniambia mimi tu nadhani kwa wanawake sio lazima sana kwenda msikitini kama nitakua nimekosea nitasahihishwa kwa kauli hii.
Msikiti haukua mbali kabisa na maeneo yale lakini pia kwa bahati mbaya sana wakati tunaelekea msikitini mzee huyu hakuongea chochote njiani sasa sijui ndio utaratibu au vipi kwani alikua bize na rosary yake mkononi akihesabu zile pingili.
Tulipofika karibu na msikiti tulikutana na bwana mdogo ambaye bila kukosea alikua ni mjukuu wa shahzad. Hivyo basi tuliongozana nae mpaka ndani ya msikiti ambao haukua mbali kabisa na maktaba ile.
Kwakua nilikua mgeni na sielewi chochote kuhusu maswala ya msikiti niliamua kujiweka nyumanyuma kidogo ili niwe na copy na ku paste zile process zote ambazo zilikua zikiendelea Ndani ya msikiti ule.
Kwanza kabisa tulipita kwenye korido ambayo ilikua na mabomba mengi sana, kitu kingine hawa jamaa misikiti yao viatu hawavui nje yaani kuna sehemu maalum ipo pembeni ya korido ile kwa ajili ya kuwekea viatu.
Watu waliongia wengi walielekea kwenye mabomba na kuosha sehemu za miili yao kama mikono miguu na vichwa. Lakini kuna namna kama walikua wanaviosha viungo hivyo kwa utaratibu au kwa kufuata mtiririko wa kueleweka.
Wakati nipo pale natafakari nianzie wapi, wapo baadhi ( wachache sana) waliokua wanapita bila hata kupita kwenye yale mabomba na kuosha viungo vyao kama walivyokua wale wengi.
Nilivyoona wapo wanaopita na kuingia ndani bila kuulizwa ahahaa mzee baba nikazama ndichi, kufika ndani nikakuta jamaa wamejipanga mstari mnyoofu huku wamesimama kama askari mikono ikiwa inang'inia.
Kilichofuata hapo ilikua ni kugeza kila hatua na nilifanya hivyo baada ya kutafuta angle ya pembeni kabisa nyuma ya mistari ile.
Kilichokua kinaendelea pale ilikua ni kuangalia majority, yaani wakiinama tunainama wote wakiinuka tunainuka wote mpaka misa ilipoisha.
Na nilivyoona watu wanatoka na mimi na kanzu langu taratiiibu nikawa najisogeza kwa nje. Nilipofika nje nikagundua mzee shahzad yeye alikua bado yupo ndani hivyo nilichukua sandals zangu nikaweka pozi maeneo ya karibu na mlangoni nikawa nawasikilizia watoke ili tuondoke.
Basi wakati nipo pale nje bwana, aslaam aleykum zilikua nyingi mpaka nikawa nataman nibadilishe location lakini sasa nilihofia kupotezana na shahzad na mjukuu wake.
Kilichonishangaza zaidi maeneo yale ni kwamba ukifika muda wa sala watu wanakua wengi msikitini yaani unaweza kukosa ata position ya kusimama.
Kulingana na sensa iliyofanywa na serikali ya Iran mwaka mmoja nyuma ya mwaka huo yaan 2011, takwimu zilionyesha karibia asilimia 99.98% ya wananchi wa Iran ni waislamu.
Na bado takwimu zilidai katika waislamu hao bado asilimia 85 wanapatikana kwenye dhehebu lililoitwa Shia na huku asilimia 11 wakiwa ni wale wa Sunni. Hawa sunn nadhani tunawajua, hawa ndio wale wazee wa kazi unakuta suruali zao zinaishia kwenye magoti na wanamsimamo sana.
Sunni na shia ndio madhehebu makubwa ya uislam kama kuna mengine niweke wazi siyajui hayo mengine.
Ukija katika nchi ya Iran wengi wa wafuasi wa kiislamu wanapatikana kwenye dhehebu hilo la shia na hao wengine yaani Sunni wengi hupatikan sana kwenye nchi za kiarabu na maeneo mengine ya middle east.
Na ni bora kabisa shahzad hakuniuliza mimi ni dhehebu gani kati ya hayo kwani lazima ningezingua. kwa maana hapo kabla sikua najua kabisa madhehebu hayo mpaka pale nilipo ambiwa na fatemeh.
Yaani kama shahzad angeniuliza dhehebu langu basi ningemwambia mimi ni bakwata maana nilishazoea bongo kusikia kuna waislamu wa bakwata na sunni. Ila kumbe kwa bahati mbaya hakuna dhehebu kwenye uislam linaitwa bakwata.
Mzee wetu shahzad alitoka na kijana ambae niliamini alikua ni mjukuu wake na wakanikuta nikiwa pale nje nawasubiri.
Shahzad alisema tunatakiwa tuende nyumbani kwake ili nikapajue na alikua anatumia kiswahili kitu ambacho kilimfanya mjukuu wake asielewe kabisa maongezi yetu.
Nilimuuliza vipi kuhusu fatemeh akasema nimpigie simu, nilipomuambia sina simu alimuomba mjukuu wake anipe simu ili nimpigie bado nikawaambia sina ata namba yake.
Mzee shahzad alicheka sana akaniambia, "bwana mdogo acha tabia za kizaramo sijui za kipemba upo kwenye nchi ya watu hii unatembeaje bila mawasiliano".
Kiukweli niliona alichokisema shahzad kilikua ni ukweli mtupu hivyo nilipanga tukionana cha kwanza kabisa natakiwa kumwambia fatemeh anipe namba yake ya simu.
Kwa kuwa maktaba haikua mbali niliwaomba nimfuate fatemeh ili nije tuongozane kuelekea kwenye nyumba ya mzee huyo.
Mzee alinikubalia lakini huku akinisema kwamba amezoea watanganyika wajanja wajanja sasa anashangaa mi mtanganyika wa wapi nimezubaa namna ile.
Wakati nakaribia nje ya maktaba nilikutana na fatemeh akiwa nje na yeye alikua anatusubiri ili tukaendelee.
FATEMEH:why are you alone?
( Mbona upo peke yako)
MIMI: the old man welcomes us to his place
( Mzee anatukaribisha kwake hivyo nimekufuata)
FATEMEH: OK, but when we arrive there, we should explain our problem in advance
( Sawa ila tuifika tueleze shida yetu mapema)
Ata mimi niliwaza hivyo hivyo kwamba tunatakiwa kueleza shida zetu mapema kwani mzee yule alikua mswahili sana yaani maneno mengi mno mengine yana maana mengine ndio hivyo tena.
Hakukua na umbali wowote kutoka tulipokua mpaka pale walipokuwepo shahzad na mjukuu wake hivyo tulifika mapema na kisha tukaingia kwenye gari kuelekea kwenye mji au nyumba ya shahzad.
Kama kawaida yake shahzad story zilikua za kutosha aisee yule mzee anasound mlima kuna muda aliniuliza kuhusiana na kiriakoo au keriakoo kama alivyoita yeye japo nilijua alimaanisha kariakoo.
Kwa maelezo ya shahzad alidai kabla hajaondoka eneo hilo la kiwanja namba 32 kulikuwepo ofisi za carrier corps na halikua na soko kubwa na la kueleweka kama hivi sasa hivyo anasema alitamani sana kufika hapo ili ashuhudie kwa macho uwepo wa soko hilo.
Kuna muda aliniuliza jambo kwa kiswahili na nilijua hakutaka wengine waelewe alichokua ana maanisha.
" Umewezaje kuelewana na huyu binti kwani kwa haraka tu nimegundua ana kiburi sana, yaani hajataka kabisa kunitajia ubini wake"
MIMI: hapana mzee wangu huyu binti ni miongoni mwa watu wastaarabu niliowahi kukutana nao ila anasababu ya msingi kwanini hajakutajia ubini wake nadhani kadiri tunavyoendelea kuwa pamoja ata kuelezea sababu hizo
Kuna muda mjukuu wa shahzad alikua wakiongea na fatemeh kwa lugha ya uko kwao lakini kwa mujibu wa fatemeh ambae alijitahidi kuni tafsiria papo kwa papo alisema:-
Yule kijana ameshangaa kumuona babu yake anafuraha sana baada ya kukutana na mimi hivyo dogo alimuuliza fatemeh mimi ni Nani.
Kwa mujibu wa fatemeh alimwambia nimetokea East Africa na nimefika hapo Tehran kwa dhumuni la kuonana na shahzad. Lakini alimwambia kuwa ata yeye fatemeh hajui dhumuni agenda yetu mimi na shahzad.
Nyumbani kwa shahzad hapakua mbali kabisa kwani tulitumia takribani robo saa mpaka kufika kwenye nyumba ya mzee huyo. Lilikua ni jumba la kifahari kwa kweli na lilionekana ni jumba la miaka mingi sana yaani ni miongoni mwa majengo ya muda mrefu kwenye mji huo wa Tehran.
Tulikaribishwa ndani na mmama wa kiislamu ambae alionekana kujistiri zaidi ata ya namna ambayo alijistiri kibonde wangu fatemeh. Mzee shahzad nae alitukaribisha kwa mara ya pili mimi na fatemeh,
tukiwa kwenye sebule kubwa fatemeh alinitonya tena katika namna kama ananikumbusha nimpange mzee kuhusu shida yangu kabla mzee hajaanza sound zake.
MIMI: mzee wangu nashukuru sana kwa ukarimu wako na namna ulivyonipokea mimi na mwenzangu kwakweli sikutegemea mapokezi haya pamoja na mambo machache uliyonifunua yanayohusu Tanganyika.
( Kabla sijaendelea aliniwahi)
SHAHZAD: nakushukuru pia mjukuu wangu, ata mimi nimefurahi ujio wanu umejitahidi kunikumbusha mengi sana niliyopitia nikiwa huko Tanganyika.
Alafu samahan mjukuu wangu huyu ni mke wako au mzinzi mwenzio maana siwaelewi tena hususani yeye ndio simuelewi sana. Na kama ni hawala yako leo ndio mwisho kukanyaga kwenye nyumba hii.
MIMI: hapana mzee, fatemeh ndio mwenyeji wangu ambae tumekutana ubalozi wa Iran nchini Tanzania au Tanganyika kama unavyoijua wewe.
Kwa mara ya kwanza nilimueleza shida yangu au dhumuni langu na aliahidi kunisaidia kufika huku na kukutafuta na ndio maana unaona yeye ndio aliomba appointment.
SHAHZAD: apo sasa nimekuelewa enhe dhumuni lako
( Shahzad alikua anaongea kiswahili lakini kuna muda sikumuelewa kabisa hivyo nilijitahidi sana alionekana kusahau maneno mengi. Kilichomsaidia kikubwa ni ule uwepo wa misamiati mingi ya kiswahili kwenye kiarabu)
MIMI: mzee mimi dhumuni la safari hii au mguu wangu huu mpaka unafika hapa, nilitaka ushirikiano wako na ufahamu wako kuhusu mji wa kale ulioitwa rapta.
SHAHZAD: hahha hahahh naona watanganyika mmeanza kufunguka sasa, na umenikumbusha bwana mmoja aliyeitwa Schulz yeye alipenda sana taarifa za mji huu.
Labda nikuulize swali moja mjukuu wangu,
Wewe ulijuaje kama mimi ninaweza kujua taarifa za kina za mji huo?
MIMI: haswaa!!! Hilo swali nililitarajia, kiukweli ni bwana huyohuyo uliyemtaja kama Schulz ambae nilikutana nae Düsseldorf yeye ndiye wa kwanza kunipa taarifa hiyo lakini pia aliniambia nikutafute kwa maelezo ya ziada.
SHAHZAD: hivi yule mwanaharamu mjaa laana bado yupo hai?
MIMI: kwa kweli sidhani kama bado yupo hai kwani Wakati ananipa habari hizi alikua ameshachoka sana.
SHAHZAD: lazima achoke yaani kwa lifestyle ya yule mpuuzi sikutarajia kama atafika ata miaka 50 asee ni bahati yake kama alifanikiwa kuzeeka. Sasa bilashaka mjukuu wangu na wewe utakua wa hovyo sana kama uliweza kukutana na Schulz kwani Schulz hana maana ata kidogo.
Kwanza unajua kama alikua ni jasusi yule mjaa laana, yaani ilikua kidogo tu niuze siri za nchi wakati ule kwani alikua rafiki yangu sana kama hajakwambia.
Mara ya mwisho marehemu mke wangu ndio aliniambia nipunguze kumuamini kwani yeye alikua na mashaka nae sana. Na kama unavyojua, siku zote kama umeoa na mke wako akakutamkia kuwa ana mashaka na rafiki yako basi huyo rafiki ako muangalie kwa jicho la tatu usipuuze.
Anaendelea shahzad,
Schulz alijifanya mjanja mjanja kuna muda alienda mpaka Tanganyika kwa ajili ya kufika rapta lakini alichemka.
MIMI: kwanini alichemka?
SHAHZAD: hahhahh usicheze na uchawi wa mtu mweusi wewe, mjerumani mwenyewe anajikubali lakini pale alichemka na hakuondoka na chochote kwani unafikiri mimi mpaka nikaamua kuweka makazi Tanganyika nilikua sina akili.
MIMI: kwaiyo mzee haukufamnikiwa?
SHAHZAD: umekuja kujua kuhusu rapta au umekuja kujua kama nilifanikiwa? Ebu acha uswahili basi.
Shahzad anaendelea,
Hizi harakati unataka uzifanye na nani kwani sio jambo la kufanya peke labda kama utakua na mtaji mkubwa lakini pia technology kubwa.
Na mwisho kabisa umejipangaje kwani serikali lazima kutakua kuna namna ya vikwazo kwakua kama wewe umejua basi wapo wengi ambao tayari wamejua.
MIMI: kiukweli kabisa kuhusu timu ya kuambatana nayo na mfuko au fund kwa ajili ya project nzima bado sijafanya maamuzi kwakua bado sijaijua vizuri project na ndio maana nikakutafuta ili nipate overview ya project nzima.
SHAHZAD: sawa mjukuu wangu naomba tupate chakula kwanza ayo mengine tutaelezana taratibu.
Binafsi nilitaman sana fatemeh angekuwa anaelewa kiswahili nikiamini angeweza kuchangia mawili matatu lakini ndio hivyo tena kwani mzee aligoma kutumia kingereza.
Hivyo nilijiandaa kwenda kutafsiri kila kitu pindi tukiwa nyumbani mimi na fatemeh ili tu ajue nini kinaendelea.
Wakati tunaendelea na chakula shahzad alisema yeye hapo awali aliwahi kufanya kazi kwenye ile maktaba tuliyomkuta lakini kuhusu documents zilizohusu mji wa rapta kwa mara ya kwanza zilihifadhiwa na familia lakini wakazihamishia kwenye maktaba iliyojulikana kama Rasht National Library.
Alidai Rasht ilikua ni maktaba ya mwanzo hapo uajemi na Ndani yaku hundred thousand of books, hivyo kama familia walipeleka documents hizo kwenye maktaba hiyo baada ya kuona hamna mtu kwenye familia ambaye yupo interested na habari hizo kwani wengi walikua ni wafanya biashara tu.
Ila aliongezea kwa kusema kuwa ata ndani ya nyumba ile pia walikua na maktaba yao hivyo ata angalia na humo pia ili kujua kama kuna masalia yaliyobaki yaliyohusu taarifa za mji huo.
Tulipata chakula safi sana na kitamu lakini wakati wote huo sikua nimekaa na fatemeh kwani wao walikua wakipata chakula tofauti na tulipokua sisi.
Baada ya chakula nilimshukuru sana shahzad na yeye aliniambia naweza kwenda nije kesho yake kwani atakua tayari amekwisha andaa kila kitu na atanifahamisha mengi.
Alidai kuwa kwa siku hiyo nilikua sijamuandaa mapema kuhusu jambo hilo. Alisema nikija kesho yake atanisimulia pia kisa cha bwana mmoja aliyewahi kuishi nchini humo yaani Iran, alisema bwana huyo alikua baharia na aliitwa Sindbad na alisema kisa hicho kinaweza kuniongezea motisha kwenye mchakato wangu huo.
Tuliaga kwa pamoja mimi na fatemeh, lakini kabla hatuja ondoka shahzad alimuita fatemeh na sijui waliongea nini kwani walitumia lugha yao hivyo nilipanga kumuuliza tukifika nyumbani.
Tukiwa nje ya nyumba ile ilikuja tena ile Toyota hiace nyeusi na tulipanda kwa ajili ya kurudi tena nyumbani.
TUKUTANE WHATSAPP 0623329512 kwa muendelezo tupo mbali mbali zaidi.
Mwenye namba ya baba jose muuza mkaa tafadhali [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
Sent from my ZTE T1002 using
JamiiForums mobile app