Utajiri wa Mark Zuckerberg wapotea kwa Dola bilioni 7 baada ya Mitandao yake kupata tatizo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Utajiri wa Mwanzilishi wa Facebook, Mark Zuckerberg umeanguka kwa wastani wa USD 5.9 B hadi 7 kwenye saa ambazo mitandao ya Facebook, Instagram na Facebook ilipata tatizo la kimtandao, kwa sasa Mark yupo No. 6 kwenye orodha ya Matajiri Duniani akiwa na utajiri wa USD 116. 8 B.

Kampuni ya Facebook imethibitisha kwamba Mitandao yake ya Facebook,Instagram na WhatsApp imerudi hewani baada ya kupata tatizo na kufanya baadhi ya Watumiaji kushindwa kufanya chochote kwenye Account zao, kwenye taarifa yao wameomba radhi Wateja wote Duniani.

Kampuni ya Faceebok imesema kilichosababisha tatizo la kimtandao lililopeleka baadhi ya Watumiaji wa Instagram,WhatsApp na Faceebok kushindwa kufanya chochote kwenye Account zao ni kufeli kwa mabadiliko ya mfumo, Wafanyakazi wa Faceebok wanasema tatizo ni la ndani na sio udukuzi.
 
Waangalie ni jinsi gani wanaweza kutulipa kwa muda ambao tumeshindwa kufanya biashara zetu kutokana na tatizo lao binafsi nimepoteza kiasi Tshs. 12,600,500/ kwasababu ya huduma yao.
 
Hata mimi nimepata hasara ya shilingi 1,500 kwa kuweka vocha na kuunga kifurushi Mara kwa mara nilizani kimeisha
Tuna haki ya kudai , wanaotakiwa kutuongoza katika madai haya ni TCRA kupitia kitengo chao cha madai ya huduma kwa mteja ila naona wamekaa kimya kama hawajui vile ...
 
Daaaah, kuna watu wanatengeneza fwezaaa! Hivi naye ATAKUFA kama MWENDAZAKE JIWEE!!!?
Alooo acha utani chief! Kafa Nuhu, kafa Ibrahim, kafa Mussa, kafa Mfalme Suleiman ambaye hata huo utajiri wa Mark ungekua ni kama ka nukta tu kwake hakuna tajiri wa kuja kuufikia wa Suleiman mpaka kiama.

Mwendazake kafa kaacha mambo yote, kaacha miradi binafsi (ya upigaji na halali) ukiwemo ule wa gari za kusafirisha mafuta za bei kama Scania, MAN, Volvo na Mercedes Benz za kampuni ya PETROCOM za kwenda Rwanza kwa ndugu yake Kagame.

Inshort Mark atakufa wakati wake ukufika na ataachiwa wengine huo utajiri wake wote.
 
Dunian kote ukiacha biasahara ya madawa ya kulevya , silaha cha kivita , inayofuata ni biashara mtandaoni....
Yeah biashara ya mtandaoni hasa Forex inaongoza pia kwenye cycle ya uchumi wa dunia mbali na hayo mengine..
 
Mbona hasemi faida anayotengeneza kwa siku?

au anaogopa TRA watamsongeshea bili?
 
Tumepeleka mswaada wa sheria bungeni, Wale mboga mboga wakiupitisha tu soon tunaanza kuwacharge Google na hawa FB.
 
Alooo acha utani chief! Kafa Nuhu, kafa Ibrahim, kafa Mussa, kafa Mfalme Suleiman ambaye hata huo utajiri wa Mark ungekua ni kama ka nukta tu kwake hakuna tajiri wa kuja kuufikia wa Suleiman mpaka kiama.

Mwendazake kafa kaacha mambo yote, kaacha miradi binafsi (ya upigaji na halali) ukiwemo ule wa gari za kusafirisha mafuta za bei kama Scania, MAN, Volvo na Mercedes Benz za kampuni ya PETROCOM za kwenda Rwanza kwa ndugu yake Kagame.

Inshort Mark atakufa wakati wake ukufika na ataachiwa wengine huo utajiri wake wote.
Hivi kama sio hadithi huyu suleiman alikua anamiliki nini
 
Back
Top Bottom