Utajiri wa Mark Zuckerberg wapotea kwa Dola bilioni 7 baada ya Mitandao yake kupata tatizo

Utajiri wa Mark Zuckerberg wapotea kwa Dola bilioni 7 baada ya Mitandao yake kupata tatizo

Pia tujiulize kama kwa saa 6 amepoteza usd 7b ina maana kwa saa 24 anapata faida ya usd 28b 😁 je mitandao yake imeanza lini na kwa hiyo faida mbona ni tofauti na utajiri wake wa sasa.? Mimi nadhani tunapigwa sana kwenye hizi taarifa kuna ile ya Ronaldo kutoa chupa ya Coca-Cola halafu ety asababishe hasara ya usd B+
Anyway hao ndio wenye dunia ngoja tuwaache
Jielimishe namna stock market au masoko ya hisa yanavyofanya kazi. Utajiri mkubwa wa Mark Zuck unashikiliwa na idadi ya hisa zake kwenye kampuni ya FB...

So kadri hisa za FB zinavyoongezeka thamani ndivyo utajiri wake unavyoongezeka. Likitokea jambo lolote likafanya thamani ya hisa hizo kushuka na utajiri wake utashuka automatically.

Kusimama kwa mitandao yake mitatu hapo jana ni suala lililopelekea thamani ya hisa za FB kushuka kwenye masoko ya hisa...yaani investors wa Fb walianza kuuza hisa zao kwa wingi kuliko wanaonunua.
 
Utajiri wa Mwanzilishi wa Facebook, Mark Zuckerberg umeanguka kwa wastani wa USD 5.9 B hadi 7 kwenye saa ambazo mitandao ya Facebook, Instagram na Facebook ilipata tatizo la kimtandao, kwa sasa Mark yupo No. 6 kwenye orodha ya Matajiri Duniani akiwa na utajiri wa USD 116. 8 B.

Kampuni ya Facebook imethibitisha kwamba Mitandao yake ya Facebook,Instagram na WhatsApp imerudi hewani baada ya kupata tatizo na kufanya baadhi ya Watumiaji kushindwa kufanya chochote kwenye Account zao, kwenye taarifa yao wameomba radhi Wateja wote Duniani.

Kampuni ya Faceebok imesema kilichosababisha tatizo la kimtandao lililopeleka baadhi ya Watumiaji wa Instagram,WhatsApp na Faceebok kushindwa kufanya chochote kwenye Account zao ni kufeli kwa mabadiliko ya mfumo, Wafanyakazi wa Faceebok wanasema tatizo ni la ndani na sio udukuzi.
Kwahiyo tufanyeje kumrudishia hela zake?
 
Back
Top Bottom