Utajiri wa nchi ni akili za Watu sio rasilimali kama madini na nyinginezo


Akili hugeuza jangwa kuwa msitu.
Akili hugeuza jiwe kuwa dhahabu,
Akili hugeuza kinyago kuwa mnyama.
Akili hugeuza maji kuwa umeme,
Akili hugeuza pamba kuwa nguo.

Akili humfanya taifa kuvamia mataifa mengine na kuyadhibiti.

Huwezi kuwa na kuitwa Tajiri hata kama unarasilimali kama hauna AKILI.
Malighafi, na viumbe vya asili huitwa Rasilimali zikishapewa value na watu wenye Akili.

Hata Watu huitwa Rasilimali Watu ikiwa watakuwa Productive..

Wanaosema Afrika ni tajiri ni watu wasiofikiri au kutumia Akili vizuri Kwa sababu wanaangalia viumbe hai na viumbe visivyohai Ila Wazungu na mataifa Makubwa Afrika huichukulia masikini tuu Kwa sababu ya watu wake kuwa wajinga
 
Akili hugeuza jangwa kuwa msitu.
Akili hugeuza jiwe kuwa dhahabu...
Kwa ulimwengu wa sasa kuwa na rasilimali ni hatua kubwa kuelekea utajiri wa wananchi kama utatumia akili yako vizuri. Akili lazima ifanyie kazi kitu fulani kugeuza kuwa utajiri wa wananchi. Kwa Tanzania ni natural resources.
 
Kwa ulimwengu wa sasa kuwa na rasilimali ni hatua kubwa kuelekea utajiri wa wananchi kama utatumia akili yako vizuri. Akili lazima ifanyie kazi kitu fulani kugeuza kuwa utajiri wa wananchi. Kwa Tanzania ni natural resources.
Ndugu yangu huo ndiyo mtazamo wa zamani sana kuhusu swali la maendeleo ya binadamu yanaletwa na nini. Tazama historia ya dunia.

Kama huelewi basi jifunze, usibishe. Usipokubali kuwa kuna masuala huelewi huwezi kujifunza. Wala si lazima uelewe kila kitu ndiyo maana binadamu tunazidiana.
 

Mkuu hili tatizo la watu wenye uwezo mdogo kuwa viongozi ni la kihistoria. Wakati Nyerere anachukua nchi wasomi walikuwa ni wachache, hivyo watu wenye elimu kubwa wakawa wanajikita zaidi kwenye kazi za taaluma.

Matokeo yake wasio na elimu wakajikita kwenye siasa. Kidogo kidogo wasio na elimu wakaanza kuwa na maamuzi.

Wasomi walipoamua kuingia kwenye siasa wakakuta wameshachelewa maana wasio na elimu ni mabingwa wa fitina na zengwe.

Hii ndio sababu kwenye siasa zetu hasa ndani ya ccm mizengwe ni njia namba moja ya kupambana.
 
Nakubaliana na wewe 100% maana kuna nchi nimewahi kuishi miaka kadhaa na haina resources ata robo ya zetu ila ukitua tuu airport ndio utaelewa tunaishi dunia mbili tofauti na sio moja....
 
Picha linaanza wakoloni walivyokuja wakagawana maeneo, wazungu/waarabu 10 walimiliki kundi la mababu zetu kama 500 hivi na bado wanateswa balaa sasa kama ni watu timam si mngewaua tuu fasta... tatizo letu kubwa kabisa ni LOW IQ & SELFISHNESS..
 
Kulaumu viongozi ni sawa ila tatizo ni sisi, kwanza viongozi ni reflection ya watu wake maana hatukodi kutoka nje badi ni sisi wenyewe, kama kiongozi umemuweka madarakani lakini akizingua kumtoa huwezi sasa hapo alaumiwe nani kama sio wewe uliemchagua..
 
Yaani leo umegusa mfupa kabisa maana, nilikua nawaza kwa nini Israel ana export matunda mengi kuanzia marekani, south africa, uingereza na kusambaza grapes kwenye viwanda vya wine dunia nzima wakati ana ardhi ndogo lakini kaweza kuhimili kilimo cha umwagiliaji? Basi jibu ni akili
 
Nikawa nawaza kwa nini rafiki yangu mmoja wa German alinishauri ukitaka kuweka akiba kwa afrika usisumbuke na masoko ya hisa maana hayako stable wewe nunua gold kila mwaka weka, baada ya miaka kumi gold inakua imepanda maradufu na utapata faida kubwa kutokana na reserve ya dhahabu
 
Kwa ulimwengu wa sasa kuwa na rasilimali ni hatua kubwa kuelekea utajiri wa wananchi kama utatumia akili yako vizuri. Akili lazima ifanyie kazi kitu fulani kugeuza kuwa utajiri wa wananchi. Kwa Tanzania ni natural resources.

Ukishakuwa na akili inatosha.
Ili kitu kiwe Rasilimali lazima kipewe Value
 
💯
Ndio maana wachumi wanasema rasilimali muhimu ya kwanza ni rasilimali watu
Maana hata nchi mkiwa 61mil kama vichwan hamna kitu mtajikuta mnaongozwa na nchi yenye watu mil 10 tu
 

Ukikosa Akili umekosa kitu nyeti na muhimu sana
 
[mention]ROBERT HERIEL [/mention] taikoni leo umeongea issue kubwa sana kwa mfano hapo kwa TMA , wao walifold utabiri wao wakawapelekea wizara zote, hivo kila wizara wanatakiwa wajua wanajipanga vipi, kwa mfano nilitegemea wizara ya kilimo ihamasishe wakulima wasisahau kulima mazao yanayohimili ukame mazao kama viazi vitamu, muhogo, mtama( mweupe na mwekundu) , mahindi yanayochukua siku 90 kuiva, lakini pia wakati wa mavuno wahimize akiba maana wananchi ndio kama hao kama unavosema mtu mwenye akili timamu huwezi kula milo mitatu wakati hauna kazi ngumu za kutumia nguvu, basi tu
 
Kwahiyo Watanzania Wengi Hatuna Akili.?

Je hao Wachache Wenye akili wako wapi?
 
Kwahiyo Watanzania Wengi Hatuna Akili.?

Je hao Wachache Wenye akili wako wapi?

Sasa unaacha ku utilize rasimali ulizonazo unakwenda kutafuta mkopo wa bilioni kadhaa huku umekalia matrillion ya rasilimali, yaani unajua wenzako wanaokunzunguka wanahitaji chakula sana, unaacha kuwekeza kikwelikweli kwenye umwagiliaji wakati una vyanzo vya maji vya kutosha na wewe unasubiri mvua kama wao, hapo unakua na akili au mwendawazimu
 
Kwahiyo Watanzania Wengi Hatuna Akili.?

Je hao Wachache Wenye akili wako wapi?

Wewe umeambiwa kutakua na ukame na nishati kama umeme unategemea maji na kila mwaka unalia kuna ukame yaani haujaona vyanzo anuwai kama upepo, makaa ya mawe, gesi ukatumia kuzalisha umeme wa kukutosha na mwingine ukauza? Yaani kila mwaka unalia tatizo lilelile bado hata kama ni kiongozi useme una akili wakati kutatua changamoto umeshindwa miaka yote
 
Ukishakuwa na akili inatosha.
Ili kitu kiwe Rasilimali lazima kipewe Value
Tuna natural resources ambazo zina demand na kwa hiyo zina value na tunaweza kuziongezea value. Nisemacho ni kuwa kama tuna akili tutazifanyia kazi ili tujinufaishe.
Asiye kuwa na natural resources atatafuta mbinu nyingine.
 
Umemaliza kila kitu
 
Ni muhimu kuangalia una nini wakati unatafuta maendeleo na kwa nchi kama tanzania natural resources ni muhimu. Hivyo hizo akili zinatakiwa zije na njia ya kuleta maendeleo kwa kutumia hizi resources.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…