Utajiri wa nchi ni akili za Watu sio rasilimali kama madini na nyinginezo

Utajiri wa nchi ni akili za Watu sio rasilimali kama madini na nyinginezo

Bara la Afrika Ina watu takribani billion 1.35 Taifa la Uswis lina watu million 8.97 Taifa la Uswis kiuchumi linabeba bara Zima la Afrika kwasababu Africa imebeba mabilioni ya watu wajinga.

Kiukweli maendeleo ni rasilimali watu wenye ubongo pevu na si vitu
Hongera mleta mada
 
UTAJIRI WA NCHI NI AKILI ZA WATU, SIO RASILIMALI KAMA MADINI N.K.

Anaandika, Robert Heriel.

Huwaga namshangaa mtu anayesema nchi yetu ni Tajiri. Kwa kweli sio tuu anachekesha Bali pia anaonyesha jinsi alivyokuwa mjinga na asiyeweza kufikiri sawia.

Kama nikiulizwa hivi leo sababu gani inatufanya Waafrika ikiwemo nchi yetu kuwa Masikini, basi jibu litakuwa ni kuwa Sisi tunaakili ndogo Kama sio kuwa hatuna Kabisa.

Taifa ili kiwe Tajiri linahitaji watu wenye akili zaidi kuliko Rasilimali. Utajiri ni Akili na sio wingi wa Rasilimali.
Kuna msemo usemao, penye miti hapana wajenzi.

Akili ndio inaweza kufanya madini kuwa Rasilimali Kwa kuipa Value. Madini kama madini hayajui kama yenyewe ni yathamani, Ila wenye akili ndio wanajua thamani ya madini hayo kutokana na matumizi waliyoyabuni kwayo.

Kidunia Bara la Afrika ndilo bara lenye malighafi nyingi kuliko bara lolote lile. Lakini watu wake wameshindwa kuzigeuza malighafi hizo kuwa Rasilimali Kwa kuzipa thamani.

Ukisikia mtu anakuambia Yeye ni Tajiri Kwa sababu nchi yake inamadini, maziwa na Mito, Ardhi yenye Rutuba, wanyama wa kuvutia, na mambo mengine lakini watu wake ni Hali zao za maisha ni duni jua mtu huyo hajui kufikiri vizuri, na pengine akawa mwendawazimu.

Nchi haiwezi kuwa Tajiri Kama ndani yake inawatu wajinga wengi. Watu wasio na akili wakiwa wengi ndivyo nchi inavyozidi kuwa Masikini.

Mtu asiye na akili Hana tofauti na mnyama wa porini, ni Sawa na tumbili au ngedere anayeishi msituni ananyeshewa mvua na kuchomwa na Jua lakini anashindwa kujenga nyumba hata ya mbao Kwa sababu ya upeo mdogo wa Akili.

Wazungu walivyotuita Waafrika manyani kuna watu walifikiri walimaanisha maumbile yetu yanafanana na nyani😀😀 Kama nawe ulifikiri hivyo basi nawe upo kundi la watu wajinga.

Wazungu walituita manyani mbali na ubaguzi wao lakini walituona akili zetu hazijaachana Sana na tumbili na nduguye ngedere.

Nyani au ngedere ukimpelekea Dhahabu au Almasi wala hataiona inatofauti na jiwe jingine. Kutokana na upeo mdogo wa Akili.

Sisi Watanzania wengi wetu tunaakili ndogo mno na hiyo ndio sababu Sisi sio matajiri. Na tutaendelea kuwa Vivi hivi Kwa Karne kadhaa zijazo.

Watanzania wengi ni Kama wanyama Kwa mambo mengi, kama unavyomuona ng'ombe basi ndivyo wengi wetu tulivyo.

Sio ajabu ukakuta watu kwenye makazi Yao kuna mavi au maji machafu waliyoyasababisha yamewazunguka, yananuka na nzi wamejaa lakini wao hawaoni Shida. Wanalala, wanakula hapohapo, na wanakunya na kukojoa hapohapo.

Hapo ati wanasubiri kiongozi aje awaambie wawe wasafi tena wengine ifikie hatua ya kupelekwa serikali za mitaa kisa anaambiwa asizibue chemba za mavi yake na familia yake, come on!

Sio ajabu jitu linakunya chooni labda cha umma alafu hali-flash uchafu wake. Hivi mtu huyo anatofauti ipi na Mnyama?

Mtu anajua kabisa ili aishi anatakiwa awe na chakula cha kutosha kinachomtosha yeye na familia yake, badala awe na ghala la kuhifadhi chakula kinachomtosha yeye na watoto wake angalau Kwa miaka miwili kulingana na Hali ya hewa.

Yeye anakula Kama mnyama asijue kesho atakula nini. Halafu ikifika kesho anaanza kumlalamikia mtu mwingine labda ni serikali au viongozi. Jamani hivi tunaakili kweli?

Tena wakati mwingine tunazidiwa akili hata na Wanyama.

Hakuna mnyama ambaye atazaa watoto ambao hawezi Kuwatunza. Hakuna na hajawahi kutokea. Mfano Kuku anaouwezo wa kutaga mayai hata Mia moja.

Lakini atataga mayai kumi (10-12) kulingana na uwezo wake wakuyaatamia, sio atage mayai 20 alafu wakati wa kuatamia mengine ashindwe kuyaatamia yajitokeze nje.

Kisha Kwa mayai 10-12 anaouwezo wa kuwachunga na kuwakuza watoto hao.

Halikadhalika na mbwa, ng"'ombe, mbuzi, Simba n.k.

Lakini Sisi unakuta mtu anazaa watoto nje ya uwezo wake wa Kuwatunza, labda watoto 10 alafu ananilaumu serikali kuwa gharama za Shule au hospitali ziondolewe.

Au anaomba msaada Kabisa wa kusaidiwa kulelewa watoto.

Hivi tumelogwa au ni kitu gani?

Mtu unajua kabisa miti ndio huleta hewa Safi, huleta mvua na kivuli kizuri, na Kupunguza joto la nchi. Alafu unakuta watu wamekata miti mtaa mzima ili wajenge nyumba.

Unashangaa mtaa mzima miti ipo 20 Kwa eneo la kilometa moja. Alafu muda huohuo unasikia mwehu akipiga kelele jamani joto Kali, jamani jua linawaka! Mara kiyama kinakaribia.

Kiama ya mavi. Ujinga na wehu wako ndio unaita Kiyama?

Utajiri WA nchi ni akili za watu na sio Rasilimali Kama madini.

Chakufanya;
I. Tujifunze kuwa na Akili ili tuwe nchi yetu itajirike.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Ww baki na elimu yako ya fasihi na pia uongelee zaidi mambo ya fasihi.Mambo ya utajiri na implication zake waachie wanaojua.Unajaza page nyingi hapa JF lakin unaongea vitu visivyo kweli.Labda niongee kwa Mfano.:Arusha Kuna madini ya Tanzanite.Tajiri mmoja aliitwa askofu Mwaka 1995 alichimba na kupata uzito mkubwa sana wa Tanzanite.Akawa Tajiri,akapanda juu ya gorofa akaanza kurusha pesa hovyo.Ww unasema nchi sio Tajiri.Gesi ya Mtwara ni utajiri wa kutosha ila Kuna wabinafsi wameikatalia.
 
Ongezea hapo wanakata miti halafu wanaitisha Dua kuombea mvua[emoji23][emoji23][emoji23]kama sio kurogwa ,Mungu anatuona jinsi tulivyoenda kinyume na nature.

Hahaaa wanakata miti kwanza kosa waweke juhudi ya kutunza mazingira kwa sheria kabisa kwamba kila mji lazima uwe na miti ya matunda hata miwili, taasisi zote shule zote nanserikali nanprivate lazima ziwe na miti, hospitali zote lazima ziwe na miti ya kutosha, makanisa na misikiti lazima wapande miti, masoko yote lazima yapande miti isiyopungua 25 au 30 , lakini anasubiriwa mwamposa aombee mvua
 
We are rich in natural resources but poor in terms of quality human resources and financial muscles.
Kwani wewe unaelewa nini kuhusu utajiri?
Achana na Eurocentric view fikiri kwa Afrocentric view utapata picha pana.
Hao unaowasifia Wana akili hawana huo utajiri na ndiyo maana walikuja huku kuuchukua kimabavu.Ni sawa na wewe umepigika na life town,alafu unapata fununu kuwa kule Nyamongo Mkanda wa madini umetema,utabaki mjini na akili yako au utaenda kusaka utajiri???
 
Sasa kama wanaume 10 weupe walikuwa wakivamia kijiji cha watu 2000 halafu wanaume wote kijijini wanakimbia na kuwaacha wake zao wabakwe hamuoni kuna kitu hakipo sawa hapo?
image_downloader_1666966539825.jpg
FB_IMG_16677036393559092.jpg
image_downloader_1666965787954.jpg
 
Vitu vyengine ni mifumo tu mibovu na kukosa uzalendo na si kwamba hatuna akili, mikataba isiyo na manufaa kwa taifa ni vitu ambavyo sio kwamba wenye kufanya hivyo hawana akili au hawajui wananachokifanya.
 
Chakufanya;
I. Tujifunze kuwa na Akili ili tuwe nchi yetu itajirike.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Mada imekushinda toka mwanzo hadi mwisho! Sasa kama umeficha madini hapo katikati ambapo sikupasoma kwa kukosa uvumilivu na niliyosoma mwanzo mwa mada na mwisho wake, lawama ni yako kwa mtindo wako mbovu wa uandishi.

Niliposoma kichwa cha habari tu, nikavutiwa sana na kutaka kujuwa yaliyomo ndani ya mada yenyewe.

Mstari wa kwanza tu, nikaona mada imepinda. Sikukata tamaa nikajikaza nivute subira. Nikasoma hadi nusu ya andiko; nikaishia hapo. Sikuwa na nguvu tena za kuendelea hadi mwisho wa andiko refu lisilokuwa na mvuto kulisoma.
Lakini nikawa na wasiwasi kwamba pengine nikiruka hadi kule mwisho nitakuta mambo yanayohusiana na kichwa cha mada yenyewe, hata kama itakuwa ni katika mhitasari tu!

Looo, sikuona kitu. Nikaamua kunyanyua hayo niliyobamiza hapo juu kwa kuwa 'disappointed' na mada nzima, isipokuwa kichwa chake cha habari tu basi!

Pole yako ya kuwa na muda wa kupoteza, na pole yetu wasomaji wako kwa kupotezewa muda.
 
Sasa kama wanaume 10 weupe walikuwa wakivamia kijiji cha watu 2000 halafu wanaume wote kijijini wanakimbia na kuwaacha wake zao wabakwe hamuoni kuna kitu hakipo sawa hapo?View attachment 2418903View attachment 2418904View attachment 2418915
Wewe, 'mkulu senkonda' si mtunzi wala mwanzilishi wa haya uliyoyaweka hapa, umeyanyanyua tu toka mahala, lakini hukutaka kuonyesha ulikoyatoa.
Unafanya kazi chafu bila ya kujuwa ni nani unayemfanyia kazi hiyo, tena bila malipo yoyote. Hii inadhihirisha wazi kabisa wewe kuwa mfano wa hao weusi wanaosemwa kwenye mada yenyewe.

Sasa kama hata huwezi kutambua kwamba Xi Jinping hawezi kusema hayo yanayosemekana kayasema, wewe akili yako itakuwa imelala kabisa.
 
Pole sana Robert Heriel. Tulianza kutoka huko kielimu, kifikra na kiutendaji. Pia tukawa na wasomi maarufu duniani hata kwenye kiwango cha Chuo Kikuu waliokuwa wanatuelekeza namna ya kutoka huko ambako leo umeamua kusimilia. Tunarudi nyuma sababu uongozi umefutika! Shule mpaka kwenye ngazi ya Chuo Kikuu nchini ndiyo haipo ya kutosha. Cha kuanza nacho ni uongozi, mawazo, elimu na utendaji utakaotutoa Watanzania wengi kwenye hiyo tabia uliyoeleza. Suala siyo kwamba hakuna akili hapa Tanzania. Ila ni suala lile la mwana falsafa Socrates, je wenye akili wanaruhusiwa kuongoza, wako radhi kuongoza au wasio na akili ambao ni wengi wanaona wana akili kwa hiyo hawahitaji wenye akili? Tatizo ni huo mfumo unaolea tabia hiyo. Hapo ndipo tatizo lilipo. Pole sana naona umeandika kwa hasira. Lakini siyo peke yako na wala hii hoja yako haihusu Chama cho chote. Inahusu future ya Taifa letu. Tanzania iliongoza Afrika kwa fikra, sasa hata majirani tu wanatupiku!!! Lakini ukitusikia bado tunajisifuu!!!
Umemsaidia sana mleta mada kunyoosha mada yake, lakini sijui kama anaelewa ulichomweleza hapa.
 
Acha nijaribu, hata kama sitapata jibu.

Naomba mwenyekujua, mambo manne yaliyosemwa na Mwalimu Nyerere kwamba yanahitajika ili nchi yetu ipate maendeleo.

Tafadhali yaweke hapa chini tuyapime kama yanahusiana kwa vyovyote katika kujibu maudhui ya mada hii inayojadiliwa hapa.
 
Nimesoma heading yako na content nimeona umekosea mahala, kutokana na ulichoandika kwenye content, ulitakiwa kusema kwenye heading yako inahitajika akili ya kusimamia rasilimali tulizonazo, na sio kusema tunatakiwa kuwa na akili bila rasilimali.

Mfano wa madini uliotoa, hapo umeshaonesha umuhimu wa rasilimali, kwa hiyo kinachotakiwa kuwepo ni akili za kuzisimamia, na sio rasilimali zisiwepo kabisa iwepo akili pekee kama ulivyoandika.
 
Acha nijaribu, hata kama sitapata jibu.

Naomba mwenyekujua, mambo manne yaliyosemwa na Mwalimu Nyerere kwamba yanahitajika ili nchi yetu ipate maendeleo.

Tafadhali yaweke hapa chini tuyapime kama yanahusiana kwa vyovyote katika kujibu maudhui ya mada hii inayojadiliwa hapa.
Watu, ardhi, siasa safi, na uongozi bora.
 
Vitu vyengine ni mifumo tu mibovu na kukosa uzalendo na si kwamba hatuna akili, mikataba isiyo na manufaa kwa taifa ni vitu ambavyo sio kwamba wenye kufanya hivyo hawana akili au hawajui wananachokifanya.

Kutokujua unachokifanya ndio kukosa akili Kwenyewe huko
 
Acha nijaribu, hata kama sitapata jibu.

Naomba mwenyekujua, mambo manne yaliyosemwa na Mwalimu Nyerere kwamba yanahitajika ili nchi yetu ipate maendeleo.

Tafadhali yaweke hapa chini tuyapime kama yanahusiana kwa vyovyote katika kujibu maudhui ya mada hii inayojadiliwa hapa.

Nchi ili ipate maendeleo Jambo kubwa kuliko yote ni Akili.
Kama Watu hawana akili hata wangeishi peponi lazima pangedorora.
 
Nimesoma heading yako na content nimeona umekosea mahala, kutokana na ulichoandika kwenye content, ulitakiwa kusema kwenye heading yako inahitajika akili ya kusimamia rasilimali tulizonazo, na sio kusema tunatakiwa kuwa na akili bila rasilimali.

Mfano wa madini uliotoa, hapo umeshaonesha umuhimu wa rasilimali, kwa hiyo kinachotakiwa kuwepo ni akili za kuzisimamia, na sio rasilimali zisiwepo kabisa iwepo akili pekee kama ulivyoandika.

Bila Akili hivyo vitu haiviwezi kuwa Rasilimali.
Ili kitu kiwe Rasilimali lazima Akili iwepo.

Jambo lolote lile linaweza kuwa Rasilimali ukiwa akili ipo.

Mfano, kabla ya Wazungu kuja mambo mengi hayakuwa Rasilimali, kama nawe ya dhahabu hayakuwa madini mpaka wenye akili walipokuja.

Gesi ya mtwara tupo nayo miaka nenda Rudi lakini hatukujua kama ipo na hata tungejua tusingejua matumizi yake Kwa sababu hatuna Akili.


Akili ndio hukipa kitu thamani, kitu chenyee Kama kitu hakina thamani mpaka akili ikipe thamani
 
Back
Top Bottom