Utajiri wa nchi ni akili za Watu sio rasilimali kama madini na nyinginezo

Unapokuwa na rasilimali ambazo huzifanyii maamuzi unakosa uhalali wa kuzimiliki kikamilifu.

Kwa kiasi kikubwa, rasilimali nyingi zilizopo Tanzania sio za watanzania tena.

Nchi inaendelea kuchuuzwa!

Na sio ajabu Watanzania wenyewe miili na akili yetu wengi wetu sio Mali yetu tena. Wengi tunamadeni nguvu tunazotumia ni kwaajili ya kulipia madeni tuliyonayo
 
Na sio ajabu Watanzania wenyewe miili na akili yetu wengi wetu sio Mali yetu tena. Wengi tunamadeni nguvu tunazotumia ni kwaajili ya kulipia madeni tuliyonayo

Mbona ndio ukweli toka uhuru wanakopa hadi leo! Na hatujaweza kujitegemea yaani tunachozalisha ndio tunalipa mikopo sasa toka uhuru hapo ujue tulishauzwa kama ulivosema yaani kuna watu huko wanatutazama kama watumwa wao basi
 
Tunapokosea ni kwenye mfumo wetu wa ajira hasa hizi za kufanya maamuzi kama makatibu wakuu wakurugenzi wa mashirika, wizara na halmashauri.

Siyo kwamba TZ haina watu wenye akili, lakini ifahamike kuwa watu wenye akili si watu wa kujikomba, si machawa. Hivyo nafasi hizi nyeti kiwa za uteuzi inafanya kujwaza na watu wengi wasio na akili.

I wish siku moja hizi nafasi ziwe zinatangazwa na watu wenye sifa na akili waombe.

kwa muda mfupi utaona tofauti.

Mara nyingi napenda kutoa mifano ya ya Clouds. Clouds imefika hapo ilipo kwa sababu ya kuajiri watu kwa merits na siyo kwa kujuana. Waanzilishi wa Clouds wali hunt na mpaka leo wana mifumo ya kupata the best people kwenye nafasi mbalimbali. Ndo maana inazidi kushamiri na kukua kila siku. Ubunifu mpya kila siku. Ila wangewekana kwa kujuana na vimemo isingefika hapo.

Hebu tufike mahali nafasi zote za kiutendaji zishindaniwe. Hata kama ni Rais atateua lakini Rais apelekewe majina ya top three yaliyopatokana kwa njia ya mchakato wa wazi.

Bila kufanya hivyo trust me miaka 59 ijayo tutakuwa hivi hivi.
 
Ni muhimu kuangalia una nini wakati unatafuta maendeleo na kwa nchi kama tanzania natural resources ni muhimu. Hivyo hizo akili zinatakiwa zije na njia ya kuleta maendeleo kwa kutumia hizi resources.
Ukisoma huu uzi wote mara nyingi utaelewa mradi using'ang'anie mawazo yako peke yake. Wenzio wanataja Israel, Hong Kong hata watawala wetu wa zamani, Waingereza; hizo resources zilizowafikisha hapo ziko wapi?
 
Ni muhimu kuangalia una nini wakati unatafuta maendeleo na kwa nchi kama tanzania natural resources ni muhimu. Hivyo hizo akili zinatakiwa zije na njia ya kuleta maendeleo kwa kutumia hizi resources.

Dhahabu unayoiona Afrika sii mali yako, Tanzanite ya simanjiro sii mali yako kwa mfano wenye akili wakuachie dhahabu yako utafanyia nini? Jibu hauna cha kufanyia maana hauna akili, unabeach nzuri kuanzia Tanga, Pwani, Dar, lindi, mtwara, kigoma, mwanza, mara, na kyela na ruvuma ( ziwa nyasa) lakini sababu hauna akili ya kuadd value na kufanya utalii wa fukwe kuimarika na upate mapato makubwa beach unabaki kuanikia dagaa, kwenda kunya na kutupa taka taka na kufua nguo wakati ukijua kila mwaka kuna maeneo duniani kuna joto hapakaliki unashindwa ku utilise watu wakaja kuishi huko kwa miezi ya joto kwa gharama nafuu na ukakusanya zaidi mapesa
 
Hii maada tamu sana , mtu mwenye akili hawezi kushindwa kuleta majawabu ya matatizo yake mwenyewe, tukiambiwa tunapenda ngono na pombe tunakataa, nenda mitandaoni nadhani utakuta watu weusi ndio wanapiga picha na hennessy au iphone ili kuoneshea wenzao kua wamefanikiwa
 
Uko sahihi kabisa.
Huhitaji rasilimali kuendelea, ukiwa na akili utazitafuta popote utazipata na utakuwa tajiri.
Nchi za wenzetu wameelewa hili zamani sana wakaweka elimu yao kuwa ya mtindo wa kutatua matatizo.
Kupitia elimu sahihi ndio tutapata watu wanaofikiri kisawa sawa na kuweza kubadili hizi rasilimali kuwa utajiri. Tatizo mifumo yetu ya elimu hairuhusu mtu kuwa mbunifu sababu hata wanaofundisha no majangaa.
Kwa hiyo tunasoma na kukariri elimu isiyo na manufaa yaani elimu usiyoweza kuitumia kutatua changamoto ni ya nini?
Lazima tujitathmini na tukubali kuanza upya sio makosa kujisahihisha pale unaposea kuliko kukomaa tu kupiga propaganda miaka nend rudi tupo pale pale.
South Korea hawana rasilimali zozote za kuizidi Tanzania lakini Wana watu wenye akili kutuzidi ndio maana wapo pale walipo leo hii.
Hatuhitaji rasilimali tuendee tunahitaji watu wenye akili ambao pia hawatokei kwa baati mbaya ila ni mipango kabambe.
 
WATANZANIA TUNA UPUNGUFU MKUBWA WA AKILI MKUU
 
Nakuunga mkono 100%,hata maofisini wafanyakazi wasio na uwezo wa kuleta ufanisi ndiyo hupewa vyeo!!
Kujipendekeza na unafiki vinaliangamiza taifa hili.

Tanzania Ni masikini kwa sababu tumewaachia waso na akili wafanye maamuzi na ndiyo hushika nyadhifa za kufanya maamuzi.
 
Thanks for the nice thread
You kill it 100%
Much appreciation Taikon wa Fasihi
 
Kwangu Mimi hii ni thread ya kufunga mwaka 2022.ni madini tupu ahsante taikon.Unaweza kukuta mtu ni daktari au MWALIMU Lakini anakula ndizi kwenye daladala anarusha maganda dirishani.Hapa taikon unahisi TATIZO ni nini??

Ndio kukosa akili huko sasa halafu mwenye akili mazingira anayokaa hua ni masafi sana, ushaona anapoishi mwenye akili panakosa garden au maua au miche kadhaa ya matunda ili kufanya hali ya hewa iwe safi? Asie na akili anakugongea pavement pote halafu anaona ufahari kumbe keshaathiri hali ya hewa kwake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…