Nakumbuka mwaka 2007 ,Kuna Mama jirani mtaa wa 6:na nilipokua nakaa ,alikua anatumia Utajiri wa Ndagu ,Maisha yake yalikua si Haba ,alitetemesha mtaa wetu na vitongoji vyake pale Tunduma
Kama kawaida Utajiri wake ulikua ni wa Kufa siku 7 anafufuka siku ya 8 na Hali mpya,Nguvu mpya na Kasi Mpya
Hapo mtashaangaa tu kanunua nyumba mpya,kaongeza maduka manzese(wale waliofika Tunduma wanapafahamu)
Kilichokuja kumuua kimoja(moja kwa moja) ni watoto wake (Huyo Mama alikua Mjane),aliwaaga kuwa anaenda Dar kuchukua mzigo ,basi akajifungia Mochwari yake ya hapo kwake(chumba chake maalumu cha kufia siku 7 hapo kwake)
Basi siku ya 4 toka Afe watoto katika kucheza sana mle ndani na wenzao,kuna mmoja aliwashawishi waingie hicho chumba
,wakatafuta Funguo Kibahati wakaipata,kufungua wakakuta Mama Mjane kafa kaoza mpaka mafunza funza yametapakaa ndani ya chumba hicho [emoji317]
Watoto kupiga kelele kwa majirani ,watu wakajaa pale nyumbani kwake ,ilikua ni Taharuki mtaani,ilikuja kujulikana baadae alikua anatumia Ndagu kwenye itajiri wake
Tulizika na Tushamsahau toka 2007