Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani - 20.
Nilikuwa nina maswali kichwani mwangu zaidi ya elfu moja na ambayo hayakuwa na majibu.Iliwezekana vipi mwanamke ambaye hakuwahi kabisa kufika kwangu hata mara moja leo aje tena kwa hoja ya kwamba ameelekezwa kwa kuulizia ulizia?Je,alimuuliza nani huyo ambaye ananifahamu pale mwisho wa lami?Pili,inakuwaje Farah afanane kiasi kile na Zahra/Maya?,sawa yawezekana wangefanana kama ndugu wa tumbo moja,lakini je hadi mchoro mkononi?,kiukweli kwangu ilikuwa ni kama sinema ambayo sikuielewa hata kidogo.Kwakuwa Ally Mpemba amewahi kuniambia Farah ni dada yake,nilidhani uenda Farah na Maya wakawa ni mapacha kwasababu pia Ally aliniambia Maya/Zahra alikuwa ni dada yake pia.
Baada ya kuingia kwenye gari niliiwasha na kuanza kuiondoa taratibu kuelekea Magomeni.Sikutaka kabisa kukaa kimya,niliona niendelee kumdodosa Aunt Farah ili niweze kuufahamu ukweli!.
Mimi "Kwahiyo dada umekuja unaulizia?"
Farah "Mbona unakuwa na mashaka sana leo?,kwanini?"
Mimi "Hapana dada sina mashaka ila nauliza tu!"
Farah "Wewe hukuwahi kumwambia Ally unakaa Gongo la mboto mwisho wa lami?"
Mimi "nimewahi kumwambia lakini kaka Ally pia hajawahi kufika kwangu".
Farah "Nilipofika hapo mwisho wa lami nimeulizia nikaelekezwa"
Mimi "ooh sawa"
Kiukweli sikutaka kumbishia maana niliona uenda tungekwazana kwasababu sababu alizokuwa akinipa zilikuwa haziniingi akilini hata kidogo,nilijua kabisa alikuwa akinidanganya,pale mwisho wa lami mahali nilipokuwa nikikaa mimi kulikuwaga hakuna watu ninaofahamiana nao sana uenda jamaa mwenye duka pale nje,pia kwa mazingira yale isingekuwa rahisi mtu kumifahamu kwasababu nilikuwaga si mtu wa kujichanganya na ndiyo maana nikasema uenda ningekuwa maarufu pale mtaani hapo angenishawishi kwa ule uongo wake laki kiukweli sikukubaliana naye hata kidogo.Niliamua kukausha tu ili mambo mengine yaendelee maana niliona nikiendelea kulifuatilia hilo suala sana kiundani uenda ningeibua mambo mengine.
Mimi "Dada nikuulize swali?"
Farah "Karibu"
Mimi "Kwenu mmezaliwa wawili tu na Kaka Ally?"
Farah "Kwanini?"
Mimi "Nimeuliza tu maana mara zote nawaona nyie tu"
Farah "mmh! hapana tupo wengi"
Aliendelea "Wengine hawakai hapa Bongo"
Mimi "Kwahiyo kwa hapa Bongo upo wewe na kaka Ally tu!"
Farah "Hapana wapo wengine!"
Mimi "ooh sawa!"
Niliamua kukaa kimya sikutaka kabisa kuendelea kuuliza maswali mengi kwakuwa hata yeye pia niliona ananijibu kishingo upande hivyo nikaona nisiingie ndani sana ijapokuwa maswali nilikuwa nayo mengi sana.Sasa kichwani mwangu nilipanga ya kwamba,usiku wa siku hiyo nikamtazame vizuri Maya atakapokuwa akila chakula chake pale sebuleni ili kujiridhisha maana kiukweli walikuwa wakifanana kila kitu na Farah.
Baada ya kufika Magomeni kwenye nyumba ya Ally Mpemba,nilifungua geti na ile gari kuiingiza hadi ndani kwenye sehemu ya kuegeshea.Nilishuka kwenye gari nikaenda kumchukulia ndani funguo ya gari dada Farah ambaye wakati huo alikuwa nje akinisubiri.Baada ya kumpatia ule ufunguo akawa amechukua mkoba wake akatoa shilingi milioni 2 akanipatia.
Farah "Hela hizi hapa"
Mimi "Nashukuru dada"
Hakuchukua muda akaingia kwenye ile Range.Nilisogea nikamfungulia geti akawa ametoka na kuondoka.Sikutaka kabisa kupoteza muda hapo nyumbani niliondoka zangu hadi sokoni kwenda kununua mahitaji ya chakula cha Maya,niliwasha gari nikawa nimetoka zangu kuelekea soko la Ilala,kiukweli wakati huo nilikuwa nimenawiri sana na nilikuwa nanyuka pamba za ukweli,ulevi wangu mkubwa ulikuwa ni kupendeza kwa kuvaa vizuri.
Sasa kuna mahali nilifika nikapaki ile gari kisha nikashuka kuelekea sokoni kununua mahitaji,wakati nikiwa nanunua mahitaji kwa mama mmoja,ghafla nikasikia sauti ya mwanamke mmoja ambaye ilinifanya nikageuka kumtazama,hadi leo sijajua ni kitu gani kilitokea ila huwa najiuliza maswali mengi sana.
Huu ulimwengu hauko kama mnavyodhani ndugu zangu,kuna muda unaweza kuwaona watu wanapendeza na kuishi maisha bora ukadhani ni rahisi lakini si hivyo!,mimi baada ya kupitia mambo hayo machache ndiyo maana leo napambana kwa nguvu zangu kufa na kupona ili kujipatia riziki,sasa kuna watu nikiwaambia mimi ni naendesha bodaboda huwa hawaamini wanadhani natania,japokuwa pia najaribu kuwekeza kwenye kilimo lakini bodaboda hiyo hiyo ndiyo inanipatia pesa ya uwekezaji huo!.Niliamua kupambana na maisha yangu ya udundulizaji kwasababu hakuna maisha ambayo sijapitia,kila baya na jema nishaona,hivyo niliamua kutulia kujipambania,huko mbele mtaelewa vizuri ni kwanini leo naendesha bodaboda.
Sauti ya kike "Mama Eliya nikuletee?"
Mama Eliya "Leo sina hela mwaya!"
Huyo mama Eliya alikuwa ni mama ambaye nilikuwa nimesimama mbele yake nikuchukua kabeji,sasa wakati akiwa kwenye pilika pilika za kunirudishia chenji ndiyo nikawa nimesikia hiyo sauti ikimwambia hivyo,baada ya kumtazama yule mwanamke aliyemuita mama Eliya kiukweli nilibaki nikimtizama.Kiukweli baada ya yule mwanamke kumuita huyo mama niliyekuwa nikinunua mboga kwake nilijikuta tu nageuka kumtazama ni nani na nilipogeuka nilijikuta namtamani baada ya kumtazama,hakuwa mwanamke mbaya,alikuwa ni mwanamke mmoja wa kawaida ila alikuwa na umbo zuri sana.
Mimi "Anauza nini huyo?"
Mama Eliya "Anauza Juisi"
Mimi "Ni nzuri?"
Mama Eliya "Juisi yake huwa tamu kweli sema leo tu ndiyo hali ngumu ila ningechukua"
Mimi "Anauza bei gani?"
Mama Eliya "Anapima kwenye glasi shingi elfu moja"
Mimi "Mwambie akupe"
Mama Eliya "Ahsante mwanangu"
Aliendelea "Nitakunywa baadae "
Mimi "Mwambie aje akupe kabisa maana nyie huwa wajanja,nitakupa hela utaisunda huta nunua,nataka na yeye umuungishe kama mimi nilivyokuungisha"
Baada ya kumwambia hivyo yule mama muuzaji alianza kucheka sana.Nia yangu ilikuwa ni kwamba amuite yule mwanamke asogee kwa karibu nipate kumtazama vizuri maana alikuwa bize na juisi yake na kwangu isingekuwa rahisi kumsimamisha pale sokoni na kuanza kuzungumza nae kwasababu mara zote nimekuwa na aibu kusimama na mwanamke machoni pa watu.
Mama Eliya "Wala usijali baba namuungisha"
Aliendelea "Wewe Ray......Raaaaaay niletee juisi nimepewa ofa"
Baada ya kuita yule mwanamke alijongea taratibu hadi pale nilipokuwa nimesimama kwa mama Eliya.
Mama Eliya "Niwekee glasi moja nimepewa ofa na mwanangu"
Mimi "Mama wewe kunywa hadi utosheke sijakupa ofa yenye kikomo"
Mama Eliya "Mmh nashukuru baba"
Nilifahamu kabisa mama Eliya anaweza kuwa anauhitaji na pesa ndiyo maana ile ofa ni kama alitamani asinywe ili ile hela achukue,sasa mimi nilipanga kumpatia kiasi kidogo kitakachomsaidia.
Mimi "Jusi yako unatengeneza na nini?"
Muuza juisi "Ni mchanganyiko wa Embe,pasheni na parachichi"
Mimi "Ok"
Muuza juisi "Nichangie basi kaka"
Mimi "Haina shida wala usijali,nimepaki gari pale ng'ambo naomba twende ili ikiwezekana nitafute chombo uniwekee"
Muuza juisi "Ninazo chupa kaka"
Mimi "Mbona hapa sizioni?"
Muuza juisi "Kuna mahali nimeziweka nakimbilia mara moja"
Mimi "Ni safi?"
Muuza juisi "Ni safi kaka huwa naziosha na maji moto"
Aliendelea "Au kama hutoridhika basi unywee hapa kaka"
Mimi "Usijali nitanunua"
Basi baada ya mazungumzo mafupi nilimpatia yule mama noti ya shilingi elfu kumi kama malipo ya juisi na itakayobaki achukue yeye,kiukweli alinishukuru sana na nilimwambia wakati wote nitakapokuwa naenda hapo sokoni kununua bidhaa ningekuwa namtafuta yeye.
Niliondoka nikaongozana na yule dada muuza juisi kuelekea nilikokuwa nimepaki gari,mimi nilikuwa mbele na yeye alikuwa nyuma yangu huku mkononi akiwa ameshika galoni ya juisi na kapu la vikombe.Tulipofika nilifungua gari kisha nikamwambia animinie kwenye glasi ili ninywe kwanza niisikie radha yake.
Mimi "Ni tamu"
Mimi "Unaitwa nani?"
Muuza juisi "Naitwa Rehema"
Mimi "Unaishi wapi Rehema?"
Yeye "Naishi Ubungo msewe?"
Mimi "Ubungo msewe iko maeneo gani?"
Yeye "Pale pale Ubungo ni jirani na chuo kikuu"
Mimi "ooh,duuu mbona kama mbali?"
Yeye "Wala hata siyo mbali"
Mimi "Unaona siyo mbali kwasababu ushazoea"
Mimi "Kwahiyo kila siku unamaliza hiyo galoni?"
Yeye "Inategemea,kuna muda nauza hizi galoni hata tatu na kuna siku hata moja haiishi"
Mimi "Ok"
Mimi "Umeolewa?"
Yeye "Sijaolewa ila nina mtu wangu"
Mimi "Mnaishi wote?"
Yeye "Hapana,mi naishi kwa shangazi na yeye anaishi kwao!"
Mimi "Kwahiyo ndiyo umepanga aje awe mume wako?"
Yeye "Hayo sasa ni maajaliwa ya Mwenyezi Mungu"
Mimi "Kwenu anafahamika?"
Yeye "Anafahamika kwasababu ninaye mtoto wake!"
Mimi "Unaye mtoto wake kivipi?"
Yeye "Nimezaa naye "
Mimi "Mbona sasa mimi nakupenda Rehema"
Yeye "Kunipenda wala siyo dhambi kaka,dhambi ni kumtamani mke wa mtu"
Mimi "Mimi sijakutamani Ray mimi nakupenda"
Yeye "Toka lini mwanaume wa Dar akapenda mwanamke?,wewe sema umenitamani tu ili unipate umalize haja zako unikimbie,nyie wanaume hata sinaga hamu kabisa na nyie!"
Mimi "Hebu tuachane na mambo mengi Ray nipe namba yako ya simu nitakupigia"
Yeye "Simu yangu inasumbua betri nimeiacha nyumbani"
Mimi "Mimi nitakupataje ili tutafute mazingira mazuri tuzungumze"
Yeye "Mimi napatikana tu hapa hapa wewe ukija utamuuliza mama Eliya"
Mimi "Lakini umeelewa nilichokwambia Ray?"
Yeye "Lakini nishakwambia ninaye mtu wangu!"
Mimi "Kwani utamwambia?"
Yeye "Siyo hivyo,kumbuka penzi ni kama kikohozi huwa alijifichi!"
Aliendelea "Halafu unataka kuniambia wewe huna mtu?"
Mimi "Ningekuwa na mtu unadhani ningekusumbua?"
Yeye "Mimi nitajuaje!,nyie wanaume kwani mnaaminikaga?"
Mimi "Kwahiyo hata huyo jamaa yako pia humuamini?"
Yeye "Simuamini ndiyo,kwani anapokaa huko ninakuwa nae?"
Mimi "Siko kama unavyodhani Ray"
Yeye "Sawa,ushamaliza kuniongopea?,mi nataka niwahi kwenye biashara"
Mimi "Sikuongopei ila amini hivyo"
Yeye "Sawa ukiwa na shida basi utanitafuta napatikana hapa hapa sokoni"
Baada ya mazungumzo yale na yule mwanamke ambaye alionekana na msimamo,nilimpatia noti ya shilingi elfu kumi akawa anataka kunirudishia chenji nikamwambia hiyo nimempatia tu.
Yeye "Ahsante"
Yeye "Ila nimesahau kukuuliza jina lako!"
Mimi "Mimi naitwa Umughaka"
Yeye "Sawa nashukuru kukufahamu Umungaka"
Mimi "Siyo Umungaka,ni Umughaka!"
Yeye "ahahahaa nisamehe jamani unajina gumu,sijui kama nitaweza kulitamka"
Mimi "Kesho nitakuja kukucheki"
Yeye "Saa ngapi sasa ili niwe maeneo jirani?"
Mimi "Mida kama hii"
Yeye "Sawa,msalimie wifi "
Mimi "Wifi tena!"
Yeye "Utakubali sasa!?"
Aliendelea "Haya basi tutaonana!"
Yule mwanamke aliondoka huku namtazama namna alivyokuwa na nyama za kutosha,kiukweli alikuwa mwanamke fulani wa kawaida ila umbo lake halikuwa la kawaida,mara zote ugonjwa wangu kwa wanawake umekuwa ni uleule wa matako makubwa wastani na hips za kuzugia,mara zote huwa sihangaiki na sura kwasababu si sehemu ya hitaji langu kubwa kwa mwanamke,huwa naangalia vinavyo nihusu na visivyo nihusu naachana navyo.
Nilielewa ni kila mwanamke ukijaribu kumtongoza ni lazima akwambie anaye mtu wake ili kujipa thamani lakini mara zote huwa haiko hivyo,hata Rehema nilifahamu kabisa ili ajipe thamani ni lazima angeniambia anaye mtu ingawa nilipomtazama macho yake ilionekana kabisa anasema uongo.
Niliwasha mchuma nikaondoka zangu kuelekea Magomeni kupeleka zile bidhaa na baada ya kufika kama kawaida niliziweka pale mezani kisha nikafunga mlango nikaondoka zangu,sasa kwakuwa ilikuwa bado mapema,nilirudi hadi pale nilipokuwepo mwanzo kwa ajili ya kuendelea na makamuzi ya bia.Muda uliposogea niliamua kuondoka kuelekea magomeni ili kuweza kuufungua mlango wa Maya,nilipofika nilipaki lile gari kisha nikaingia ndani nikafungua mlango wa kwenye kile chumba cha Maya kisha nikauacha wazi nikatoka zangu nje.
Kwakuwa nilikuwa nimeshiba,niliingia kwenye ile gari nikafunga mlango nikawa nasubiri mida mida ifike ili niweze kumtazama Maya kwa uzuri ili kujiridhisha.Mpaka wakati huo sikuiona simu ya Ally Mpemba wala nini!,niliendelea kusubiri nikidhani angenipigia kama alivyokuwa ameniahidi lakini haikuwa hivyo.
Ilipofika mida ya saa 3 usiku nilianza kusikia yule kiumbe Maya akitafuna kile chakula chake kwa sauti kama mara zote ambavyo huwa akifanya.Nilifungua mlango wa gari taratibu kisha nikasogea hadi dirishani ambako kungeniwezesha kumtizama vizuri kwakuwa nilikuwa nimewasha taa na kufungua lile pazia.Nilisogea hadi pale dirishani kisha nikaanza kumtizama kwa makini sana,sasa wakati namtizama yeye alikuwa amenipa mgongo,nilijaribu kumuangalia kwa umakini mkubwa sana na kiukweli walifanana kila kitu na Faraha,kuanzia urefu hadi umbo,ile alama ya mkononi nilijaribu kuitazama lakini sikuweza kuiona kwakuwa muda wote mikono alikuwa ameshika chakula chake akiendelea kula,hivyo kufanya nisiweze kuitazama vizuri,sasa wakati nikiwa namtazama aligeuka ghafla kama mtu ambaye alihisi kitu akawa anaangaalia pale dirishani huku akiacha kutafuna kwa mshangao,nilisogea pembeni ili asinione,baada ya muda nilipochungulia pale sebuleni sikuweza kumuona tena akawa amendoka.Nilirudi zangu kwenye gari nikiwa najiuliza sana maswali mengi,kumbuka pamoja na mambo yote ikiwemo kulala na Maya lakini ni kiumbe ambaye sikupaswa kumzoea na hakuzoeleka.
Ilipofika mida ya saa 5 usiku nilisikia honi ikipigwa getini na ilikuwa ni honi ya lile gari alilokuwa amechukua Farah,niliondoka nikaenda kumfungulia geti kisha akawa ameingiza gari ndani.Aliposhuka kwenye ile gari akawa ameniambia anahitaji kuingia ndani kwenda kujisaidia.
Mimi "Habari za huko dada"
Farah "Nzuri,ndiyo narejea!"
Aliendelea "Nilidhani uenda nisingekukuta ila nimewasiliana na kaka Ally ameniambia upo"
Aliendelea "Ngoja nijisaidie kidogo nimebanwa"
Nilitaka kumzuia asiingie ndani lakini nilishindwa kumzuia kwasababu nilifahamu kabisa ni ndugu yake na Ally Mpemba pia walitoka kuongea muda si mrefu.Hapo awali Ally Mpemba aliwahi kuniambia sipaswi kabisa kumruhusu mtu yeyote kuingia ndani ya ile nyumba yake hata akiwa ndugu yake,kitu alichoniambia Ally Mpemba ambacho naweza kufanya ni kuruhusu ndugu zake tu kukalia kiti cha mbele kwenye gari aliyokuwa amenipatia kupigia misele lakini mtu mwingine hakuruhusiwa.
Sasa kabla hata sijamwambia chochote,nilishitukia kufungua mlango na kuingia ndani,kitu cha ajabu wakati Maya amemaliza kula nilikuwa bado sijasafisha pale sebuleni na mara zote huwa nasafisha asubuhi,sasa nilitaka kumwambia Farah atumie choo cha nje ili asingiingie ndani ambako kungeleta taharuki,niliingia ndani pale sebuleni lakini sikumuona Farah nikiamini uenda alikuwa ameingia chooni,nilianza kusafisha ile meza na pale chini kwa haraka,kabla hata sijamaliza nilimuona anafungua mlango wa chumba cha Ally na kutoka,kilichonishangaza zaidi ni kwamba ule mlango nilikuwa nimeufunga na funguo na funguo mara zote zilikuwa zinakaa kwenye kimeza cha luninga,nikajaribu kuzitazama funguo nikakuta zipo pale kwenye kimeza,sasa nikawa najiuliza ule mlango sikuufunga?,na kama nisingeufunga zile funguo zisingechomoka pale mlangoni!,na kwanini ameingia kwenye chumba cha Ally akashindwa kwenda chooni ambako vyoo vilikuwa vinajitegemea?.
Kiukweli hofu ilianza kuniingia na kwakuwa nilikuwa mtu mzima nilitambua fika yawezekana Farah hakuwa mtu wa kawaida.
Farah "Mimi nakwenda!"
Mimi "Sawa dada nikusindikize?"
Farah "Hapana"
Mimi "Sawa dada usiku mwema tutaonana kesho"
Farah "Panapo majaaliwa"
Baada ya kuondoka Farah kiukweli sikuelewa ile hali.
Itaendelea....................