Sehemu ya 25 | Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini ShetaniNimeishia sehemu ya 24...
lakini natafuta sehemu zinazofuata sizioni ila nakutana na MICOMMENT kibao hadi inaboa
Kwelii hili mimi nina ndugu yangu lakini hataki kunipa hata ela ya mtaji wala hakuna ndugu hata mzazi wetu mmoja anaejua kwake kuanzia ameondoka nyumbani yapata miaka mi5 hajwah kurudi ila tunaskia tuu jamaa anamafanikio ila hatupajui Hata kwenye Miradi yakeMpkaa sasa iv nmegundua ukiona una ndugu yako yupo sehem nzuri lkn hawaiti ndugu zake kwenye hyo miradi yake usilalame sana,jua tuu kuna issue behind.
Kwa jinsi alivyoelekeza kwamba ni nyuma ya big bon huo mgahawa upo maeneo ya mkunguni na mtaa wa nyamwezi na pale kuna mgahawa unachoma nyama kwa wingi nadhani ndio huo.Leo Nimepita KARIAKOO MTAA WA MKUNGUNI… Nimethaminisha Migahawa yote ya mtaa ule na kukumbuka Details kwamba Ally Mpemba ana Range Rover, na ana pesa za kutosha hivyo hawezi kuwa na Mgahawa Uchwara… napata hisia Mgahawa wa Ally Mpemba ni ule uliopo ndani ya lile Jengo La AL-Uruba[emoji848]
Mbaya zaidi akauza pagale lake ili ampeleke Rehema chuo, na tunavyojua mchumba hasomeshwiYeah risk aliyochukua wkt anatafuta maisha ni kubwa mnooo lkn sasa utelezi na kutokufuata mashariti kumemgalimu. Maana shariti usipakie abiria seat ya mbele simple. Yeye kaenda piga mitungi kasahau hilo shariti. Kazi kubwa sana alishafanya mpaka kutembea na msukule. Matanuzi ya Audi, mitungi na mademu imemponza masta.
Namanyele ni Nkasi, sio SumbawangaNimehuzunika master kupoteza utajiri wake kizembe kisa mapenzi.. Story nzuri sana..
Nimeona uchawi wa sumbawanga ni mkubwa kuliko wa chumbe
Kajifunze lugha fasaha kwanza ndio urudi na kashfa zako za kipuuzi hapa. "Kuzalia sio kudhalia"....Wewe ni muongo mkubwa sana na hujui kutunza kumbukumbu kwa kile ulichoongopa.
Kwenye ile stori yako nyingine ulituambia umemaliza form 6 mwaka 2019 ndipo ukaingia kwenye ujambazi ambao uliufanya miaka kadhaa kabla hujaachana nao na kuja dar kuanza maisha mapya
Na hapa kwenye hayo maisha mapya kuna miaka kadhaa imepita kabla hujakutana na huyo Rehema jumlisha miaka uliyomesha ,halafu unakuja kutuambia amekudhalia binti anayetimiza miaka mitano.
Chai yako imedoda.
Safi sana kamanda...[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Kama ulienda shule basi una wazazi wapumbavu kuliko wote duniani,huwezi kuzaa kondoo halafu ukaipeleka shule,hii Ada ambayo wazazi wako walitumia kukupeleka Shule ni bora wangenunua hata Kuku wakaanza ufugaji!.
Hebu Quote au Screen short mahali ambapo nimewahi kusema nimemaliza form six mwaka 2019.
Naomba watu wote nendeni kwenye uzi wangu waUzi huu unapatikana kwenye jukwaa la HOJA MCHANGANYIKO halafu msicreen short kipande au sehemu ambayo nilisema nimemaliza form 6 mwaka 2019.Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani
Nisikuchoshe na usinichoshe, tusichoshane! Kwenye haya maisha kuna wakati huwa ninakaa chini na kusema "Kama sikufa kipindi kile,basi siwezi kufa mpaka Mungu atakaporuhusu" Nadhani wengi mtakumbuka ni siku chache tu zimepita nimeandika kisa cha maisha ambayo nilikutana nayo wakati nikiwa...www.jamiiforums.com
Wewe ni mwanaume kweli?,mbona kama nina mashaka na jinsia yako[emoji848]
Safi sana mkuuSehemu ya 25 | Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani
=
Sehemu ya 26 | Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani
=
Sehemu ya 27 | Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani
Naweza kupata msaada wa kukisoma pia?Nilinunua soft ya kitabu chake watsap aisee kuna Mambo mengi Sana ya dunia hii kwenye ushirikina
Usinisahau mkuuAkikutumia nitumie na mimi kaka
Ulipatwa na nini?Zile Mbina zilitakaga kuchukua maisha yangu nakumbuka nilienda na Babu kwenye Mbina na Marehemu Babu kuuza Miwa, Machungwa, Machenza na Mastafeli kwenye trailer la kusukumwa na Ng'ombe nikajichanganya nikaenda mpaka kwenye kichanja anachosimama Mringi aisee kilichonipata, Ni kwa sababu tu Ukoo wa Babu ulikuwa wa Kichifu
Wapi nakupa Nina part oneUlipatwa na nini?
Naomba link mkuuWapi nakupa Nina part one
Vp kuhusu hao wanafanyakazi ambao uliwatafutia ajira kwenye mgahawa na wanatakiwa kufa kama kafara....hukufanya mpango wa kuwashtua hata kupitia kupitia indirect ili kuwaokoa kwa huruma ya kibinadamu na huo msala wa kuwa kafara??Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani - 27.
Nilifanikiwa kufika Sumbawanga na ilikuwa ni Safari iliyochukua takribani siku siku mbili kwasababu nakumbuka tulipofika Mbeya tulilala pale halafu kesho yake tukaianza tena safari, nilipofika Sumbawanga sikutaka kupoteza muda nilitafuta gari zilizokuwa zinaelekea Namanyere nikawa nimekata tiketi,muda ulipowadia tuliondoka.
Nilifanikiwa kufika kwa yule mtaalamu niliyekuwa nimeelekezwa kwake,alinipokea na nikawa nimeambiwa nisubiri kwanza amalize kuwatibu watu kadhaa niliowakuta pale;Zamu yangu ilipofika aliiniita nikawa nimeingia ndani ambako alikuwa akifanyia shughuli zake za uaguzi.Sasa alinipatia kigoda nikawa nimekalia na akaniambia nitulie nisizungumue jambo lolote,alianza kuhesabu tudude fulani kama tumawe kisha akawa ananiambia.
Mganga "Hadi sasa uko hai inabidi ushukuru Mizimu kukulinda"
Aliendelea "Naangalia namna ulivyotupiwa jini linaloendelea kukutesa na inapaswa ufe,kuna sehemu ulienda ukatengenezwa ndiyo imesaidia"
Aliendelea "Mtu uliyemuamini ndiye kafanya yote haya"
Mganga "Huyu mtu ni nani kwako?"
Mimi "Ni rafiki yangu tu"
Mganga " Kwanini unaishi na rafiki ambaye anakufanyia mambo mabaya namna hii?"
Aliendelea " Huyu mtu ni hatari sana kwako"
Aliendelea "Huyu mtu anafuga jini ambalo ndilo limekuhangaisha na kwakuwa ulikuwa kwenye himaya yake alikuwa anakufanya anavyotaka!"
Aliendelea "Ndiyo maana nasema Uishukuru Mizimu yako kwasababu alikuwa amekutegeshea Jini hilo likuangamize kabisa"
Baada ya kuniambia maneno hayo ndipo sasa akaniambia nizingumze ninachokitaka.
Mimi "Nimekuja unisaidie maana hali yangu si nzuri "
Mganga "Nitakusaidia ondoa shaka ila inabidi kuna vitu ununue niweze kukutengeneza vizuri"
Basi akawa ameniambia nikanunue vitu kadhaa ambavyo vitahusika katika matibabu yangu,mimi nilitoa fedha na vitu hivyo vikaenda kununuliwa na mtu ambaye alimtuma yeye.Baada ya kununuliwa vitu hivyo nilianza matibabu na matibabu yenyewe nakumbuka kuna mengine yalifanyika makaburini akiwa ameniambia ni kuzika mikosi yote na uchawi wote ule wa Ki-Unguja(Chumbe).
Nilikaa kwa yule mtaalamu takribani wiki 2 na baada ya kuwa amekamilisha zoezi la matibabu,kuna dawa kadhaa alinipatia ambazo aliniambia nitazitumia nikapafika Dar es salaam.Niliondoka nikawa nimerudi Dar es salaam na sikutakiwa kabisa kumsogelea Ally Mpemba hata kidogo,nakumbuka maisha yalianza kuwa magumu sana tena kwa upande wangu,kwakuwa nilishazoea kupambana sikutaka kabisa kukaa,fedha ambayo nilikuwa nayo kwa kipindi hicho ndiyo ilinisaidia kwa kipindi chote ambacho sikuwa na kazi,pia ndiyo fedha niliyotumia kumlipia Ada na matumizi mpenzi wangu Rehema wakati wote akiwa chuo cha ualimu.
Kuna kipindi hali ilipokuwa mbaya kiuchumi nilikuwa naenda pale Gongo la mboto kwa washikaji kujipendekeza kwenye magari na hatimaye kuna gari ambalo nililipata nikawa konda mimi na mshikaji wangu mmoja,lile gari lilikuwa likifanya ruti za Gongo la mboto kwenda Mbagala,niliamua kuto mtazama mtu usoni ili niweze kupambana,sasa nakumbuka Steve alikuwa akinishangaa mimi kuwa konda wa daladala ilihali niliacha kazi ambayo angalau ilikuwa kidogo na heshima ya usajili wa line,jamaa yeye aliona ni heri kuwa msajili line kuliko kuwa konda kazi ambayo ilikuwa ikidharaulika na kila mtu!,mimi sikuona taabu yeyote kwasababu nilishaifanya na ambacho nikagundua ni kwamba wakati huo makonda walikuwa wakipiga sana hela,yaani kulaza kwa siku elfu 20 lilikuwa jambo la kawaida kabisa,hiyo elfu 20 ni hela ambayo unabaki nayo baada ya mambo mengine kama msosi n.k
Mimi sikutaka kumuangalia mtu ananipangia nifanye nini,niliangalia kitu ambacho kinanipatia hela nzuri na ambacho nakifanya kwa moyo mmoja,aibu haikuwaga na haipo hadi leo kwenye maisha yangu ya utafutaji!.Kwenye lile gari nakumbula makonda tulikuwa wawili kwasababu lilikuwa gari lililokuwa na milango miwili,hivyo tukawa tunafanya kazi kwa kushirikiana!.
Namshukuru Mungu hata Rehema wangu ni mwanamke ambaye alikuwa hajali wala hachukii kile nilichokuwa nakifanya,tena nakumbuka ni mwanamke ambaye alinitia sana moyo katika kupambana.Alipomaliza chuo akawa ameajiliwa mkoani Morogoro wilaya ya Ifakara ambako ndiko anafanyia kazi hadi leo,baada ya kuwa ameajiliwa na kupangiwa kituo cha kazi akawa ameondoka.
Mimi niliendelea kupambana sana kwenye kazi ya ukonda na nikawa najinyima kiasi kwamba nikapunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima.Baada ya kutengeneza kama milioni 2 kwa miezi kadhaa ya kujinyima,nikawa nimenunua tena uwanja maeneo ya kibamba,nililipa hela nusu nikawa napambana kutafuta pesa nyingine ili angalau nilipe yote kile kiwanja nikimiliki,nilipambana sana na hatimaye nikawa nimemaliza kulipia kile kiwanja,sasa kumbe kiwanja chenyewe kilikuwa na mgogoro wa kifamilia.Kiukweli nilihangaika sana na kile kiwanja,ilifika sehemu mtu aliyeniuzia tulifikishana hadi mahakamani,jamaa aliahidi kuwa atakuwa ananipatia hela kidogo kidogo hadi hela niliyompatia itakapokwisha,sasa ulipaji wake ulikuwa wa kusua sua na ikabidi niachane nacho,alinilipaga pesa kama nusu ya kile nilichompatia ikabidi niachane nae.
Rehema aliniambia nitulie niachane nacho na kama ni uwanja tungenunua mwingine,huu mji kiukweli umenitesa sana ndugu zangu.
Namshukuru Mungu baada ya kupata tena fedha kiasi ambazo nilizikusanya kwenye kazi yangu ya ukonda kwa kudunduliza,Rehema akawa ameniongezea fedha nyingine nikawa nimenunua pikipiki yangu na nikaanza rasmi kazi ya bodaboda ambayo ndiyo inaniweka mjini hadi leo.
Rehema alinizalia mtoto wa kike mzuri kama yeye na mwaka huu ifikapo mwezi wa kumi anatimiza umri wa miaka 5.Rehema hadi sasa ni mwanamke wangu ingawa mi naishi Dar es salaam na yeye akiwa kituo cha kazi hapo Ifakara,huwa naenda na yeye pia huwa anakuja Dar es salaam.
Ally Mpemba hadi sasa ninavyoandika hapa yupo na naona jamaa amekuwa mtu mkubwa sana,lile duka la pale gerezani walilifunga na ile fremu sikuhizi naona ina mtu mwenye biashara nyingine,duka lile la Aggrey bado lipo na huwa jamaa anakuwepo pale mara moja moja,ule mgahawa hadi sasa upo na unayo sifa ileile ya kuua wafanyakazi wake.
Jamaa kwasasa sijajua atakuwa anabiashara gani nyingine lakini hizo nilizoziacha bado zinafanya kazi.
Mwaka jana nikiwa kwenye mitikasi yangu Kkoo nilipita pale Aggrey nikawa nimemuona ila yeye hakuniona.Jamaa bado anaendeleza libeneke na kupiga pesa.
Mimi niliamua nichague haya maisha yangu yasiyokuwa na msongo hata kidogo kwasababu naridhika na hichi kidogo nikipatacho.
Kuna uwanja mwaka jana nimenunua kwa kushirikiana na Rehema wangu upo maeneo ya Maili moja,na Mungu akisaidia mwaka huu tunaweza kuanza ujenzi mdogo mdogo.
Kituo changu cha kazi huwa ni Bunju ingawaje pia huwa niko bize wakati fulani,mimi napaki Bunju ila sikai Bunju ndugu zangu.
Maisha si lelemama kama mnavyodhani,kama una nafasi ya kufanya chochote ambacho ni halali wewe fanya ili ukimbilie ndoto zako,usiogope kufanya kwa kuhofia watu watasema nini,wewe kaza moyo fanya,hao wanakucheka leo yawezekana kesho wakaanza kusema weww ni freemason,hivyo wape kisogo na fanya chochote ilimradi kinakuingizia pesa.
Usimuangalie mtu wewe ziangalie fedha,huyo mtu anakucheka kwasababu huna fedha,ukizipata hata kuwa na muda wa kukucheka tena.
MWISHO.
Kupitia stori yako nimejifunza na kulink matukio/stori tunazosikia mtaani......utasikia tajiri wa mabasi alikuwa anawatoa kafara madereva wake lakn sasa hv kabadili anatoa kafara ya wanyamaUtajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani - 27.