Wiki iliyopita nikiwa kwenye pilikapilika zangu za Bodaboda kuchukua mzigo wa mteja wangu pale Kkoo,nikakutana na dada mmoja ambaye tulifahamiana wakati nikiwa nafanya kazi za Ally Mpemba,sasa baada ya kuonana kama mjuavyo kwakuwa ilikuwa ni muda mrefu tukabadilishana namba za simu.
Sasa jana mida ya saa 5 usiku kuna mtu akanipigia simu ikiwa ni namba ngeni ambayo haikuwa kwenye moja ya watu niliowasevu,baada ya kuipokea ndipo kumbe alikuwa Brother Ally Mpemba.
Daaah!,nilipigwa na butwaa kwasababu sikuwa na namba yake na yeye hakuwa na namba yangu,nilipomuuliza kaipata wapi namba yangu kaniambia kapewa na yule dada na hiyo ni baada ya wao kupiga stori.
So,jamaa kaniambia leo 23.3.2023 tuonane kuna mambo ya msingi tuzungumze.
Nitaonana nae na nitawajuza