Mkuu
UMUGHAKA kama kweli hivi visa unavyovisimulia in vya kweli basi naweza kuitimisha kwa kusema hujui kabisa kuzitumia akili ulizopewa na mwenyezi Mungu
Tukianzia kule kwa Monica ulikopakwa pakwa na kuchanjwa chanjwa na wachawi,tuje kule kwa akina Jipe ulikoamua kuwa jambazi eti kwa sababu rafiki yako Mutatiro alikubali.Tuje hapa kwenye hiki kisa chako cha kumuamini shetani ambako ulikabidhiwa kazi ya kufungua na kufunga chumba usichojua kimehifadhi kitu gani nawe ukakubali tu kama likondoo tena ukaambiwa uwe unalala kwenye gari nje bado hukuinusa hatari
Tuje hapa unaposema ulipelekwa kwa mganga huko Unguja bila kujua unakwenda fanya nini na wewe ukaenda kimya kimya bila hata kumuaga msela wako Steve
Kwa kutumia tu hayo matukio yako machache uliyoyaweka hadharani mpaka sasa naweza kusema ulikuwa na haki zote kupata zero advance na baba yako alikuwa na haki zote kukutimua nyumbani kwake uende ukaibiwe million 9 zako za ujambazi na mlevi Kiheri