Enzi hizo bado niko mdogo kuna tukio la ajabu sana liliitokea familia ya jirani yetu
Huyu jirani yetu alikuwa akifuga ng'ombe mmoja nyumbani kwake mwenye ukilema wa mguu mmoja na alikuwa akipendana nae sana kiasi cha kuzua ya kuzuriwa na majirani,sasa siku moja bwana mida ya kama saa 12 hivi asubuhi kikasikika kwake kilio cha mtu mzima aliyekuwa akilia kwa uchungu sana;
Sasa kwa kujiongeza tu tukajua lazima atakuwa kafiwa na ndugu,hivyo majirani wakakusanyika fasta kwake kumtia moyo(kumpa pole kwa kipagani),tulipofika pale kwake akawa ndio kazidisha kilio kwa lugha ya kitaa tunaweza kusema kuwa aliongeza volume mpaka mwisho
Basi bwana watu wakakaa kaa hapo,wazee wenzake akiwamo na baba yangu ambae ndio babu yenu kwa sasa wakawa wanamwambia atulize moyo sasa awaeleze ni kipi kimemkumba,akalia lia kama robo saa nzima kisha eti akatutaka radhi majirani zake kwa kutuamsha na vilio vyake na cha kushangaza akasema yeye hajapatwa na msiba wowote ila asubuhi alipokwenda chumbani kwa ng'ombe wake kumjulia hali kama afanyavyo siku zote kamkuta ng'ombe wake kipenzi hatuko nae tena Duniani.
Huwezi amini hazikupita hata siku tatu yule dingi akawa amedanja(kufa),tukamzika akaoza na kuwa udongo mpaka leo tunasubiria na sisi tufe tukamuulize ilikuaje wakapishana na ng'ombe(ngombhe kwa kihaya) wake siku 3 tu kufa au kulikiwa na siri fulani kubwa kati yake na ng'ombe wake