Utajiri wa ushirikina una masharti magumu sana

Utajiri wa ushirikina una masharti magumu sana

Bwa Uyoga alikua mfanyabiashara wa kawaida lakini huku Kwamtogole tulimuona wa mboga saba, alikua na usafiri wa IST na mke wake hakupanda basi kwenda sokoni. Watoto walisoma English Medium.

Katika kupambana na maisha alikutana na fundi aliyemuahidi utajiri wake utaongezeka akifuata masharti yake. Sharti la kwanza ni kuwa mwanaune wa kwanza kulala na binti yake mkubwa na la pili ni kutokulala na mke wake usiku. Uyoga alianza kufanya mapenzi na binti yake, utajiri ulianza kumiminika na mke alinunuliwa Mercedes Benz Sport Car. Sifahamu kama mama alifahamu au la.

Kule ofisini oder ziliongezeka mpaka ilibidi atatute sehemu kubwa ya kuweka ofisi na kuanza kuajiri vijana wasomi wa kusaidia kuendesha biashara. Katika wasomi wakiajiriwa kulikua na kijana mhasibu, alijipenda sana, alikua nadhifu muda wote.

Mhasibu alikaa sana bench tangu amalize chuo kwahiyo ile kazi kwake ilikua life line, alifanya kazi mpaka saa mbili usiku siku nyingine mradi alikwenda nyumbani aliacha hesabu zime balance. Uyoga. alimpenda sana mhasibu, hata mikutano yake mingine ya kibiashara alimuomba amuakilishe kama mikutano inaingiliana.

Kule nyumbani binti wa Uyoga alikamata ujauzito. Uyoga hajui afanye nini, akiwa Mzee wa heshima katika jamii. Alimuita Mhasibu na kumuweka kikao ofisini kwake. Alimuambia unaoa mwezi ujao, unamuoa binti yangu na harusi yote nitaigharamia mimi. Mhasibu alipewa ghorofa la kuanzia maisha gari na mtaji wa biashara kwa masharti pia awe mhasibu wa Uyoga kwa siku hata mbili kwa wiki.

Harusi ilikua kubwa sana, ndugu wa mhasibu walisafiri kutoka kijijini kwa usafiri wa ndege na walifikia hotelini.. Baada ya harusi mhasibu anagundua yaliyomo yamo mkewe ni mjamzito tena mimba karibu miezi mitatu. Ndipo alipofahamu kuwa hakuna free lunch mjini. Alilea mimba mpaka inakua na mtoto anazaliwa.

Mtoto alizaliwa na matatizo ya kiafya kutokana na muingiliano wa genes. Uyoga aliwasaidia wanandoa wapya kutafuta matibabu nje ya nchi ikiwemo Afrika ya Kusini na India. Watoto waliofuata walikua ni wa mhasibu.
Mbona story yenyewe umeikata ghafla au mwenyewe kaja....😜😂

Malizia bac mpendwa...🤔🤔
 
I chai yako mbona tam sana[emoji39][emoji39] umeweka sukar au Asali?
Arabika.
FXjjeL9acAESdF-.jpg
 
Ila kuna sehemu kama tumepigwa na dude zima kichwani "wazazi wa muhasibu walisafiri kwa ndege kutoka kijijini" kwa Nchi hii iliyorogwa ni kijiji gani kina uwanja [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Sasa ulitaka niandike walioga na kuvaa kandambili wakasubiri bodaboda mpaka airport!
 
Ni utajiri wa mateso kwa maana ya masharti kibao
 
Shetani hana shukrani wala fadhila hata umpe ukoo wako wote ukishawamaliza ni lazima akumalize na utajiri wake anajua kisha anampa boya mwingine kwa mtiririko huo huo
 
Sasa story zako mbona zinaisha kama filamu za kinaigeria
 
Huyo mganga wa Sky Eclat Cha mtoto.
Yuko mganga Tanzania hii unakwenda kwake huna hata Mia, ukikubali masharti yake unapewa mtaji wa 30 mpaka 40 m uanzie biashara. Huyu hakuambii utembee na bi mkubwa Wala binti Ila masharti yake yamewashinda wengi.
Kwanza hataki utembee na mwanamke zaidi ya mke wako, sharti jingine Ni kurudisha ule mkopo on time ile wengine wakopeshwe. Ila masharti mengine........wengi wanarudi.
 
Back
Top Bottom