Utakapokuwa Askari Usisahau mambo haya

Utakapokuwa Askari Usisahau mambo haya

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
UTAKAPOKUWA ASKARI; USISAHAU MAMBO HAYA.

Anaandika Robert Heriel.

Na endapo utaamua kuwa Askari, iwe wa Kulinda Amani, au wa kulinda Mali, au kulinda na kusimamia sheria au amri Fulani, iwe kulinda utawala au viongozi.

Tena ukiwa Askari wa upelelezi, au kuongoza misafara ya Magari au vyombo vyote vya usafiri Kwa Aina zake.
Tena ukiwa Askari wa kuharibu, kuua na kuangamiza watu, au kuharibu Mali, au kuharibu Jambo lolote lile.

Tena ukiwa Askari magereza, kulinda na kuwasimamia wafungwa. Tena ukiwa Askari wa kulinda mipaka ya nchi, na kulinda nchi yako au kulinda kundi Fulani huenda ni wakimbizi au watu wenye uhitaji maalumu wa dharura.

Tena siku ukiwa Askari wa kukusanya iwe Ushuru, au makusanyo yoyote Yale iwe ya mamlaka na utawala au yamtu awaye yoyote Yule au kundi lolote lile. Basi usije ukasahau mambo haya.

Tena ukiwa Askari wa Wanyama Pori, au Askari wa majini iwe kwenye Mito, mabwawa, maziwa, bahari kubwa na bahari ndogo, tena Askari wa Anga la chini, Kati au anga la juu. Usisahau mambo haya;

Usiiamini Silaha yako kuliko Akili yako. Naam usiitegemee silaha yako Bali itegemee zaidi akili yako. Hata hivyo usiiamini Akili yako kuliko Imani yako. Yaani usiitegemee akili yako zaidi ya Imani yako. Hata hivyo Imani isizidi akili na akili isizidi Imani.

Endapo utakuwa Askari wa kuua, kuangamiza hasa watu wa nchi yako MWENYEWE. Ukatumwa na kiongozi wako, ukamuue mtu Fulani ambaye ni mtu wa nchi yako mwenyewe. Nawe Kwa kujua kabisa mtu Yule Hana hatia isipokuwa Kiongozi wako ameingiwa na roho ya kishetani. Basi umtiapo mikononi mtu huyo uliyeagizwa umuue, usisahau kumpa nafasi ya kutafakari maisha yake.

MPE nafasi ya kutafakari maisha yake walau Kwa dakika tano, tena usisahau kumpa nafasi ya kumuomba Mungu wake, labda amsaidie au amsamehe ikiwa hatamsaidia.

Nawe usijemuua mtu wa nchi yako mwenyewe bila kumpa nafasi ya kuyatafakari maisha yake, tena kumnyima nafasi ya kutubu Kwa Mungu wake.

Kwa maana hiyo ni Haki yake. Kamwe usimnyime. Usipuuze Jambo hili, nawe hautahesabika unahatia ikiwa uliagizwa na Mkuu wako, na hapa ninaposema Mkuu wako namaanisha Mkuu haswa, na Wakuu HAO ni mfano wa hawa; Mfalme, Rais, Mkuu wa Majeshi na jemadari Mkuu katika Taaluma ya kijeshi, Mkuu wa Polisi, au Mkuu wa idara za kipelelezi na kijasusi na Wakuu WA mfano Kama huo
Hao wakikuagiza basi utaenda wala usiwapinge, Ila utende Kwa hekima.

Ikiwa utaishi kwenye nchi ya demokrasia basi usijipendekeze kupitiliza kwa wanasiasa, Usiwe kihere here mbele ya watawala Kwa kutaka kufanya mambo kuwafurahisha, na kuwatukuza, Kwa maana Mtawala hujua Askari wenye Haki na waadilifu, na pia hujua Askari waovu na wenye dhulma.

Dalili moja wapo ya Askari Muovu ni kujipendekeza na kiherehere, ujapokuwa kiherehere Watawala watakutumia kwenye kazi zao Ovu na hatari, nawe utashindwa kukataa Kwa sababu unapenda kuwafurahisha, pengine ukafikiri watazidi kukupenda lakini sivyo, kwani utaangamia Kwa Uovu wako mwenyewe.

Utende kazi yako kwa uadilifu ili Wakuu zako wakutume kazi za uadilifu. Kwa maana Mkuu humtuma Askari kulingana na tabia ya Askari. Ukiwa mwadilifu utatumwa kazi za uadilifu, ukiwa Muovu utatumwa kazi za kiovu.
Ukiwa na akili utatumwa kazi za akili, na ukiwa Mpumbavu utatumwa kazi za kipumbavu.

Basi jihadhari, tena jitahidi kujionyesha kuwa wewe ni mtu Mwema, mwenye haki na unayechukia uonevu na dhulma nao Wakuu wako watakutambua Kwa namna hiyo, nawe utajirahisishia katika Kazi zako.

Usimuonee mtu asiyestahili kuonewa. Wala usichukue Rushwa kwa mtu apataye pesa yake Kwa taabu. Mwenye Sura dhaifu, fukara wa Mali na mavazi. Huyo usichukue chochote mkononi mwako. Endapo utaamua kuwa Askari asiyemuadilifu basi jitahidi utende Uovu Kwa hekima, usije ukaiingiza familia yako katika laana.

Usibishane Na Mkuu wako akuagizapo, ukijua kuwa Mkuu wako amekuagiza kutokana na jinsi ulivyojionyesha tangu siku ya Kwanza. Ukiona amekutuma kwenda kudhulumu basi jua wewe ni mdhulumaji na ulijitambulisha hivyo kimatendo.

Kwa maana hakuna Mkuu atakayemtuma Askari mwenye Moyo laini kwenda kuua, tena hakuna Mkuu atakayemtuma Askari mwema na mwenye haki kwenda kudhulumu. Basi usimzuie wala kumpinga Mkuu wako akuagizapo kutenda kazi fulani kwani yu akituma kulingana na anavyokujua.

Utakapochukua MATEKA, hasa MATEKA WA watu wako mwenyewe, yaani wa nchi yako mwenyewe, basi usisahau kumpa chakula, tena usisahau kumlaza sehemu itakayomfaa, Kama utamtesa usimguse korodani zake kiasi cha kuziharibu, tena usimharibu macho yake, wala usimfire au kumlawiti. Kwa maana Mkono wowote ushikao korodani na kuziharibu anastahili kuuawa, Kwa maana ameharibu kiwanda cha kuzalisha uzao hapa duniani.

Lakini kama utachukua MATEKA wa watu wasiowako mwenyewe, yaani watu wa nchi nyingine, basi waweza kufanya vyovyote utakavyo isipokuwa kumuingilia kimaumbile, ndiko kumfira na kufanya ulawiti, hilo ni kosa na nilaana.

Usitoe Siri za kijeshi Kwa mtu yeyote Yule hata Kama ni mke wako. Ikiwabutafanya hivyo utakuwa umeamua kuwa Msaliti, na siku zote malipo ya Msaliti ni KIFO.

Ikiwa umeagizwa kumkamata Mhalifu, na Yule mhalifu akakimbilia kwenye nyumba ya Ibada, iwe ni kanisani au msikitini au sehemu yoyote panapotajwa jina la mwenyezi Mungu, hata Kama huamini katika Imani hiyo. Basi usije ukajiingiza pasipo AKILI, usiingie katika nyumba hiyo bali utasubiri mpaka mhalifu huyo atakapotoka.

Na ikiwa Mhalifu huyo yu aleta madhara ndani ya nyumba ya Ibada, basi ndipo utakapoomba sala ya kuingia kanisani au msikitini au nyumba yoyote ya Ibada. Kisha ndipo mtamkamata huyo mhalifu.

Lakini kama haleti madhara yu ajificha muacheni mpaka atakapotoka, Kwa maana yoyote amkiliaye Mungu au eneo ambalo Mungu atajwa atasitiriwa mpaka atakapotoka.

Usiue mtu asiye na hatia ikiwa ni Kwa amri yako MWENYEWE. Na ikiwa umeshinikizwa na Wakuu wako basi nilikuambia chakufanya hapo juu.

Usiiache silaha yako nyumbani kwako sehemu ya wazi ambapo mtu yeyote yuaweza kuifikia, na Kama ukiiacha basi Kama ni bunduki isiwe na RISASI. Hata hivyo silaha yako usiiweke mbali Sana ambapo hapafikiki Kwa urahisi asijekutokea adui kwa ghafla ukashindwa kumkabili.

Usipende kujitambulisha Kama Askari katika Mazingira yasiyo ya kazi.
Wala usivae Sare za Uaskari mazingira yasiyo ya kazi.
Tena usipende kutumia jina la Uaskari Kama kinga yako, Bali matendo yako Mema ndio yawe kinga kwako.

Endapo utapewa kazi ya kumpeleleza na kumtafuta Mtu.
Ikiwa mtu huyo hujui alipoenda, na huna taarifa zake za Msingi. Basi anzie mahala pa mwisho uliposikia au kumuona kuwa alikuwepo.
Hata hivyo lazima ujue majina yake matatu ikiwezekana manne, umri wake, Kimo chake, rangi yake, Kama anafamilia au laa.
Kama ameoa ni rahisi zaidi kumpata na kumfuatilia, lakini kama hajaoa basi kazi inaweza kuwa ngumu kidogo japo sio Sana.

Kwa maana mtu yeyote aliyeoa huongeza uwanda wa watu wamjuaoa.

Kama hajaoa, yupo single, ukamtafuta Kwa muda wa wiki moja usimpate, basi usimtafute yeye tena Bali tafuta Baba yake na Babu yake.

Hivyo tumia jina lake la pili na latatu.
Hivyo uliza watu unamtafuta Mzee Fulani Bini Fulani.

Kwa mfano; unamtafuta Robert Chambua Heriel, ambaye sijaoa. Ukanitafuta Kwa wiki mbili usinipate. Basi usijihangaishe tena kunitafuta Kwa jina la Robert, Bali mtafute Mtu aitwaye Mzee Chambua Heriel, tena umtafute Kwa watu wazima wenye uwezo wa kumzaa mtoto mwenye umri Kama wangu.

Wapi utafanya hivyo, maana watu wanahama hama, utatafuta kulingana na taarifa za awali za msingi za Robert Chambua Heriel, mahali alipozaliwa, akasoma shule ya Msingi n.k.

Kama hujui na huna taarifa hizo, basi huwezi nitafuta mpaka upate taarifa hizo Kwanza. Labda uwe na picha lakini pia utafutaji wa picha sio mzuri Sana Kama huna taarifa za msingi za mtu unayemtafuta. Kwa maana unaweza muuliza mtu wa karibu wa unayemtafuta akamoa taarifa kuwa watu wanaokutafuta wamefika.

Usimpeleleze mtu ambaye humjui vizuri.

Endapo utakuwa Askari Magereza, usiwatese Sana Wale wote unaowaona waliingizwa Jela kimakosa, tena usiwatese watumishi wa Mungu ikiwa waliingizwa jela Kwa kuitetea haki. Tena usiwapendelee wafungwa wenye vipato Kwa vipato vyao ikiwa ni wahalifu.

Usimuamini yeyote katika Kazi yako ya Uaskari.

Kwa Leo Taikon naomba niishie hapa.
Niwatakie majukumu Mema.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Airport, Dar es salaam
 
kuna wajinga wataona kama umewasema watu flani flani . natamani kila askari asome.

sijawahi kusoma uzi mkali na uliosimama kama huu. kuna muda nilikuwa nahsi kama nasoma kipande cha biblia kilichokataliwa.
 
kuna wajinga wataona kama umewasema watu flani flani . natamani kila askari asome.

sijawahi kusoma uzi mkali na uliosimama kama huu. kuna muda nilikuwa nahsi kama nasoma kipande cha biblia kilichokataliwa.


Ndivyo Dunia ilivyo Mkuu
 
.
20220129_083321.jpg
 
Back
Top Bottom