Utake usitake huu ndio ukweli, jiandae kisaikolojia

Utake usitake huu ndio ukweli, jiandae kisaikolojia

Ni sahihi kabisa, lakin pia jambo hili sio tu kubadilisha mindset za graduates hata serikali ijitafakari, hivi inakuaje tunajisifia kutoa mikopo ya 100% kwa vijana ilihali watarudi kukaa tu nyumbani? kwanini tusiwekeze kwenye kuinua fursa za kujiajiri zaidi?
 
Serikali ingejikita kwenye kutoa nafasi nyingi zaidi kwa vijana kujifunza ujuzi kwenye vyuo vya kati badala ilivyokuwa inafanya kuvibadili vyuo vya kati kuwa vyuo vikuu. Hawa vijana wanaohitimu vyuo vya kati ndo watendaji kazi hasa kuliko kujaza graduates ambao wanavaa suti na tai waende kukaa ofisini.
 
Nchi hii haina tatizo la Ajira.
Dunia haijawahi kuwa na Tatizo la Ajira.

Isipokuwa wapo watu wanaotengeneza tatizo lionekane lipo Kwa maslahi Yao ili wapate Watumwa.

Ni Sawa na Wachungaji wa michongo wanaolazimisha kuwaambia watu wamelogwa ilhali hawajalogwa isipokuwa wao ndio wanawaloga Kwa maneno Yao ili wajipatie Pesa
 
Msomeshe mwanao mpka akishajuwa kusoma na kuandika inatosha sana, kama una vijibiashara bas akifika form4 sio mbaya na akimaliza mpeleke short course za biashara ama chuo chochote cha ufundi ama chuo cha kumkazia na language muhimu za kimataifa maana siku hizi lugha ni muhim ktk biashara hivyo ndivyo vya muhimu.

mwaka mmoja unamtosha sana kuelewa mambo ya msingi, baada ya hapo anza kukaa nae ktk biashara yako ukimfunza A- Z kuanzia faida&Hasara na tricks za kuwin ktk biashra hiyo, hakikisha unammpa jukumu kubwa na ajitambue kuwa siku yoyote hayo majukumu yatabaki kuwa yake bila kukutegemea, mfanye mwanao aweze kuishi bila uwepo wako.

Mfanye mwanao aone mambo ya starehe+bata ktk maisha ni kitu cha kawaida, namaanisha mfunze matumiz sahihi ya pesa, atakapolelewa kuwa pesa ya mtaji&saving huwa haiguswi wala haichezewi no matter what, atumie faida atakavyo lkn si kuchezea source ya shughuri yenu inayowapa kipato,
Kwa namna hiyo mwanao hata akiwa wa hovyo kiasi gan, hata awe na matumiz mabovu ya pesa na tamaa za hovyo, ataogopa kuharibu shughuri yenu, pia hata mambo ya anasa atayafanya lkn kwa displine, na hiki ndicho wenzenu huko dunian hufanya, unaweza muona mtoto wa mtu anaspend more than 2mil per day ktk ulevi na kuhonga ukamuona muharibifu wa pesa, kumbe mwenzako hesabu zake zinamruhusu kukitumia kile kipande cha faida aipatayo ktk shughuri yake, i mean mfanye mwanao aone pesa na matumiz ya pesa ni jambo la kawaida sana, sio pesa zimuogopeshe.

Kwa hakika kama nchi tulishachelewa sana kujuwa dunia inakwenda vip, kizaz cha sasa sio cha kuhangaika tena na elimu ya kuchapana viboko, kukalilishana past papers, na kufanyishana ma assignments ya kipumbavu,
hili la kukalili na kusoma kwa bidii tuwaachie baadhi ya fani ambazo ni muhimu kwa jamii mfano, udactari napo wasomeshwe wananchi wachache wakwenda kujazia jazia nafasi wazi zinazohitajika kila mwaka😂.
Mim mtoto wangu atakuwa mwanafunz wa kwanza kula bata akiwa mwanafunzi, i mean sitotaka akimbizane na hizo syllabus zinazowachosha wanafunzi kwa mizigo ya masomo, hata akichelewa kujuwa kusoma, isn't a case kwangu, hata akifeli sana mi sijari, chamuhimu amalize la7 na uwezo wa kusoma&kuandika, pia kuzungumza lugha ngeni, hiki ndicho cha muhimu maana kitamsaidia ktk sensitive&productive issues.
 
Ikiwa mfumo wa elimu unamuandaa mtoto aajiriwe ndio utamfanya mwanafunzi afikirie kujiajiri, basi tunatwanga maji kwenye kinu.
Wala siyo kuwa mfumo WA Elimu ni mbaya kiivyo Ila kiuhalisia sekta nyingi za kiuchumi zilipigwa kabali hasa sekta binafsi taasisi nyingi binafsi hazikuajiri Kama inavyotakiwa na nyingine Hadi kufikia kupunguza wafanyakazi serikalini Napo walipunguza wafanyakazi Kwa kisingizio cha vyeti feki na kibaya zaidi hata hawakuajiri kufidia magepu yaliyoachwa Sera za kiuchumi ndyo zilitufikisha apa wala tusilaumu mfumo waelimu
 
Kuenda kazini kwa kujisikia...
Kuripoti kituo cha kaz na kurudi baada ya miezi 3....
Kazi bila interview.....
Ttz la ajira lipo ila kama mawazo ndio kama hayo apo juu bas taifa lina safar ndef na ndio maana magufuli alichukiwa sana
Watu ni kama hawataki kufanya kazi wanataka kupokea mishahara tu 😳😳😳
 
Mpaka Mtu unajiuliza hakuna wanaostaafu? Wanaokufa?

Gap yao inafidiwa na nani?
Nimecheka mbavu cna hapa, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kazi ipo kubadili elimu kuwa pesa..😁
Miaka inavyozidi kwenda vijana wanaanza kujitahidi kubadili elimu kuwa pesa. Ni kubadirisha tu mtazamo wa maisha, ni faraja kuona kijana anafungua genge au mgahawa au anauza matunda kwa namna ya kisomi kitaalam zaidi. Kwa wakat tuliopo sitegemei kuona kijana anafungua biashara kilimo au ufugaji then anaendesha mradi huo kama zaman wazee wetu walivyofanya...
Kinacho takiwa ni vijana watambue ni lazima kuanza chini ktk mradi wowote ule, huwez kuanza mgahawa leo baada ya mwezi uwe mkubwa kama wa KFC
 
Kuenda kazini kwa kujisikia...
Kuripoti kituo cha kaz na kurudi baada ya miezi 3....
Kazi bila interview.....
Ttz la ajira lipo ila kama mawazo ndio kama hayo apo juu bas taifa lina safar ndef na ndio maana magufuli alichukiwa sana
Watu ni kama hawataki kufanya kazi wanataka kupokea mishahara tu 😳😳😳
Mkuu hizo zama zilishapita sikuhiz watumish wa umma wanatimiza majukum yao na ukizingatia changamoto ya ajira ni kubwa mtu anafanya bidii kazin ili asipigwe chini...
Zamani watumish wa umma walikua wanasumbua kwasabab walikua wachache na wasomi wa kuziba nafas zao walikua wachache, tofaut na sikuhiz ikitangazwa nafas 1 ya kazi waombaji ni 10,000
All in all kama taifa tumepiga hatua ktk uwajibikaji ktk kazi, mapungufu mengine ni madogo ambayo yapo ndan ya uwezo wa mtu na serikal kuyaondoa.
 
Nchi hii haina tatizo la Ajira.
Dunia haijawahi kuwa na Tatizo la Ajira.

Isipokuwa wapo watu wanaotengeneza tatizo lionekane lipo Kwa maslahi Yao ili wapate Watumwa.

Ni Sawa na Wachungaji wa michongo wanaolazimisha kuwaambia watu wamelogwa ilhali hawajalogwa isipokuwa wao ndio wanawaloga Kwa maneno Yao ili wajipatie Pesa
Nimekuelewa sanaaa hapo
 
Kuenda kazini kwa kujisikia...
Kuripoti kituo cha kaz na kurudi baada ya miezi 3....
Kazi bila interview.....
Ttz la ajira lipo ila kama mawazo ndio kama hayo apo juu bas taifa lina safar ndef na ndio maana magufuli alichukiwa sana
Watu ni kama hawataki kufanya kazi wanataka kupokea mishahara tu 😳😳😳
Exactly.
 
Mr Director popote ulipo ndugu big up kwako , nimekusoma nimekuelewa sana , bado kuna haja jamii ya kitanzania kufunzwa kuwa elimu si kupata pesa ila kuwa na maarifa ya kupata hiyo kheri , shida ni kuwa bado wazazi na walezi hiyo hali hawajaikubali na kuilewa hivyo kutwa kucha kuwasumbua vijana vipi utaajiliwa lini ?

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Na

Nashukuru mkuu...
 
Back
Top Bottom