Utalii: Simba 17 wahamishiwa katika hifadhi ya taifa ya Burigi - Chato

Utalii: Simba 17 wahamishiwa katika hifadhi ya taifa ya Burigi - Chato

Watakula nini?..... wanaenda kufaa njaa hao
Kuna wanyama wadogo wadogo na wakubwa Wala majani japo siyo wengi sana,na mzigo ambao Simba 17 wanapiga kwa siku,nadhani Ni miezi mitatu tu wanyama watapungua.
 
Watanzania bwana soma hapo ili ujue simba wapo huko long time ago mnabishana tu Bure Biharamulo Game Reserve

Geographical area coverage ya B'mulo Game reserve ni 1300 square kilometer, baadhi ya sehemu ya Game reserve ni thick forest na nyingine ni Savannah, actually uwanda wa savannah ndio ina-cover mpaka Burigi, Kimisi,Karagwe na Kitengule; Simba hawana jadi ya kuishi/kaa kwenye misitu minene - ndicho nilikuwa namaanisha.
 
Nilichogundua watu wengi hamuielewi jiographia ya Burigi vizuri. Burigi sio kile kipande katikati ya Biharamulo na Muleba na Chato. Burigi imeizunguka Wilaya ya Biharamulo inaambaa mpaka kule karibu na Rusumo na inaingia hadi Kimisi.

Hoja ya misitu minene na kwamba hakuna plains ni dhaifu na inaongelewa na watu wasioijua hifadhi bali wapita njia ya Biharamulo - Muleba. Kimisi game reserve haina misitu ni savannah na ni sehemu ya Burigi National park. Ziwa Burigi lenyewe linaonekana kwa urahisi ukipita njia ya Kimisi Benaco - Karagwe. Chato yenyewe haina msitu wowote wa kutisha. Msitu pekee na ambao watu humu wanajua ndio Burigi ni poli la Kasindaga.

Kwa wasiojua mpaka wa Akagera National Park (Rwanda) na Burigi Chato ni mto Kagera. Kama Simba wanaweza kuishi Akagera tunachotakiwa ni study aina ya Simba waliopo kule ndio hao hao waletwe upande wa Burigi.

Hata zamani kabla ya wafugaji kuvamia hifadhi, Burigi ilikuwa na wanyama wengi wakiwamo Simba (Simba hawa walikuwa wembamba warefu), Swala, Twiga etc. Kikichowaondoa na ufugaji na uwindaji haramu.
The right perspective

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii bugiri chato imekuja kuwa tatizo kubwa! Kila kitu bugiri chato!
 
Geographical area coverage ya B'mulo Game reserve ni 1300 square kilometer, baadhi ya sehemu ya Game reserve ni thick forest na nyingine ni Savannah, actually uwanda wa savannah ndio ina-cover mpaka Burigi, Kimisi,Karagwe na Kitengule; Simba hawana jadi ya kuishi/kaa kwenye misitu minene - ndicho nilikuwa namaanisha.
Ulishaenda ngorongoro highland forest? Kwa taarifa yako kule simba wako wengi ni ni closed forest kuliko hiyo unayoongelea ya burigi chato au selous kule ilonga karibu na mbarangandu
 
Wanyama hawashindwi kuvuka mto hata uwe na kasi gani, tume shuhudia mara ngapi Nyumbu wakivuka mto Mara kwenda Masai Mara Kenya.
Kwa sababu unataki ligi ya ushandani sawa umeshinda. Lakini elewa kasi ya mtirieiko wa maji ya mto Mara kamwe huwezi ilinganisha na kasi ya mto Lubuvu. Pale hakuna mnyama ataweza kukatiza na akijaribu lazima asombwe na maji. Hato mto Mara unaousemea kuna baadhi ya kipindi nyumbu hawavuki. Hasa wakati huu wa masika hakuna nyumbu anakatiza.

Kwa uumbaji wa Mungu amewapa uelewa wa mda maalum wa kuvuka ambao ni wakati mvua zinataka kuanza kunyesha. Ndiyo maana utawasikia wenyeji wakisema nyumbu wakiona dalili mawingu na mwanga wa radi Kenya huvuka mto na kwenda nchini Kenya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Njia pekee ya kuweza kumhamisha mnyama kutoka katika natural habitat yake ni labda umfunge kwenye cage (zoo) na fences ambazo zitamzuia kurudia katika makazi yake ya zamani ambako ndio ali thrive.

Blind political move.
Inaitwa animal orphanage
 
Nadhani wanasiasa wanafikiri wataweza kuifanya Burigi Chato sawa na Serengeti au Tarangire.

Ukweli mchungu kuuza safari kanda ya kaskazini ni rahisi zaidi kwasababu mbuga zote maarufu zipo karibu na nirahisi kumshawishi mteja kwenda huko.

Ukishuka Kilimanjaro Airport unakutana na Kilimanjaro National Park 20 kilometer,ARUSHA National Park 30 kilometers,Tarangire 70 kilometers,Manyara 70 kilometer,Ngorongoro & Serengeti 130 kilometers Hii ni parkage moja katika eneo moja.

Rubondo,Kitulo,Mahale & Gombe zipo muda mrefu lakini hazimo miongoni mwa hifadhi zinazoingiza mapato.Zipo kwasababu ya ruzuku from others Park kama Kilimanjaro,Serengeti & Ngorongoro.
Serikali zilizopita hazikujishughulisha na hifadhi za Burigi, Gombe nk. Kama ilivyofanya kwa Ngorongoro, Mikumi nk. We need to diversify tourism products.
 
Hivi ilifanyika mwezi mmoja kabla ya Lissu kuuliza huko twitter mahala aliko bwana hayati màgufool
 
Back
Top Bottom