Bukyanagandi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2009
- 11,061
- 16,753
Tusipo kuwa makini wataishia kwenye mbuga ya wanyama ya huko Rwanda "Akagera!!"
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na Ranchi ya Kitengule yenye uwanda unaofanana na makazi yao ya asiliTusipo kuwa makini wataishia kwenye mbuga ya wanyama ya huko Rwanda "Akagera!!"
Uzalendo kwanzaJumla ya Simba 17 wamehamishiwa katika hifadhi ya taifa ya Burigi huko Chato ikiwa ni hatua ya kuimarisha vivutio vya utalii Kanda ya Magharibi.
Simba hao wamepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Gaguti ambaye amewataka wananchi wa maeneo hayo wawe wakarimu wakati wa kuwapokea na kuwahudumia watalii.
Source: ITV habari!
Jumla ya Simba 17 wamehamishiwa katika hifadhi ya taifa ya Burigi huko Chato ikiwa ni hatua ya kuimarisha vivutio vya utalii Kanda ya Magharibi.
Simba hao wamepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Gaguti ambaye amewataka wananchi wa maeneo hayo wawe wakarimu wakati wa kuwapokea na kuwahudumia watalii.
Source: ITV habari!
Na Ranchi ya Kitengule yenye uwanda unaofanana na makazi yao ya asili
Sent using Jamii Forums mobile app
Sishabikii mbuga ila natoa taarifa kuwa Simba walikuwepo kabla ya barabara za Muleba Biharamulo na Muleba Chato kuwekwa lami. Wanaoifahamu barabara ya Muleba Biharamulo kuna mlima unaitwa mlima wa Simba.
Watetezi wa haki za wanyama wapo wapi? Hawa simba wanatendewa ukatili sana aisee. Huko Chato simba ataishije? Ecosystem ya huko mbona haikuwa na simba originally? Kwanini huyu Jiwe anafikiri kuwa mbuga zilizopo zilitengenezwa kwa maagizo? Afrika wake up.
Hiyo hifadhi siku zote ilikuwa mkoa wa Kagera. Imekuwaje Chato, Mkoa wa Geita?
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo unabishana na Msomi wa kemia?Simba hawakai porini, wanapendelea savannah, wataondoka tu huko burigi.
Hapo mimi natofautiana na wewe na kumuunga mkono Waziri.Kati ya hifadhi zote Kilimanjaro ndio inaingiza fedha nyingi ikifuatiwa na Serengeti.
Serengeti inatembelewa na watalii wengi kuliko hifadhi zote lakini kimapato kilimanjaro inaongoza.
Kwanini Kilimanjaro inaongoza kimapato wakati inazidiwa idadi ya wageni wanaotembelea Serengeti?.
Ipo hivi mtalii anayetembelea Serengeti anaweza kutumia siku moja au mbili baada ya hapo ataondoka either kwa gari au ndege.Mtalii anayepanda mlima atatumia siku 7 hakuna usafiri wa gari ni miguu so siku atakazo tumia hifadhini ni nyingi na hizo siku maana yake ni fedha nyingi zaidi.
Nilikuwa namshangaa sana tena sana Waziri wa Utalii alipokuja na wazo la kutumia magari ya nyaya (sijui kama ni lugha sahihi) maana yake mtalii atatumia siku chache na ajira ya wabeba mizigo itaondoka.
Ni kweli, ndio uwanda huo huo wa Kimisi kwenda Karagwe hauna tofauti na Serengeti na Ngorongoro ila misitu ya Chato, Biharamulo na Kasindaga ni vigumu Simba kuishi kwenye enviroment zenye misitu minene.
Nilichogundua watu wengi hamuielewi jiographia ya Burigi vizuri. Burigi sio kile kipande katikati ya Biharamulo na Muleba na Chato. Burigi imeizunguka Wilaya ya Biharamulo inaambaa mpaka kule karibu na Rusumo na inaingia hadi Kimisi.
Hoja ya misitu minene na kwamba hakuna plains ni dhaifu na inaongelewa na watu wasioijua hifadhi bali wapita njia ya Biharamulo - Muleba. Kimisi game reserve haina misitu ni savannah na ni sehemu ya Burigi National park. Ziwa Burigi lenyewe linaonekana kwa urahisi ukipita njia ya Kimisi Benaco - Karagwe. Chato yenyewe haina msitu wowote wa kutisha. Msitu pekee na ambao watu humu wanajua ndio Burigi ni poli la Kasindaga.
Kwa wasiojua mpaka wa Akagera National Park (Rwanda) na Burigi Chato ni mto Kagera. Kama Simba wanaweza kuishi Akagera tunachotakiwa ni study aina ya Simba waliopo kule ndio hao hao waletwe upande wa Burigi.
Hata zamani kabla ya wafugaji kuvamia hifadhi, Burigi ilikuwa na wanyama wengi wakiwamo Simba (Simba hawa walikuwa wembamba warefu), Swala, Twiga etc. Kikichowaondoa na ufugaji na uwindaji haramu.
samahani twende taratibu hapa kuna kitu nataka nijifunze. Kabla ya mnyama kuhamishwa kuna approach zipi zinafanyika ili kuhakikisha au kujiridhisha mahitaji ya mnhama huyu ndani ya ikolojia x ya hifadhi fulani ni sawa na mahitaji yaleyale ya ikolojia y ndani ya hifadhi fulani?Hawajui chochote ndg Sina imani Kama haya maamzi yamefanywa na wahifadhi nahisi watakuwa wanasiasa.
Kama wataweza kuishi Hilo eneo ambalo Lina mistu mikubwa Basi hata sokwe wataweza kuishi Serengeti au Tarangire
Ni vitu vingi,ikiwa Ni pamoja na...samahani twende taratibu hapa kuna kitu nataka nijifunze. Kabla ya mnyama kuhamishwa kuna approach zipi zinafanyika ili kuhakikisha au kujiridhisha mahitaji ya mnhama huyu ndani ya ikolojia x ya hifadhi fulani ni sawa na mahitaji yaleyale ya ikolojia y ndani ya hifadhi fulani?
Kama ninavyokuota wewe
Chato itafwanana na Gbadolite ya Mobutu Seseseko Kuku wa GbenguChato itakuwa ka Nairobi
You are talking of something else. The link has a lot of nonsense information. Biharamulo Game reserve is just part of the larger Burigi Chato.![]()
Biharamulo Game Reserve
Biharamulo Game Reserve The Biharamulo Game Reserve is found in Tanzania. It was established in 1959.The reserve is situated in Kagera region in the North Western part of Tanzania and covers an area...shivaworldtours.weebly.com
Hakuna cha kushangaza hapo. Chato ilikuwa ni sehemu ya Wilaya ya Biharamulo mkoa wa Kagera mpaka pale mkoa wa Geita ulipoanzishwa. Hiyo hifadhi iko mkoa wa Kagera kwa sehemu kubwa na kidogo mkoa wa Geita.Hiyo hifadhi siku zote ilikuwa mkoa wa Kagera. Imekuwaje Chato, Mkoa wa Geita?
Sent using Jamii Forums mobile app