Utalii: Simba 17 wahamishiwa katika hifadhi ya taifa ya Burigi - Chato

Utalii: Simba 17 wahamishiwa katika hifadhi ya taifa ya Burigi - Chato

Sishabikii mbuga ila natoa taarifa kuwa Simba walikuwepo kabla ya barabara za Muleba Biharamulo na Muleba Chato kuwekwa lami. Wanaoifahamu barabara ya Muleba Biharamulo kuna mlima unaitwa mlima wa Simba.
Wameenda wapi?
 
Sio uchawi ni ukweli, angalia maeneo yenye idadi kubwa ya simba nchini, ni uwanda wa wazi. Hata uwabebe uwapeleke wapi, kama wako huru wataondoka tu na kurudi savannah, wakiwa njiani wataua mifugo ya watu pengine pamoja na watu.
Hawajui chochote ndg Sina imani Kama haya maamzi yamefanywa na wahifadhi nahisi watakuwa wanasiasa.
Kama wataweza kuishi Hilo eneo ambalo Lina mistu mikubwa Basi hata sokwe wataweza kuishi Serengeti au Tarangire
 
Ni evolving story tu, habari inaanzia hapa hao Simba walipotokea.
 
Sishabikii mbuga ila natoa taarifa kuwa Simba walikuwepo kabla ya barabara za Muleba Biharamulo na Muleba Chato kuwekwa lami. Wanaoifahamu barabara ya Muleba Biharamulo kuna mlima unaitwa mlima wa Simba.

Simba hao wa kipindi hicho walikuwa na mazoea ya kushambulia/kuua watu na mifugo... Walitokomezwa wote... Ni dhahiri kuwa hata hawa Simba wa Sasa nao hawatadumu muda mrefu!
 
Anae kaa porini ni Simba malala wengine watarudi waliko toka
Yajayo yana furahisha uko tayari
 
Hao wanao wapeleka huko ni wataalamu wa wanyama nina imani wanajua wanachokifanya.
Mifano ipo wazi! Wataalamu waliwahi kuwapeleka wanyamapori hifadhi ya kisiwa cha Rubondo huko huko Geita... Mpaka sasa idadi ya wanyamapori waliobaki haijulikani...
Serengeti kule Faru walipelekwa hadi hii leo hawajuhi kwa uhakika wapo wapi...
Kule Mkomazi (Same) walipelekwa Faru na Mbwa mwitu... Mpaka leo ni shida tu...!
Unapoamua kuwaamini wataalamu jitahidi pia uwe na akili ya kufikiria mambo kwa kina sana!
Usije ukafadhaika ukisikia yale yale ya Muganza, Biharamulo, Mukuranga na Mbagala yakijirudia... Visa vya Simba-Mla-Watu!
 
Jumla ya Simba 17 wamehamishiwa katika hifadhi ya taifa ya Burigi huko Chato ikiwa ni hatua ya kuimarisha vivutio vya utalii Kanda ya Magharibi.

Simba hao wamepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Gaguti ambaye amewataka wananchi wa maeneo hayo wawe wakarimu wakati wa kuwapokea na kuwahudumia watalii.

Source: ITV habari!
Ninachojua mimi hao samba wataenda kufa huko, na wakifa hatutaambiwa, na ukihoji kufa kwao utaambiwa mchochezi na utabambikwa kesi ya utakatishaji fedha
 
Na huko watawamaliza Sokwe wote wa Mlima virunga!

Simba Hawaii kwenye Misitu minene kama ya Biharamulo, Gombe au Virunga. Wanaishi sehemu zenye mvua chache, nyasi ndefu na vichaka vya hapa na pale.

Sasa Burigi Chato itakuwaje? ....Mungu tupe Maarifa zaidi ya Matamanio ya mioyo yetu.
Binafsi mimi sielewi aina ya viongozi tulionao kwa sasa na uwezo wao kifikra wa kushauri, hapa watakuwa wamepokea maelekezo au maagizo kutoka kwa meko na wao wakatekeleza bila kuhoji, hao samba sijui kama wataweza kuishi huko.
 
Ninachojua mimi hao samba wataenda kufa huko, na wakifa hatutaambiwa, na ukihoji kufa kwao utaambiwa mchochezi na utabambikwa kesi ya utakatishaji fedha

Niiweke vizuri... Kabla ya kufa watakuwa washaua na kuleta madhara anuwai!
 
Mwenye kujua idadi ya wanyama waliwao ,walao nyasi Burigi atujuze, nimepita karibuni huko ni nadra kumuona hata swala, sasa hao simba ,chui ,watakula nini. Serengeti wanyama na kwingineko waliwao ni utitiri, huko nahofia wafugaji jirani na binadamu pole yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na huko watawamaliza Sokwe wote wa Mlima virunga!

Simba Hawaii kwenye Misitu minene kama ya Biharamulo, Gombe au Virunga. Wanaishi sehemu zenye mvua chache, nyasi ndefu na vichaka vya hapa na pale.

Sasa Burigi Chato itakuwaje? ....Mungu tupe Maarifa zaidi ya Matamanio ya mioyo yetu.
Dah, mkuu umeongea kwa uchungu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sishabikii mbuga ila natoa taarifa kuwa Simba walikuwepo kabla ya barabara za Muleba Biharamulo na Muleba Chato kuwekwa lami. Wanaoifahamu barabara ya Muleba Biharamulo kuna mlima unaitwa mlima wa Simba.
Kwa kawaida simba hukaa sehemu yenye chakuka ambacho ni wanyama. Mapori yote hayo likiwemo pori la Moyowosi miaka ya nyuma lilijaa simba ambao walikuwa wanavamia wafugaji na kuua ng'ombe na mbuzi, kilichowahamisha ni uwindaji haramu!.

Tanzania imekaa kama sinia kubwa ambapo upande wa magharibi ukivuka mpaka unapambana na miinuko na milima na mabonde ya hatari. Maeneo yote haya yana mbuga na uoto wa savanna ambao hautofautiani sana na mbuga zilizoko Kilimanjaro Arusha na Manyara, Kimsingi kama ujangiri utadhibitiwa, ndani ya miaka mitano ijayo tutashudia makundi makubwa ya wanyama katika mbuga zilizotangazwa.
 
TUMEPATA DAWA YA WAFUGAJI WANAOVAMIA HIFADHI. HUKO BURIGI WAHIFADHI WAMEPATA AHUENI YA KUPAMBANA Na WAVAMIZI WAFUGAJI NA WENGINEO. WAMELETWA ASKARI KWELI KWELI. Je wakikosa swala wananchi wajitayarishe kama huko TUNTURU. WAKIKOSA SWALA WANAVAMIA WATU!!!
 
Back
Top Bottom