Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 20,654
- 35,887
Mlima Kilimanjaro unahamishwa lini ?
Kati ya hifadhi zote Kilimanjaro ndio inaingiza fedha nyingi ikifuatiwa na Serengeti.
Serengeti inatembelewa na watalii wengi kuliko hifadhi zote lakini kimapato kilimanjaro inaongoza.
Kwanini Kilimanjaro inaongoza kimapato wakati inazidiwa idadi ya wageni wanaotembelea Serengeti?.
Ipo hivi mtalii anayetembelea Serengeti anaweza kutumia siku moja au mbili baada ya hapo ataondoka either kwa gari au ndege.Mtalii anayepanda mlima atatumia siku 7 hakuna usafiri wa gari ni miguu so siku atakazo tumia hifadhini ni nyingi na hizo siku maana yake ni fedha nyingi zaidi.
Nilikuwa namshangaa sana tena sana Waziri wa Utalii alipokuja na wazo la kutumia magari ya nyaya (sijui kama ni lugha sahihi) maana yake mtalii atatumia siku chache na ajira ya wabeba mizigo itaondoka.