Utalii: Simba 17 wahamishiwa katika hifadhi ya taifa ya Burigi - Chato

Utalii: Simba 17 wahamishiwa katika hifadhi ya taifa ya Burigi - Chato

Jumla ya Simba 17 wamehamishiwa katika hifadhi ya taifa ya Burigi huko Chato ikiwa ni hatua ya kuimarisha vivutio vya utalii Kanda ya Magharibi.

Simba hao wamepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Gaguti ambaye amewataka wananchi wa maeneo hayo wawe wakarimu wakati wa kuwapokea na kuwahudumia watalii.

Source: ITV habari!
Wote hao wataenda Rwanda kwa kina Magu.

MnzilanKENDE
 
Sishabikii mbuga ila natoa taarifa kuwa Simba walikuwepo kabla ya barabara za Muleba Biharamulo na Muleba Chato kuwekwa lami. Wanaoifahamu barabara ya Muleba Biharamulo kuna mlima unaitwa mlima wa Simba.
Unajua kuna matabaka mangapi ya simba? Hao waliokuwemo humo siyo sawa na hawa wa savanna wanaolazimishwa kuhamia huko,unajua tofauti ya simba wa serengeti na wa ngorongoro? Japo ni maeneo jirani kabisa? Jifunze, uelewe,ndipo uongee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo habari ilikuwa kama wiki mbili au moja nyuma.

Hao Simba wamekamatiwa huko huko mkoa wa Geita kama sikosei, kuna familia mbili zilisogea sana karibu na makazi ya watu na kuweka kambi. Baadae wakaanza kuvamia mifugo na kujeruhi watu kadhaa.

Walipo ripotiwa jamaa wa hifadhi ya taifa wakaenda kuwakamata na ikaamuliwa wakishikwa wote 17 watapelekwa Chato. Na sehemu ya zoezi lenyewe la ukamataji kwenye TV ilionyeshwa na wananchi waliokuwa na wasiwasi walihojiwa.
 
Siyo Geita, nafikiri ilitokea vijiji vinavyopakana na mbuga ya Serengeti mkoa wa Mara ndo wakaamua kupunguza baadhi ya familia za Simba.
 
Simba waliopelekwa ni 17 kati yao mmoja jike alikuwa na mamba Tayari Kazaa watoto wakati wenye afya nzuri.

Kwahiyo Simba waliopelekwa Burigi Chato ni Simba 20.
 
Siyo Geita, nafikiri ilitokea vijiji vinavyopakana na mbuga ya Serengeti mkoa wa Mara ndo wakaamua kupunguza baadhi ya familia za Simba.
Inawezekana ni Mara ila kulikuwa na familia mbili kwenye habari niliyoona, mpaka maafisa wa wanyamapori wanahojiwa walikuwa washa kamata familia moja yenye Simba kumi. Wanaanza awamu ya pili ya familia nyingine yule jamaa akawa anasema inabidi wafanye ivyo kwa sababu Simba awana utamaduni wa ku socialise familia tofauti ivyo awawezi kuwaweka pamoja.

Hila wote wakikamtwa hatma yao ilikuwa watapelekwa Chato.
 
Back
Top Bottom