Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,194
- 911
Mikakati ya makusudi ya kukuza utalii wa mikutano (MICE) ndani ya Jiji la Arusha imeanza kuzaa matunda, huku makundi mbalimbali ya kijamii yakishuhudia manufaa makubwa ya kiuchumi kuanzia ngazi ya mtu mmoja mmoja hadi jamii kwa ujumla.
Miongoni mwa wanufaika wakuu ni madereva wa taksi ambao wameeleza kuwa mikutano mikubwa ya kimataifa inayofanyika mkoani hapa inaimarisha vipato vyao kupitia ongezeko la abiria. Wadau hao wamesema mwingiliano huo mkubwa wa wageni umechangamsha taswira ya Jiji la Arusha na kufungua milango ya fursa mpya za kibiashara.
Ukuaji huu unathibitishwa na ujio wa washiriki zaidi ya 3,000 wanaohudhuria Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Huduma za Afya ya Msingi unaoendelea sasa katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) huku mkutano wa Umoja wa mabunge Duniani IPU ukitarajiwa kufanyika hivi karibuni.