Bufa
JF-Expert Member
- Mar 31, 2012
- 12,599
- 26,263
Maendeleo ya vitu bila ya kuwepo kwa Haki, Uhuru na Demokrasia ni sawa na kazi bure, work done equal to zero!
Wananchi wengi zaidi waliopo kwenye hizo nchi hawana Uhuru Wala demokrasia, kwa kifupi ni kwamba hawafurahii maisha wakiwa kwenye hizo nchi zao. Karibia wananchi wote kabisa waliopo kwenye hizo nchi wamegeuzwa kuwa Mateka wa Watawala.
Utawala wa China ndio unaongoza duniani kwa Sasa kwa kunyonga Watu wengi zaidi nje ya mfumo wa kimahakama. Aidha, utawala wa Urusi pia unaongoza hapa dunianu kwa kuwafanyia uovu/uhalifu wananchi wake wasio na hatia ambao wanakosoa utawala. Idara ya Usalama wa taifa ya Urusi yaani KGB/FSB imekuwa ikitekeleza operesheni hatari Sana za udhalimu dhidi ya raia kwa kuwateka, kuwatesa, na kuwaua, kila siku raia wa Urusi wamekuwa wakiuawa kwa kuwekewa sumu na Mawakala wa Siri kutoka KGB/FSB.
But all in all, China kwa sasa ina sera mseto za itikadi ya siasa za ukomunisti, ujamaa, ubeoari, n.k.
Nini kinafanya TZ isi adopt sera mseto au za ubepari hivi sasa? Nyerere bado yupo kukataza hilo hivi sasa?