Utamaduni wa Watanzania kudhani masuala ya siasa hayatuhusu utatugharimu sisi na vizazi vyetu


Nini kinafanya TZ isi adopt sera mseto au za ubepari hivi sasa? Nyerere bado yupo kukataza hilo hivi sasa?
 
Umesema ukweli kabisa! Sisi ni makondoo na mazombi! Tozo za kununua Esther! Halafu tuna mwenge, ndio tatizo!
 
Kumbe kubadilika inawezekana? Nini kinafanya TZ isibadilike au Nyerere bado anakataza mabadiliko? Point is, kuendelea kumlaumu mtu aliyeondoka madarakani over 30yrs ago kwa changamoto za sasa ni ufinyu wa mawazo.
Atalaumiwa kama muasisi wa hii mifumo ambayo ni rigid kimabadiliko, brain washing iliyofanyika kipindi chake ina athiri mpaka vizazi vya leo kimaamuzi, kiutawala, almost nyanja zote na hili alijua ila hakuweka mifumo ya ku counter hayo mazingira au haku set in motion kuondoa hizo effects.

But then lawama zote haziwez kuwa zake japokuwa yeye ndio source
So walimfuata
 
Nini kinafanya TZ isi adopt sera mseto au za ubepari hivi sasa? Nyerere bado yupo kukataza hilo hivi sasa?
One things. Fear of unknown. Lakini pia kuna tabaka au ombwe la viongozi ambao wanaogopa kuruhusu mabadiliko hayo kwa kuhofia vizazi vyao havito pata nafasi mbeleni or vitapotea

Matokeo yake imetengeneza vizazi vya hovyo, na sheria za hovyo( si zote)
 

Ni sawa na kumlaumu babu yako kwa setbacks zako. Mzee wako kashindwa ku rectify na wewe umekuwa mtu mzima bado upo pale pale. Hapo tatizo ni wewe.

Kuna mambo alifanya yalikuwa sawa kwa muda na mazingira ya wakati huo, tatizo ni wale waliomfuata kubaki pale pale na hata kizazi cha sasa ni tatizo maana hakifanyi jitihada zozote kubadilika.

Hao Russia, China, Singapore, S. Korea wote walikua na hizi sera na umaskini kama wetu miaka ya uwani ila leo wapo mbali.

โ€œIf you are born poor, it's not your fault, but if you die poor it's your faultโ€ Bill Gates Sr.
 
Nini kinafanya TZ isi adopt sera mseto au za ubepari hivi sasa? Nyerere bado yupo kukataza hilo hivi sasa?
Sababu ni Uhafidhina (Conservativeness) wa CCM. Ccm haitaki mabadiliko, waliopo huko wapo rigid na fikra mgando za "zidumu fikra za mwenyekiti."
 

Uchawi tu unakolezwa kila mwaka ili waendelee kuwa makondoo wa kuchinjwa kile kibatati kinachoitwa mwenge ni cha kupiga vita!!
 
Nyerere huwezi kumlaumu sana
Yeye alikuwa mchanga kwenye siasa na mifumo ya utawala
Hivyo kukosea ilikuwa laZima
Sasa sisi ndo tuyanyooshe mapungufu yake
 
Unategemea nini zaidi iwapo unaishi kwenye nchi ambayo biriani limetengewa hadi siku wanakuletea popote ule na mpishi wake? Kwamba kijana aliyeshiba biriani na kapewa na biriani jingine la kimwili atoke kupigana na polisi?
Kweli kabisa ๐Ÿ˜…๐Ÿ˜€
 
Reactions: Tsh
Baada ya 2035 in shaa Allah akitawala mtanganyika mwenzenu mtapiga kelele kama ivo?
2025 kipindi cha kwanza then 2030 anamalizia kipindi cha pili mpaka 2035 !
Au nimeelewa tofauti bandugu ??!
๐Ÿ˜…๐Ÿ˜€๐Ÿ™๐Ÿ‘
 
Tukijaribu TUNATEKWA, TUNAUWAWA we mwenzetu unaandika kutokea Kenya au upo humu humu.

Mchana chadema unavaa mboga mboga, usiku kilingeni unakuwa kamanda.
 
Kujumuisha kwamba wote hawaijui ni upotofu sana.Wewe ukiulizwa leo maswali ya darasa la tatu kutoka kwenye kitabu toleo la mwaka 1987 utakumbuka?
Na hakuna Nchi yeyote Duniani ambayo Wananchi wake wanaijua Katiba yao yote !
Kila mtu huwa anaijua Katiba katika vijisehemu vidogo vidogo vile vitakavyo mgusa kwenye mambo yake na harakati zake !

Hata hao wanasheria waliosomea Sheria mpaka waangalie kwenye Vitabu vyao vifungu vya Sheria kutoka kwenye kitabu cha Sheria Mama ambayo ndio inaitwa KATIBA !
Mwananchi wa kawaida ataijuaje Katiba yote ???!
Tusidanganyane Bandugu !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ