Utamaduni wa Watanzania kudhani masuala ya siasa hayatuhusu utatugharimu sisi na vizazi vyetu

Utamaduni wa Watanzania kudhani masuala ya siasa hayatuhusu utatugharimu sisi na vizazi vyetu

Kwahiyo China na Urusi hazijaendelea sababu nao walikua wajamaa?
Hizo nchi zimeachana na communist ideas. Wenyewe waliona hawatopiga hatua , wakaachana na mifumo hiyo waka adopt mix of mifumo ya kiutawala ndio wanaenda nayo
 
Utalaumu soka bure. Watanzania hapa mjini wanashiba mno, si rahisi mtu anayepata chakula na anasehemu ya kulaza ubavu ukamshawishi akapigane na wanasiasa. Akitishiwa kidogo anaona ana la kupoteza.

Hapa mjini kuna sehemu unapata hii kwa Tsh 3000. Siku hii inapotea hili unalolitaka litawezekana kiwepesi mno.
View attachment 3119614
Wewe Leo utashiba lakini wanaona na wajukuu inatakiwa uwafikirie
Serengeti unaleta maelfu ya watalii, Sasa inaondoshwa
Bandari zinauzwa
Masai ni wakimbizi kwenye nchi Yao
Tujiulize zaidi kuhusu kesho
Wazee wetu wangeharibu hata ugali samaki tusingekuwa tunakula
 
Watanganyika wamejenga dhana ya kutohoji wala kufuatilia masuala ya kisiasa na kudhani siasa haimunufaishi.

Mtu anaona kwakuwa anakula na kuishi mambo mengine sio ya muhimu, aani kwamba Katiba mpya sio suala linalotuhisu kwakuwa unaamka asbh unapata mkate basi.

Bandari zinauzwa
Serengeti unaenda kuchimbwa madini, kwa baadae Serengeti haitakuwepo, tupo kimya, Sasa vizazi vyetu vitakuta nini? Vitatuona tulikuwa wajinga kiasi gani?

Rushwa serikalini imekuwa kubwa, mali za umma zinauzwa.

Utekaji na mauaji
Tunaona kawaida Kwa kuwa hatujatekwa au kuuliwa sisi au ndugu wa karibu

Huduma mbovu za kijamii
Shule hazina walimu na madawati. Hospital hakuna madawa, watu hawana bima. Maji hakuna, umeme wa uhakika haupo.

Bunge limekuwa kama sehemu ya kuimba mapambio. Bunge limewekwa mfukoni. Bunge la wananchi linatunga sheria za kuwakandamiza wananchi, rejea mambo ya tozo n.k. Tuko kimya tu.

Tujifunze Kenya wao wale sio makondoo kama Watanganyika
Kile kibatali kinaitwa mwenge wa uhuru kina mchango mkubwa katika huu ukondoo wa Watanganyika.
 
Utalaumu soka bure. Watanzania hapa mjini wanashiba mno, si rahisi mtu anayepata chakula na anasehemu ya kulaza ubavu ukamshawishi akapigane na wanasiasa. Akitishiwa kidogo anaona ana la kupoteza.

Hapa mjini kuna sehemu unapata hii kwa Tsh 3000. Siku hii inapotea hili unalolitaka litawezekana kiwepesi mno.

Wapi hii unaipta Mkuu.

Watu wakiwa na hakika ya shibe ni vigumu sana kusumbua..
 
Wewe Leo utashiba lakini wanaona na wajukuu inatakiwa uwafikirie
Serengeti unaleta maelfu ya watalii, Sasa inaondoshwa
Bandari zinauzwa
Masai ni wakimbizi kwenye nchi Yao
Tujiulize zaidi kuhusu kesho
Wazee wetu wangeharibu hata ugali samaki tusingekuwa tunakula
Boss, Tusidanganye, tuweke unafiki pembeni, Hii nchi ina wanasiasa wanaopigania maslahi ya kisiasa wanaoitwa wapinzani ila hakuna mtu wa kupambana na wanasiasa kwa maslahi ya mwananchi.
 
Utalaumu soka bure. Watanzania hapa mjini wanashiba mno, si rahisi mtu anayepata chakula na anasehemu ya kulaza ubavu ukamshawishi akapigane na wanasiasa. Akitishiwa kidogo anaona ana la kupoteza.

Hapa mjini kuna sehemu unapata hii kwa Tsh 3000. Siku hii inapotea hili unalolitaka litawezekana kiwepesi mno.
View attachment 3119614
Duu nimess maziwa yaliyo oza, (mtindi)
 
Wapi hii unaipta Mkuu.

Watu wakiwa na hakika ya shibe ni vigumu sana kusumbua..
Kwa wamama ntilie maeneo mbalimbali mkuu. Kama unaenda kwenye kibanda cha mama ntilie kila siku hashindwi kukupa na mengine ambayo hukutarajia, ndo yanayoendelea kwenye hii nchi.
 
Kwahiyo China na Urusi hazijaendelea sababu nao walikua wajamaa?
Maendeleo ya vitu bila ya kuwepo kwa Haki, Uhuru na Demokrasia ni sawa na kazi bure, work done equal to zero!
Wananchi wengi zaidi waliopo kwenye hizo nchi hawana Uhuru Wala demokrasia, kwa kifupi ni kwamba hawafurahii maisha wakiwa kwenye hizo nchi zao. Karibia wananchi wote kabisa waliopo kwenye hizo nchi wamegeuzwa kuwa Mateka wa Watawala.

Utawala wa China ndio unaongoza duniani kwa Sasa kwa kunyonga Watu wengi zaidi nje ya mfumo wa kimahakama. Aidha, utawala wa Urusi pia unaongoza hapa dunianu kwa kuwafanyia uovu/uhalifu wananchi wake wasio na hatia ambao wanakosoa utawala. Idara ya Usalama wa taifa ya Urusi yaani KGB/FSB imekuwa ikitekeleza operesheni hatari Sana za udhalimu dhidi ya raia kwa kuwateka, kuwatesa, na kuwaua, kila siku raia wa Urusi wamekuwa wakiuawa kwa kuwekewa sumu na Mawakala wa Siri kutoka KGB/FSB.

But all in all, China kwa sasa ina sera mseto za itikadi ya siasa za ukomunisti, ujamaa, ubeoari, n.k.
 
Katiba mpya ya kazi gani?..kenya wanna katiba mpya, matatizo yameisha!?..
Ona huyu naye!

Mkuu unawaza kwa kutumia nini vile!

Kistaarabu ukiona jambo haulielewi, unanyamaza, hauwwzi kupungukiwa chochote.
 
Ukiwekewa glass ya maziwa ya mgando hapa na wito wa maandamano ya katiba pale unachagua nini mkuu? Sema ukweli.
Shibe kwanza, ukiwa na njaa huwezi kuamsha ubongo, binadamu huhifadhi anachosikia, ona, nusa, fundishwa hata kutishwa, binadamu akitaka ufumbuzi wa jambo lake hutafsiri kumbumbu alizo hifadhi na kupata jawabu uwezo wake wa kutafsiri ndiyo huitwa akili, kama hana alichohifadhi atakwenda kwa mtu mwingine na kutatua changamoto iliyojitokeza
 
Shibe kwanza, ukiwa na njaa huwezi kuamsha ubongo, binadamu huhifadhi anachosikia, ona, nusa, fundishwa hata kutishwa, binadamu akitaka ufumbuzi wa jambo lake hutafsiri kumbumbu alizo hifadhi na kupata jawabu uwezo wake wa kutafsiri ndiyo huitwa akili
Bora umesema kweli. Mzalendo mnafiki angejifanya ana hasira kweli na nchi yake kumbe tapeli tu na yeye anapigania kwenye keyboard akiwa na glasi yake ya maziwa.
 
IMG-20241007-WA0000.jpg
 
Acha kulaumu watanzania, laumu wanasiasa ambao wamegeuka kutumikia matumbo yao wala hawaeleweki..., Sio Bongo tu Policitians worldwide are out of touch..., kwahio hao ambao wanapata ruzuku na hio ni kazi yao waanze kueleweka na kuelewesha Watanzania na waeleweke....,

Kuhusu watu kuanza kuhoji na kugoma bado Watanzania hawajabanwa na wana hope na future prospects..., kinachoendelea sasa kikiendelea kuendelea sitashangaa ya French Revolution kujirudia...
 
Bora umesema kweli. Mzalendo mnafiki angejifanya ana hasira kweli na nchi yake kumbe tapeli tu na yeye anapigania kwenye keyboard akiwa na glasi yake ya maziwa.
Walio wengi humu, tunapokaribia uchaguzi huwa wanahilisha kufikiri kizalendo a.k.a kujizima data
 
Hizo nchi zimeachana na communist ideas. Wenyewe waliona hawatopiga hatua , wakaachana na mifumo hiyo waka adopt mix of mifumo ya kiutawala ndio wanaenda nayo

Kumbe kubadilika inawezekana? Nini kinafanya TZ isibadilike au Nyerere bado anakataza mabadiliko? Point is, kuendelea kumlaumu mtu aliyeondoka madarakani over 30yrs ago kwa changamoto za sasa ni ufinyu wa mawazo.
 
Back
Top Bottom