Part 2.
Ipo hivi .. huu ulikuwa ni mtego wa kumnasa Mordechai pasipo kuleta tafrani na mamlaka za uingereza. Ikumbukwe kipindi hiki uingereza ilikiwa ikiongozwa na mwana mama mwenye msimamo na asiyecheka na kima yoyote Margreth Thatcher a.k.a Iron lady.
Hivyo Mossad kwa kumtumia huyu mrembo Cindy, walitaka wamnase kiulaini Mordechai nje ya mipaka ya uingereza ili kuepusha tafrani na kwa wepesi. Na italia ni kwamba tayari mkurugenzi wa ujasusi wa mossad bwana Nahum Admoni na admiral fulvio Martini aliyekuwa mkurugenzi wa ujasusi wa italia walikuwa na urafiki mkubwa sana hivyo zoezi hili lingekuwa jepesi sana . Na zaidi kutokana na ushirika huu ,kamwe isingeweza tokea hata siku moja mamlaka za italia zingekuja kukiri kwamba Mordechai alitekwa kwenye ardhi yake. ..
Sasa basi kwa Bashasha na mahaba mazito ,wapenzi wawili hawa yaani Cindy na Mordy walipanda ndege ya kampuni ya British airways,safari namba 504 hadi rome Italy tarehe 30 September mwaka 1986. Na walifika italia majira ya daa tatu kamili usiku na kupokelewa na derava taxi aliyekuja na maua na kuwakabidhi wapenzi hawa wawili. Kisha akakusanya mabegi yao hadi kwenye gari na kuwaendesha hadi kwa dada yake Cindy 😅 aliyepo hapo italia.. njia nzima Cindy na Mordy ilikuwa ni mwendo wa ea kukisiana 🫂🫂🤗 💋💋 na kukumbatiana njia nzima.
Walifika kwenye nyumba moja ndogo hivi, wakashuka garini na kwenda hadi ndani.. Cindy akafungua mlango na Mordechai akawa wa kwanza kuingia😳😳😳. Ghafla bin vuu kama mwewe akidaka kifaranga mlango ulifungwa Paap na njemba mbili zikamkwida Mordechai Vanunu na kumwangusha chini kwenye sakafu. Ghafla akapigwa sindano ya usingizi hapohapo. Mara paap akaona tu gizagiza. Maskini Mordechai 🤣🤣🤣
Akabebwa juujuu akiwa hajitambui hadi kwenye gari aina ya van kisha moja kwa moja safari ya masaa kadhaa ikaanza kuelekea kaskazini mwa italia kwenye bandari ya La Spezia. Hapo akashushwa na kupakishwa tena kwenye boti za mwendokasi Hadi katikati ya bahari ambapo meli kubwa ya mzigo ya Israel iliyoitwa Tapuz ilikuwa imesimama. Haraka akashushwa na kupakiwa humo melini kisha ikaanza safari hadi ISRAEL. Meli haikutia nanga bandarini Mordechai alishushwa kisha akapakiwa tena kwenye boti nyingine ya mwendokasi hadi ufuoni. Hapo alikabidhiwa kwa maagent kadhaa na maafisa wa polisi waliokuwa wakimsubiri na kumpeleka moja kwenye gereza la Shikma kwenye mji wa Ashkeloni.
Wakati hili zoezi likiendelea mpaka Mordechai kukamatwa na kufikishwa Israel, magazeti mbalimbali duniani yalianza kuchapisha hii habari za Israel kuhusu kumiliki silaha za nyuklia na sehemu zilipokuwa zikitengenezwa ndani ya Israel . Habari hizi zilikuwa ni za moto sana duniani kwa wakati huo.
Baadaye baada ya mlolongo mrefu wa kimahakama ,bwana Mordechai Vanunu alihukumiwa miaka 18 jela kwa kosa la uhaini na ujasusi . Huko duniani yaani Ulaya na marekani alionekana kama shujaa ambaye hakutaka dunia kuangamizwa na nyuklia . Baada ya kutumikia miaka 18 jela jamaa alitoka na kuendeleza maisha yake ya kawaida akiishi mji wa Jerusalem. Demu wake Cindy ndio akawa ammepotea hivyo.
Ila ilikuja kubainika huyo Cindy alikuwa ni mtoto wa milionea mmoja wa kimarekani anayefanya biashara za matairi. Huyu Cindy jina lake halisi lilikuwa ni Cheryl BenTov ñee hanin.
Huyu mrembo kutokana na kuwa na IQ kubwa na ambaye aliwahi tumikia jeshi la IDF, aliajiriwa na mossad. Kutokana na uelewa wa maswala ya kijasusi na pia kumiliki passport ya marekani alijikuta amewekwa kwenye operation hii ya kumnasa Mordechai Vanunu. Baadaye alikuja kustaafu harakati za ujasusi na kwa sasa ni kikongwe anayeishi huko Florida marekani kama mfanyabiashara mkubwa wa real estate