Utamu wa Asali ulivyomkamatisha Jasusi wa Israel kizembe

Upwiru nao ukiusikilizia Sana mwisho wake uta,,,mba Moto utaungua mavuzi ndio haya ya Mordechai
 
View attachment 3517258
Mtoto Cindy aliyemkamatisha Mordy au Mordechai kwa makachero wa mossad
Huyu jasusi Cindy nimempenda, kuanzia ujanja wa kujilengesha na kuweza kumnasa jamaa kisaikolojia na kisha kumsafirisha hadi nchi za mbali kufuata 'tamu' yake tu!

Huyo mwanamke anastahili pongezi kwa kweli.

Na huyo mwanaume tusimlaumu sana kwa kuzebezwa namna hiyo na mwanamke.

Hivi tujiulize, hapa kwetu katika asilimia mia ya wanaume, asilimia ngapi inaweza kuruka hiko hihunzi?

Sasa baada ya kutoka jela jamaa si angelimfuata huyo demu ili aishie hata kuambulia naniliu wakamalizane!

Haiwezekani mtu ule kwa macho halafu uambulie mvua za kutosha 'Ukonga'!

Halafu mwandishi haujatueleza jamaa alizindukia wapi!
 
Huo mtego ni ngumu kuuvuka na mbaya zaidi ukute ni udhaifu wako... . kuhusu huyo demu yeye alikuwa kikazi na alikuwa tayari ni mke wa afisa wa Mossad tayari..sema jamaa alikolea vibaya sana asee.
 
Dah! Mbele wanajali sana uhai wa Mtu...Pamoja na Jamaa kutindinganya uhai wake aliachiwa, ingekuwa Malawi!!!!!
Kama umebahatika kupitia makala moja humu jf iliyoandikwa na memba anaitwa Habibu Anga , OPERATION WRATH OF GOD ya majasusi wa Israel wa Mossad, utagundua wapo Smart sana katika mipango yao... Lakini huyu wangeamua kumuua tu endapo siri hii angeivujisha kwenye nchi ambazo ni maadui wa Israel Hususani za kiarabu... Lakini kwenda uingereza na kuitoa tena kwenye gazeti la Sunday Times ,hii kidogo waliamua kum-spare maisha yake ikawa ponapona yake
 
Dah sasa jamaa baada ya miaka 18 upwiru wote ushakata.
Ila mataifa ya wenzetu yana historia ndefu sana, leo 2026 tunasoma mambo yao makubwa ya miaka 80, 70 kurudi nyuma! Natamani nisome makala kama hizi za kwetu pia!
 
Bonge moja la story kama vile nilikuwa naangalia movie hivi .

Hakuna movie yake maana jamaa huwa wanatumia story kama hizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…