Utamu wa pesa, kwako ni upi?

Utamu wa pesa, kwako ni upi?

Siku zote pesa inatakiwa ikupe mahitaji ya msingi, ndio maana tunatumia nguvu nyingi katika kuzitafuta.

Tunaamini na imethibitika, hatuwezi kuishi miaka 150; mara nyingi tumezidi sana tena kwa wale wachache sana wanaweza kubahatisha miaka 100.

Sasa, maisha ni nini, Je ni kuishi kwa furaha katika maisha yako yote au kuishi kwa mateso ndani ya hiyo miaka 100 kama utafika?

Pesa unayo; sehemu za starehe huendi kuondoa msongo wa mawazo, pombe hunywi, kutalii nje ya nchi huendi, mbuga za wanyama hutembelei, pisi kali huna, zaidi ya kuwaona kwenye mtandao kama wale wanaopatikana Peru, Colombia, Venezuela n.k

Sasa, kwako utamu wa pesa nini?​
Kuenezea Injili plus kuendelezea vipaji vya watu hasa watoto[emoji120]
 
Raha ya pesa ni kukupa wide range of freedom of choice. Kwenye choice kila mtu anavipaumbele vyake.kuna anaependa wanawake, kusafiri, kunywa pombe lakini kuna mwingine hivo vitu hata hana muda navyo.
 
Kuwa na pesa ndio utamu wenyewe kuna ule uhuru binafsi unakuwa nao wa kufanya chochote ndani ya gharama zozote na ukazimudu, kwangu hii ndio utamu wa pesa. Yale mambo ya kutaka kufanya jambo fulani mpaka uombe usaidizi wa fedha yanakwamisha na kukarahisha sana.

Kuwa financially free ni furaha.
 
Utamu wa pesa ukutimizie mahitaji yako na familia yako, pia ukupe moyo wa kuweza kusaidia wengine wenye uhitaji
na la zaidi sana, usikupe kiburi cha kudharau wengine ambao hawana hizo pesa kwani kuna wengine wanafanya kazi kubwa na ngumu kuliko wewe lakini hawazipati hizo hela.
In general, pesa isikubadilishe kutoka mtu mwema na kuwa mtu katili ila ikufanye uongeze busara zaidi kwenye maisha yako. Pia umkumbuka muumba wako kwa kumshukuru kwa ajili ya pesa alizokupa na uzima/uhai.
Hii imekaa kiimani zaidi
 
Kuwa na pesa ndio utamu wenyewe kuna ule uhuru binafsi unakuwa nao wa kufanya chochote ndani ya gharama zozote na ukazimudu, kwangu hii ndio utamu wa pesa. Yale mambo ya kutaka kufanya jambo fulani mpaka uombe usaidizi wa fedha yanakwamisha na kukarahisha sana.

Kuwa financially free ni furaha.
sana jaman na umaskini tuseme ukweli unasababisha mtu kutenda dhambi ambayo haikuwa kusudi lake
tuseme mfano rahisi ni kama unahis njaa halafu uone embe la mtu na huna hela, lazima ulikwapue ila kama pesa zipo unanunua tu unaepuka dhambi ya wizi
 
Know the difference between enjoying your life and destroying your future.
 
Kula nikitakacho,Kunywa nikitakacho,Kusafiri nitakako,Kupata matibabu,Kusolve Matatizo yanapotokea,na Kuwa na uwezo wa kushiriki ktk uenezaji wa Injili pale ninaoombwa mchango na kusaidia wahitaji.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
Pesa unakuwa nayo, ata olduvai Gorge unakuwa hujui iko wapi; hii imekaaje?
 
Raha ya pesa ni kukupa wide range of freedom of choice. Kwenye choice kila mtu anavipaumbele vyake.kuna anaependa wanawake, kusafiri, kunywa pombe lakini kuna mwingine hivo vitu hata hana muda navyo.
Anakuwa na muda na nini; na ni vitu gani vinamzuia asiwe na muda na vitu hivyo?
 
Kuvaa vizuri kukoje, kula vizuri kukoje, pisi kali zikoje? Hayo yote uliyoorodhesha ni definition ya mtu. Pisi kali kwako kwa mwingine mbovu.
Ila kuna pisi ikipita, wote wananyoosha mikono juu
 
sana jaman na umaskini tuseme ukweli unasababisha mtu kutenda dhambi ambayo haikuwa kusudi lake
tuseme mfano rahisi ni kama unahis njaa halafu uone embe la mtu na huna hela, lazima ulikwapue ila kama pesa zipo unanunua tu unaepuka dhambi ya wizi
Mkuu umenielewa vyema kabisa, umasikini sio dhambi ila sio jambo jema. Kuna ile time unakutana na kitu at affordable price ila kwa kuwa huna balance unashindwa kukifanya kiwe chako kwa faida yako. Inakera sana.
 
sijasema ni dhambi ila nimesema unasababisha dhambi

teh teh asante kwa kunielewa,,,umaskini ki kitu kibaya sana na hakuna anayependa kwa kweli
mimi nikiwa wa kwanza ,,,"I hate poverty"
 
Back
Top Bottom