Pesa unayo; sehemu za starehe huendi kuondoa msongo wa mawazo, pombe hunywi, kutalii nje ya nchi huendi, mbuga za wanyama hutembelei, pisi kali huna, zaidi ya kuwaona kwenye mtandao kama wale wanaopatikana Peru, Colombia, Venezuela n.k
Sasa, kwako utamu wa pesa nini?
Haya uliyoandika hapa ni matamanio ya watu wasio na pesa. Ukiwa huna pesa unatamani vitu vingi sana...lakini siyo vipaumbele vya watu wenye pesa. Ukizipata vitu vyote vinakuwa vya kawaida. Unaweza kufanya hayo mambo once and a while na tena kwa kificho. Maana si kipaumbele.
Kuna makundi ya watu kama matatu hivi linapokuja swala la pesa.
1. Kundi la kwanza ni wale ambao hawajui kesho yao. Tunasema wana maisha magumu. Hawa hulala sehemu mbaya ambazo hazistaili binadamu kulala. Nyumba za nyasi au mabanda kama mazense. Kula yao ni ya shida na hawawezi kutimiza mahitaji yao ya msingi. Hawa ndo watu waliokata tamaa na wako tayari kufanya lolote wapate riziki ya siku. Pia wengine ni wavivu wasiopenda kujishughulisha kutokana na kukata tamaa. Yaani kwao wameshafika kibao cha Hakuna Maendeleo. Wanasogeza siku.
2. Ni kundi la watu wasio na hela lakini wenye malengo na matumaini ya kupata hela. Hawa wana amini msemo wa "One day yes". Hawa hujitahidi kutafuta hela kwa njia halali ili kutimiza malengo yao. Sasa hapa malengo yanatofautina....
2.1 Kuna wale ambao malengo na furaha yao ni kufanya hayo uliyoyataja...kuwa na wanawake warembo, kula raha kwenye ma club etc. Mapedeshee wengi ni wale wenye malengo kama yako. Hawajengi, hawasaidii wazazi, hawaangalii future yao wao pesa ni za ku enjoy.
2.2 Kuna wale ambao malengo yao ni kutengeneza business empire, kuwa na biashara kubwa kubwa, kuwekeza na kujitengenezea himaya ya utajiri. Nadhani hawa ndo unao walenga unauliza wanapata faida gani na pesa zao? Hawa furaha zao mara nyingi ni.
1. Kutatua changa moto za maisha za watu wengine. Hawa wao wana wito na wanaumia kuona watu wanapata changamoto nyingi za maisha. Hivyo wanafanya juhudi kutatua changamoto mbalimbali..na pale wanapozitatua wanaona fahari na kufurahia maisha.
2. Kutengeneza fursa kwa watu kama kutoa ajira. Kuna mtu anaona furaha kuajiri watu na . Ni wito
3. Kupata umaarufu kwenye jamii. Kuna mtu anao furaha kuwa maarufu kwenye jamaa.
4. Financial freedom. Kwa sababu wanajua wakitumia vibaya pesa zitaisha. Hivyo wanajua principle ya fedha ni kuzizalisha.
5. Kusaidia ndugu, jamaa na marafiki.
6. Kutoa misaada kwa watu wasiojiweza.
7. Kupata pesa ambazo watazitumia kufanya ubunifu ambao unawasumbua kichwani mwao. Wanataka kujaribu vitu vipya kama Ilivyo kwa Elon Mask ndoto yake ni kupeleka watu kwenda kuishi Mars.
Bill Gates yeye anataka kutokomeza Malaria.
Na mengine mengi. In short hawa watu wamevuka kwenye hizo mambo ulizotaja hapo and it no longer their agenda.