Usilinganishe elimu ya darasani na elimu ya mazingira, ni vitu viwili tofauti,
Kwanza asilimia kubwa ya wanafunzi (watu) waliokuwa na akili sana darasani huwa hawafanyi vizuri kwenye maisha ya mitaani , na kinyume chake wale waliokuwa hawafanyi vizuri darasani huwa wajanja sana mitaani,
Jiulize kama elimu ya darasani ndio u-smart wa maisha unaouzungumzia, kwanini waliosoma sana mfano maproffesors wa uchumi sio matajiri wakutupwa?!
Badala yake wale matajiri wakutupwa sio wasomi sana, mfano aliyekuwa Mkurugenzi wa IPP bwana mengi, Bakhresa, dewji, sio maproffesor kama kina lipumba, nk
Hata wakina bill get, naaliyekuwa job Steve, mkuu wa amazon, nk sio wasomi kihivyo!
Ukweli ni kwamba maproffesors wengi wanaishia kuajiriwa tu, wachache wanajiajiri, wale walioacha Chuo (shule) kama kina bill gets ndio wanaibuka matajiri,
Elimu ya darasani ni tofauti sana na elimu ya mtaani