Utapeli miamala ya simu: Usikubali malipo kwa simu toka kwa usiyemjua

Utapeli miamala ya simu: Usikubali malipo kwa simu toka kwa usiyemjua

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Huku tozo, kumbe kama vile haitoshi miamala nayo ni kwa risk zetu wenyewe?

Jamaa yangu mmoja alikubali malipo kwa M-pesa. Muamala ukasoma safi, lakini baada ya muda mlipaji akauchukua kama alivyokuwa kautuma. Wizi na utapeli wa mchana kweupe!

Kuwapata wenye mtandao wao, wakadai hii inawapata wengi.

Cha kujiuliza kama vodacom wanaujus wizi huu kuwa rampant kwanini hawajachukua hatua hata za kuuelimisha umma tu?

Au ni kuwa Vodacom wamechagua kuwa sehemu kwenye uwezeshaji wa wizi huu?

Tukimbilie wapi sisi ya Rabi?
 
Eleza kwa kina
Kina kipi zaidi ya hapo mkuu?

Malipo kwa M-pesa yanakuhusu mlipaji ku cancel malipo hayo bila kumshirikisha mlipwaji.

Kwenye kadhia hiyo vodacom (mmiliki wa mtandao) anakiri hili kuwa athiri wengi huku akidai kuwa yeye hahusiki.

Wewe unaona hiyo iko fair?

Yangu ni alert. Yamemkuta ndugu yangu yasipokukuta nawe si ndiyo furaha yangu?

Nakazia: kina kipi ukitaka zaidi ya hapo?
 
Hebu tulia kwanza halafu uandike vizuri
Siyo kuwa utulie wewe na kwamba urejee shule au hata ngumbalu kujifunza kuandika vyema?

Minufaikaji ya utapeli tapeli mkiguswa kwenye anga zenu kwani huwa mnaweza japo kukaa kimya?

Mbona hatutaacha kuwapelekeeni moto? Tafuteni kazi zingine huku hatutawaacha salama.

Na bado!
 
Huna akili wewe, malipo unalipa kwa lipa namba. Hi ni kwa mitandao yote. Hujui lakini unaleta ujuaji mwingi
 
Huo ni uongo..ukilipa kwa lipa ya voda huwezi rudisha muamala..acha kuchafua makampuni ya watu
Kwamba unaita uongo bila ya kuwa na ufahamu wowote wa kadhia hii?

Vodacom amekiri tatizo hili ni rampant?

No wonder kuna Tanzania ya viwanda ikijengwa katika awamu fulani.

Bure kabisa!
 
Hana alijualo lakini anatukana tu watu

Ulijualo wewe ni lipi ndugu? Yamewakuta wengine. Alert inawekwa hapo kukutahadharisha na wewe ukiwamo kabla ya hatari umekomaa. Kwani ujinga ni nini basi?
 
Kulipia bidhaa unajua inatakiwa utumie njia gani? Je ni kwa mpesa au lipia namba??
 
Huku tozo, kumbe kama vile haitoshi miamala nayo ni kwa risk zetu wenyewe?

Jamaa yangu mmoja alikubali malipo kwa M-pesa. Muamala ukasoma safi, lakini baada ya muda mlipaji akauchukua kama alivyokuwa kautuma. Wizi na utapeli wa mchana kweupe!

Kuwapata wenye mtandao wao, wakadai hii inawapata wengi.

Cha kujiuliza kama vodacom wanaujus wizi huu kuwa rampant kwanini hawajachukua hatua hata za kuidhinisha umma tu?

Au ni kuwa Vodacom wamechagua kuwa sehemu kwenye uwezeshaji wa wizi huu?

Tukimbilie wapi sisi ya Rabi?
Story iko shallow sana
 
Story iko shallow sana

Kwamba kuna watu wanakubali kulipwa kwa mpesa kupisha changamoto fulani zinazoweza kujitokeza?

Kwamba baada ya hapo walipaji wana reverse miamala?

Kwamba vodacom wamekiri kadhia hii ipo na kuwa imeathiri wengi?

Kwamba habari hii ni alert kwa wengine kama wewe isikikukute kwani hutopata msaada?

Kwamba kwako hayo ni shallow?

Kwa hakika kama nchi tumekubuhu kwa ujinga!
 
Kulipia bidhaa unajua inatakiwa utumie njia gani? Je ni kwa mpesa au lipia namba??

Mada uesoma mkuu?

"Usikubali kulipwa kwa mpesa na mtu usiyemfahamu. Tatizo hili limeathiri wengi." Vodacom anathibitisha hayo privately lakini si publicly.

Wakati vodacom anasema hayo hayo na waathirika in privacy hapa nimeweka hadharani kwa faida ya wengine.

Tatizo liko wapi hapo jombi?
 
Back
Top Bottom