- Thread starter
- #41
Umeandika vyema.Nadhani nilikuwa sijakuelewa lakini nikawaza sana hii sio issue ya voda tu ni mitandandao yote sababu kuna option ya mtu kurudisha muamala hata wewe unaweza kufanya ikiwa uliyemtumia ile pesa hajaitumia au kuitoa sasa huu wizi unaweza kutumika ikiwa humjui mtu unayefanya kazi au kwa mfanya biashara ni kuwa na line pekee anayojuwa yeye tu ukimtumia then anatuma kwenye number nyingine lakini hilo nalo issue kwenye makato. Option pekee kukabiliana na hili malipo kubali kwa mtu unamjuwa huyu ni nani au mitandao ya simu waondoe hii option japo ilikuwa na nia nzuri lakini sote tunajuwa kuna watu kazi yao kuharibu tu. Inabidi waje na system more safe ya kurudisha muamala iwe labda ukikosea kutuma kwa mtu na unataka kurudisha isiwe unarudi kwako ila kwa kampuni then after 48 hours kuipata ile pesa upite voda au kampuni yoyote wajiridhishe hii itampa muda mwingine kujuwa kama katapeliwa. wizi wa mitandao ni changamoto unaweza kupunguza ila tabu kuzuia 100% makampuni makubwa Visa na Mastercard hii hali wanapitia sana ni level tofauti tu. kikubwa nakubaliana na hoja usikubali malipo hovyo hovyo labda ukiwa umejiandaa kuhamisha pesa ikiingia tu safe number. kwa wafanya biashara wa kubwa best option kuwa na number unayoijuwa wewe tu sio mteja kuhifadhi baada ya kutumiwa na mteja.
Mteja ana haki ya kulindwa. Kumnyima elimu sahihi na kwa wakati kiasi cha kumwacha exposed kwenye utapeli kama hivi makampuni ya simu hayawezi kukwepa lawama.
Sikumaanisha hili ni voda peke yake.
Ninakazia: kama taifa tunayo safari ndefu bado kuhusiana na uwezo wa kuchakata habari. Kwa maana hata waliopaswa kuelimisha wengine ndiyo hao unaowaona humu JF.
Cc: Allency