Mwalimu wa tuisheni
JF-Expert Member
- Oct 19, 2019
- 6,602
- 10,801
Zote mbiliKulipia bidhaa unajua inatakiwa utumie njia gani? Je ni kwa mpesa au lipia namba??
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Zote mbiliKulipia bidhaa unajua inatakiwa utumie njia gani? Je ni kwa mpesa au lipia namba??
Mkuu option ya kurudisha muhamala ni nzuri sana na inahitajika kwenye swala zima la kutuma pesa. Mpesa au Tigopesa ilianzashwa kwa lengo la kutumiana pesa na siyo kufanyia malipo. Baada ya watu kuanza kutumia Mpesa au tigopesa kama njia ya kufanya malipo ndiyo kampuni hizo zikaja na suluisho la lipa namba.Umeandika vyema.
Mteja ana haki ya kulindwa. Kumnyima elimu sahihi na kwa wakati kiasi cha kumwacha exposed kwenye utapeli kama hivi makampuni ya simu hayawezi kukwepa lawama.
Sikumaanisha hili ni voda peke yake.
Ninakazia: kama taifa tunayo safari ndefu bado kuhusiana na uwezo wa kuchakata habari. Kwa maana hata waliopaswa kuelimisha wengine ndiyo hao unaowaona humu JF.
Cc: Allency
Hapana mkuu, mpesa ni kwa kutuma pesa na lipa namba ni kwa kufanya malipo. Ukitumia mpesa kwa kufanya malipo na ukapigwa basi jua imekula kwako na wala kampuni haitahusika kwa huo ujinga wako. Sema wajinga ni wengi sana nchi hii ndiyo maana bado kuna watu wanapigwa na wale wa tuma kwenye namba hii.Zote mbili
Ndio Kuna namba maalum za uwakala zinaitwa LIPA KWA M-pesa au TIGOPESA, Hizo Ni kwa wale wafanyabiasharaKina kipi zaidi ya hapo mkuu?
Malipo kwa M-pesa yanakuhusu mlipaji ku cancel malipo hayo bila kumshirikisha mlipwaji.
Kwenye kadhia hiyo vodacom (mmiliki wa mtandao) anakiri hili kuwa athiri wengi huku akidai kuwa yeye hahusiki.
Wewe unaona hiyo iko fair?
Yangu ni alert. Yamemkuta ndugu yangu yasipokukuta nawe si ndiyo furaha yangu?
Nakazia: kina kipi ukitaka zaidi ya hapo?
Huyo aliyetapeliwa Ni mjinga, usikubali kulipwa kwa njia ya kawaida ya mtandao, Kuna namba maalum zakulipia bidhaa kwa mtandaoKwamba unaita uongo bila ya kuwa na ufahamu wowote wa kadhia hii?
Vodacom amekiri tatizo hili ni rampant?
No wonder kuna Tanzania ya viwanda ikijengwa katika awamu fulani.
Bure kabisa!
LIPA NAMBA YA MPESA AU TIGO PESA inapokea pesa kutoka mitandao yote... shukrani. Wafanyabiashara wanasubiri kuchangamkia huduma hiyo (Lipa kwa X-Pesa)? Ila kama ingewezekana kutokea mtandao mmoja ukalipa mtandao mwingine ingekuwa vizuri sana.
Pia lipa namba zinapatikana bure bila malipo kabisa. Mtu anatuma pesa then anakuja kulalamika eti alifanya malipoNdio Kuna namba maalum za uwakala zinaitwa LIPA KWA M-pesa au TIGOPESA, Hizo Ni kwa wale wafanyabiashara
Kuna uthibitisho toka vodacom kuwa tatizo hili ni rampant kwao. Bila shaka Airtel, Tigo na Halotel. Yet unathubutu kusema nani asiyejua?Yaani your alert is too obvious. Ni sawa na kuwaambia watu kuwa dawa ya kupaka usiinywe. Nani asiyejua
Umeandika vyema.Kuna jamaa alikuwa na coaster alikuwa anatoka kupelekanwanafunzi mazinde, akaja pale segera akatubeba, abiria wawili wakasema hawana cash hela ipo kwa simu akwapa namba yake ya simu wakamtumia nauli yao kwa simu pesa, wale jamaa waliahuka chalinze, ile coaster ikawa inaenda moro, na mm naenda moro hivyo nikabaki kwenye hiyo coaster, kufika mdaula jamaa anagundua wale watu wawili walomlipa kwa simu pesa wamejirudishia ule muamala, so wizi wa aina hii upo
Kuchangia mada ambayo mwenyewe hujaielewa ndiyo matokeo yake haya.Pia lipa namba zinapatikana bure bila malipo kabisa. Mtu anatuma pesa then anakuja kulalamika eti alifanya malipo
Kabisa lipa namba naikubali sana,jaman wafanyabiashara wenzangu tuamke...lipa namba mtu hawez rudisha muamala.Hujaelewa alichoandika, soma tena
Inajulikana, Lipa namba, business namba na ukitumamtandao mwingine huwezi rudisha ,
Ila muamala wa kumhamishia mtu unaweza rudisha sababu assumption ni kuwa mtumaji kakosea kutuma. Kama unahitaji kulipwa sajili lipa namba ni bure
Pana maswali manne yaliyo wazi pale. "Ndiyo" hii ni jibu kwa swali lipi?Ndio Kuna namba maalum za uwakala zinaitwa LIPA KWA M-pesa au TIGOPESA, Hizo Ni kwa wale wafanyabiashara
Ujinga ina maana kutokujua jambo kwa wakati huo. Mtu akishaelimishwa ujinga huishia hapo. Uzi huu umelenga kutoa elimu hiyo. Hata kichwa cha habari nacho hukusoma?Huyo aliyetapeliwa Ni mjinga, usikubali kulipwa kwa njia ya kawaida ya mtandao, Kuna namba maalum zakulipia bidhaa kwa mtandao
Huku tozo, kumbe kama vile haitoshi miamala nayo ni kwa risk zetu wenyewe?
Jamaa yangu mmoja alikubali malipo kwa M-pesa. Muamala ukasoma safi, lakini baada ya muda mlipaji akauchukua kama alivyokuwa kautuma. Wizi na utapeli wa mchana kweupe!
Kuwapata wenye mtandao wao, wakadai hii inawapata wengi.
Cha kujiuliza kama vodacom wanaujus wizi huu kuwa rampant kwanini hawajachukua hatua hata za kuuelimisha umma tu?
Au ni kuwa Vodacom wamechagua kuwa sehemu kwenye uwezeshaji wa wizi huu?
Tukimbilie wapi sisi ya Rabi?
Walioingia mkenge waliamini kuwa wamelipwa au wewe wamekwambia vinginevyo?Hapa wewe unakuwa ulipi kwa Mpesa bali UNATUMA pesa kwa Mpesa kama form ya malipo ya biashara iliyofanyika, hizi ni huduma mbili tofauti, ambapo ukilipa kwa Mpesa hakuna uwezekano wa ku reverse malipo!
Mkuu sema walimtumia pesa na siyo kuwa walimlipa, huwezi lipa kwa Mpesa au tigopesa, kulipa inabidi utumie lipa namba ya MPESA au Tigopesa au nyinginezo. Pia kumbuka unaweza lipa toka mtandao wowote na lipa namba ni bureKuna jamaa alikuwa na coaster alikuwa anatoka kupelekanwanafunzi mazinde, akaja pale segera akatubeba, abiria wawili wakasema hawana cash hela ipo kwa simu akwapa namba yake ya simu wakamtumia nauli yao kwa simu pesa, wale jamaa waliahuka chalinze, ile coaster ikawa inaenda moro, na mm naenda moro hivyo nikabaki kwenye hiyo coaster, kufika mdaula jamaa anagundua wale watu wawili walomlipa kwa simu pesa wamejirudishia ule muamala, so wizi wa aina hii upo
Soma mada kujiridhisha kuwa swali lako ni relevant.Huduma ya lipa kwa simu huijui?!
Niliona hatari ya huduma hii tangu ilipoanza.
Ninawashauri Vodacom na watoa huduma wengine kuongeza kipengele cha kuwasilisha madai katika migogoro ya namana hii.
Wakati mtu anarudisha muamala unaoshukiwa au anafanya hivyo kwa sababu ya ulaghai. Watoa huduma wanatakiwa kuzuia muamala kwa pande zote mbili na kisha wote wajulishwe na kuwasilisha madai yao pamoja na uthibitisho wa huduma au bidhaa iliyotolewa.
Pia ninawashauri wanaopokea malipo kuanza kutumia "Lipa kwa Simu" itakuwa rahisi kwa watoa huduma kutofautisha miamala ya kibiashara na miamala ya kibinafsi. Kwa sababu ni rahisi kwa watu wanaotumia miamala ya kibinafsi kujuana kuliko wale wanaofanya miamala ya biashara.
Kwa upande wa wanunuzi, natumai watadai risiti ya mauzo ya bidhaa au huduma ili waweze kutetea malalamiko yao pale mfanyabiashara anapojaribu kutumia mwanya huu kufanya utapeli.
Na mwisho, serikali kupitia mamlaka ya mapato TRA, iboreshe mifumo ya utoaji wa risiti za mauzo kidijitali.
Tuache hizi mashine za EFD tuwe na App ambayo mfanyabiashara ataweka kwenye kifaa chake cha kidijitali ili afanye mauzo, sio kama hii App unayopigiwa chapuo, App inayolenga kukusanya kodi bila kumsaidia mfanyabiashara, haitaweza kutatua changamoto hii ya ulaghai.
App inapaswa kuwa mfumo kamili wa POS ambapo mfanyabiashara anaweza kuingia kwa kutumia TIN namba yake na kisha kuugeuza ili uweze kukufaa kulingana na biashara anayofanya. Na kila mauzo yanapaswa kuwa na taarifa za kina kuhusu bidhaa au huduma iliyotolewa pamoja na nambari ya serial ya mauzo hayo, ambayo itakuwa ya kipekee kwa TIN na mfanyabiashara huyo. Hii itafanya upataji wa maelezo ya mauzo kuwa rahisi na haraka.
Kazi ni kwa mlalamikaji kuwasilisha serial number ya muamala huo, TRA wataithibitisha kupitia data za mfanyabiashara, kama ilivyo kwa control namba ya huduma za serikali. Na mtoa huduma (SP) atakuwa na taarifa za kutosha kujua kama muamala umekosewa au kulikuwa na jaribio la ulaghai.
Kwa uharaka na ufanisi nyenzo za kidigitali huu mchakato unaweza kufanyika chini ya masaa 24.
Na hii changamoto ikapata muarobaini wake.
Tupo katika mazingira ya kidijitali ambayo yanaacha alama katika kila jambo tunalofanya, lakini iwapo mazingira haya hayana mwingiliano mzuri na mazingira asilia basi kutakuwa na ugumu wa kutatua migogoro inayohusisha mazingira haya yote kwa pamoja. Watoa huduma na mamlaka za serikali lazima ziendane na kasi ya mabadiliko ya kidijitali, la sivyo watakuwa na changamoto ambazo watashindwa kuzitatua.