- Thread starter
- #121
mkuu kwanza pole kwa matatizo
pili Polisi, TCRA, na kampuni za simu wanatoa sana elimu kwa njia ya sms.
ukipata muda pitia hapa:
Nawatetea Serikali, TCRA, Polisi na mitandao ya simu kuhusu utapeli wa "Tafadhali tuma kwa namba hii"
Nitangulize samahani kwa wadau watakaodhani natetea uhalifu (ubaya) wa namna yoyote. Lakini wema na ubaya havijawai kuachana kama mwanga na giza. Ifikie hatua waibiwaji tujitathmini. Ubaya ukikwaza wengi mtu timamu huangalia wapi tatizo linaanzia. Hili la wizi wa mtandaon kama "tafadhari...www.jamiiforums.com
Nimepapitia pote mkuu pamoja na vikorombwezo vyake.
Ikumbukwe tunatofautiana kielimu, cognition power, instincts nk. Vyote vyote kwa pamoja vikikamilisha vinavyoitwa ubinadamu. Hatuwezi kuwa sawa.
Wajomba wa tuma kwa namba hii, na hii ya kuhamishiwa muamala baada ya huduma au manunuzi (ndani ya changamoto kadhaa) ni tofauti.
Angalia posts #86 na #89 kujiridhisha.
Jamaa yangu yalipompata ilikuwa yapata 22:00 baada ya kuwa wamemsingizia na tapeli mbobezi huyo kutafuta vibanda vya mpesa bila mafanikio ili atoe cash bila ya mafanikio.
Kuhamisha muamala kwa simu kiungwana ikawa ni compromise ukizingatia ustaarabu na kauli za mteja yule.
Ama kwa hakika umdhaniaye siye, ndiye.
Hivi sasa keshaumwa na nyoka. He learnt it the hard way.
Kwamba ma operator wanatoa elimu kwa SMS? Nikiri sijawahi kuona moja iliyo katika msingi wa mada hii.
Binafsi nikiri pia, haya hayajanikuta thanks ni kwa instincts tu na kwa hakika ashukuriwe bwana wa majeshi!
Nayasema haya tokea mjini, sembuse pande za dongo beshi, nanjilinji na mwalusembe huko?!
Ninakazia: Jamaa yangu katapeliwa kwa kutowajibika ipasavyo kwa wabeba dhamana. Kwao Tozo ni muhimu zaidi wala si usalama wetu.