Hii njia niliwahi itumia kwa hawara mshenzi!
Nikamtumia 30k nikasubiria ahsante yake.
Nilivyoona kapiga kimya nikampandia hewani kumuuliza kulikoni kimya?
Alinijibu hadi nikatetemeka kwa ghadabu:
"Hela gani ya nyanya hiyo mwanaume mzima unatuma?"
Baada ya majibu yake hayo, faster nikairudisha kwa option ya kutuma hela kimakosa!
Hata iliporejeshwa, yeye kwenye account yake akabaki na figures zile zile.
Kimbembe kilikuja alipotaka kwenda kutoa ili anigidie mimi bwege, kakuta sifuri.
Kwa kuwa nilijua atanitafuta, nikamblock mapema kimya kimya.
Baada kama ya siku3 nikakuta simu imejaa miss call zake, nikajua tayari jiwe nililolirusha gizani limepopoa mtu.