Utapeli miamala ya simu: Usikubali malipo kwa simu toka kwa usiyemjua

Utapeli miamala ya simu: Usikubali malipo kwa simu toka kwa usiyemjua

Kwamba kuna watu wanakubali kulipwa kwa mpesa kupisha changamoto fulani zinazoweza kujitokeza?

Kwamba baada ya hapo walipaji wana reverse miamala?

Kwamba vodacom wamekiri kadhia hii ipo na kuwa imeathiri wengi?

Kwamba habari hii ni alert kwa wengine kama wewe isikikukute kwani kutopata msaada?

Kwamba kwako hayo ni shallow? Kwa hakika kama nchi tumekubuhu kwa ujinga!
Unaandika pumba.

Hueleweki.

Either story umehadithiwa ukaipokea vibaya.

Ama aliyekuhadithia naye kaipokea vibaya.
 
Kina kipi zaidi ya hapo mkuu?

Malipo kwa M-pesa yanakuhusu mlipaji ku cancel malipo hayo bila kumshirikisha mlipwaji.

Kwenye kadhia hiyo vodacom (mmiliki wa mtandao) anakiri hili kuwa athiri wengi huku akidai kuwa yeye hahusiki.

Wewe unaona hiyo iko fair?

Yangu ni alert. Yamemkuta ndugu yangu yasipokukuta nawe si ndiyo furaha yangu?

Nakazia: kina kipi ukitaka zaidi ya hapo?
Asante
 
Unaandika pumba.

Hueleweki.

Either story umehadithiwa ukaipokea vibaya.

Ama aliyekuhadithia naye kaipokea vibaya.
Unayeandika pumba mbona ni wewe mkuu?

Nimeandika wapi taarifa nimeipata.

1. Tapeli kapewa huduma halali.
2. Kulipa hakukuwa na vibanda vya mpesa karibu.
3. Baada ya kuzunguka kutafuta vibanda mtoa huduma akakubali pesa hizo ahamishiwe yeye.
4. Masaa takribani 10 baadaye muamala ukawa reversed.
5. Mtoa huduma akawalisiana na vodacom kupata ufafanuzi.
6. Vodacom anakiri madhila kama haya kuwapata wateja wake wengi.
7. Ndiyo nimehadithiwa.
8. Nimetafiti vya kutosha kabla ya kuleta uzi huu.

Zingatia - vodacom wanasikitika kwa mapungufu yao haya.
 
Huna akili wewe, malipo unalipa kwa lipa namba. Hi ni kwa mitandao yote. Hujui lakini unaleta ujuaji mwingi
Kama hujaelewa busara huwa ni kuuliza.

Ulichoandika hapa kwa hakika hakina uhusiano na mada iliyopo.

Sorry to inform you: "you're totally out of context."
 
Kwa hiyo nimemtumia mtu fedha kimakosa, nimerudisha muamala wangu, mimi nimekuwa tapeli?

Mbona kama hujielewi, au ndio tapeli kazidiwa ujanja
 
Unayeandika pumba mbona ni wewe mkuu?

Nimeandika wapi taarifa nimeipata.

1. Tapeli kapewa huduma halali.
2. Kulipa hakukuwa na vibanda vya mpesa karibu.
3. Baada ya kuzunguka kutafuta vibanda mtoa huduma akakubali pesa hizo ahamishiwe yeye.
4. Masaa takribani 10 baadaye muamala ukawa reversed.
5. Mtoa huduma akawalisiana na vodacom kupata ufafanuzi.
6. Vodacom anakiri madhila kama haya kuwakataa wateja wengi.
7. Ndiyo nimehadithiwa.
8. Nimetafiti vya kutosha kabla ya kuleta uzi huu.

Kwamba mburula mmoja au wawili kama wewe ndiyo wenye hoja nyepesi nyepesi hizi kuwa ndiyo werevu?

Zingatia - vodacom wanasikitika kwa mapungufu yao haya.
Huyo wa Vodacom uliyewasiliana nae either ni tapeli kama wewe au hamkuelewana kama jinsi ambavyo hujaeleweka hoja yako hapa
 
Kwa hiyo nimemtumia mtu fedha kimakosa, nimerudisha muamala wangu, mimi nimekuwa tapeli?

Mbona kama hujielewi, au ndio tapeli kazidiwa ujanja
Kwamba umepokea huduma. Ukadai huna cash ukadai utafute kibanda cha mpesa. Muda umekwenda hakuna kibanda kilicho wazi karibu.

Ukapendekeza uhamishe pesa hizo kwa mtoa huduma. Kiungwana kwa kutuona mstaarabu mtoa huduma akkubali kukupunguzia usumbufu.

Masaa 10 baadaye uka reverse muamala huo.

Wewe si ni tapeli tu?

Si kuwa jamii isiyo na uelewa mpana na watu kama nyie inastahili kuelimishwa kuwa macho na watu kama wewe?

Am hakika wa kuchomwa moto si nyie wala si kibaka mwizi wa kuku?
 
Huyo wa Vodacom uliyewasiliana nae either ni tapeli kama wewe au hamkuelewana kama jinsi ambavyo hujaeleweka hoja yako hapa
Siyo kuwa hujaelewa hoja mjomba, bali ukimbilia kuandika?
 
Umekunywa bia, na kuamua kulipa bili kwa kumtumia pesa zilizoko kwenye simu yako aliyekuuzia, awe Barmaid au Kaunta wa hiyo bar.

Baada ya muda ukazirudisha hizo pesa kwako tena. Kwenye simu yako kupitia huduma ya kurudisha muamala uliotumwa kimakosa.

Hapa inamaana umemwibia aliyekuuzia Bia.

Tahadhari.
Usikubali kulipwa kwa njia ya kurushiwa pesa ya kwenye simu na mtu usiye mjua.

Atarudisha muamala wake aliokutumia pesa na kukusababishia hasara ya bidhaa yako.
 
Huku tozo, kumbe kama vile haitoshi miamala nayo ni kwa risk zetu wenyewe?

Jamaa yangu mmoja alikubali malipo kwa M-pesa. Muamala ukasoma safi, lakini baada ya muda mlipaji akauchukua kama alivyokuwa kautuma. Wizi na utapeli wa mchana kweupe!

Kuwapata wenye mtandao wao, wakadai hii inawapata wengi.

Cha kujiuliza kama vodacom wanaujus wizi huu kuwa rampant kwanini hawajachukua hatua hata za kuidhinisha umma tu?

Au ni kuwa Vodacom wamechagua kuwa sehemu kwenye uwezeshaji wa wizi huu?

Tukimbilie wapi sisi ya Rabi?
Nadhani nilikuwa sijakuelewa lakini nikawaza sana hii sio issue ya voda tu ni mitandandao yote sababu kuna option ya mtu kurudisha muamala hata wewe unaweza kufanya ikiwa uliyemtumia ile pesa hajaitumia au kuitoa sasa huu wizi unaweza kutumika ikiwa humjui mtu unayefanya kazi au kwa mfanya biashara ni kuwa na line pekee anayojuwa yeye tu ukimtumia then anatuma kwenye number nyingine lakini hilo nalo issue kwenye makato. Option pekee kukabiliana na hili malipo kubali kwa mtu unamjuwa huyu ni nani au mitandao ya simu waondoe hii option japo ilikuwa na nia nzuri lakini sote tunajuwa kuna watu kazi yao kuharibu tu. Inabidi waje na system more safe ya kurudisha muamala iwe labda ukikosea kutuma kwa mtu na unataka kurudisha isiwe unarudi kwako ila kwa kampuni then after 48 hours kuipata ile pesa upite voda au kampuni yoyote wajiridhishe hii itampa muda mwingine kujuwa kama katapeliwa. wizi wa mitandao ni changamoto unaweza kupunguza ila tabu kuzuia 100% makampuni makubwa Visa na Mastercard hii hali wanapitia sana ni level tofauti tu. kikubwa nakubaliana na hoja usikubali malipo hovyo hovyo labda ukiwa umejiandaa kuhamisha pesa ikiingia tu safe number. kwa wafanya biashara wa kubwa best option kuwa na number unayoijuwa wewe tu sio mteja kuhifadhi baada ya kutumiwa na mteja.
 
Umekunywa bia, na kuamua kulipa bili kwa kumtumia pesa zilizoko kwenye simu yako aliyekuuzia, awe Barmaid au Kaunta wa hiyo bar.

Baada ya muda ukazirudisha hizo pesa kwako tena. Kwenye simu yako kupitia huduma ya kurudisha muamala uliotumwa kimakosa.

Hapa inamaana umemwibia aliyekuuzia Bia.

Tahadhari.
Usikubali kulipwa kwa njia ya kurushiwa pesa ya kwenye simu na mtu usiye mjua.

Atarudisha muamala wake aliokutumia pesa na kukusababishia hasara ya bidhaa yako.

Umeandika vyema. Dawa ya hili ni elimu ya kutosha kwa watu. Makampuni ya simu yalipaswa kuwa mstari wa mbele kwenye kuwapa watu elimu hiyo.

Kwamba tunasema hapa na kwa kutokuelewa kwao wengine wanaona wajinga ni sisi?

Hiyo ndiyo Tanzania sasa ambako hata asiyekuwa na ujuzi ni nguli mbobezi.
 
Siyo kuwa hujaelewa hoja mjomba, bali ukimbilia kuandika?
Hujaelewa alichoandika, soma tena
Inajulikana, Lipa namba, business namba na ukitumamtandao mwingine huwezi rudisha ,

Ila muamala wa kumhamishia mtu unaweza rudisha sababu assumption ni kuwa mtumaji kakosea kutuma. Kama unahitaji kulipwa sajili lipa namba ni bure
 
Mada uesoma mkuu?

"Usikubali kulipwa kwa mpesa na mtu usiyemfahamu. Tatizo hili limeathiri wengi." Vodacom anathibitisha hayo privately lakini si publicly.

Wakati vodacom anasema hayo hayo na waathirika in privacy hapa nimeweka hadharani kwa faida ya wengine.

Tatizo liko wapi hapo jombi?
Hapa wewe unakuwa ulipi kwa Mpesa bali UNATUMA pesa kwa Mpesa kama form ya malipo ya biashara iliyofanyika, hizi ni huduma mbili tofauti, ambapo ukilipa kwa Mpesa hakuna uwezekano wa ku reverse malipo!
 
Umekunywa bia, na kuamua kulipa bili kwa kumtumia pesa zilizoko kwenye simu yako aliyekuuzia, awe Barmaid au Kaunta wa hiyo bar.

Baada ya muda ukazirudisha hizo pesa kwako tena. Kwenye simu yako kupitia huduma ya kurudisha muamala uliotumwa kimakosa.

Hapa inamaana umemwibia aliyekuuzia Bia.

Tahadhari.
Usikubali kulipwa kwa njia ya kurushiwa pesa ya kwenye simu na mtu usiye mjua.

Atarudisha muamala wake aliokutumia pesa na kukusababishia hasara ya bidhaa yako.
Hapa mkuu kwa Vodacom kwao hujafanya Malipo bali Umetuma pesa au umehamisha pesa kwenda kwenye namba ya Bar maid au Kaunta ya Baa, kulipa kwa Mpesa unatumia namba ambayo sio ya simu ndio maana hakuna maelewano hapo juu, na huduma ya kulipa kwa Mpesa haina huduma ya ki reverse transaction.
 
Mpumbavu hujui unalolisema ... security ya lipa ni kubwa kuliko unavolinda private parts zako

Mpumbafu zaidi ni wewe. Hawakukosea waliotambua - ajidhaniaye kasimama ..

Umesoma mada ukaelewa au kukurupuka tu kama unataka msalani?

Vodacom anakiri kadhia hii ipo na imeathiri wengi sembuse mrugaruga wewe?
[/QUOTE]
Najua nnachokisema
 
Unayeandika pumba mbona ni wewe mkuu?

Nimeandika wapi taarifa nimeipata.

1. Tapeli kapewa huduma halali.
2. Kulipa hakukuwa na vibanda vya mpesa karibu.
3. Baada ya kuzunguka kutafuta vibanda mtoa huduma akakubali pesa hizo ahamishiwe yeye.
4. Masaa takribani 10 baadaye muamala ukawa reversed.
5. Mtoa huduma akawalisiana na vodacom kupata ufafanuzi.
6. Vodacom anakiri madhila kama haya kuwapata wateja wake wengi.
7. Ndiyo nimehadithiwa.
8. Nimetafiti vya kutosha kabla ya kuleta uzi huu.

Zingatia - vodacom wanasikitika kwa mapungufu yao haya.
Ebu sema uyo mtu aliyeibiwa izo hela ..hela alitumiwa kwenye laini zipo Kati ya hizi...?? 1.lipa kwa simu 2.Laini ya kawaida..? 3.laini ya uwakala wa mpesa.
 
Back
Top Bottom