Utapeli miamala ya simu: Usikubali malipo kwa simu toka kwa usiyemjua

Ndo maana kuna kitu inaitwa lipa kwa Number hii
 
Voda lipa
 
Kuna lipa kwa number hii, sasa kama mnalipana kwa njia ya kawaida hio ni shauri yenu
 
"Kupelekea moto" ni msamiati wa matusi ya nguoni.

Kwa nini umeutumia katika kuwasilisha agenda chanya?
 
Hivi mtoa mada angeliandika kwa usanifu hivi, kungelifurika hoja za missunderstanding zisizo na ulazima?
 
Tatizo lugha uliyoitumia kuwasilisha mada mkuu.

Huoni huyo jinsi alivyoeleweka kirahisi?
 
... na ndio maana wajanja kama unataka kumtumia pesa kutokea mbali hakubali umtumie kwenye namba yake. Anakutumia details za wakala utume kwake kuondoa risk ya ku-cancel mwamala baada ya kutuma.
Hii njia niliwahi itumia kwa hawara mshenzi!

Nikamtumia 30k nikasubiria ahsante yake.

Nilivyoona kapiga kimya nikampandia hewani kumuuliza kulikoni kimya?

Alinijibu hadi nikatetemeka kwa ghadabu:
"Hela gani ya nyanya hiyo mwanaume mzima unatuma?"

Baada ya majibu yake hayo, faster nikairudisha kwa option ya kutuma hela kimakosa!

Hata iliporejeshwa, yeye kwenye account yake akabaki na figures zile zile.

Kimbembe kilikuja alipotaka kwenda kutoa ili anigidie mimi bwege, kakuta sifuri.

Kwa kuwa nilijua atanitafuta, nikamblock mapema kimya kimya.

Baada kama ya siku3 nikakuta simu imejaa miss call zake, nikajua tayari jiwe nililolirusha gizani limepopoa mtu.
 
Airtel wanakutangazia kifurushi cha "dakika 150 kwa 1000 Tsh mitamdao yote" lakini ukishalipia wanakupa dk 110 Airtel to Airtel na only dk 40 mitamdao yote! Wizi mtupu!
 
"Kupelekea moto" ni msamiati wa matusi ya nguoni.

Kwa nini umeutumia katika kuwasilisha agenda chanya?

Kila mtu ana haki ya tafsiri yake. Vyema kuwa umetambua agenda ni chanya. Ila maneno highlighted hapa chini uliweza kuyaona au hata kuyatambua tu?
"Kupelekea moto" ni msamiati wa matusi ya nguoni.

Kwa nini umeutumia katika kuwasilisha agenda chanya?

La kheri umetambua agenda ni chanya. Wengine akiwamo huyu mwamba Allency hawakuona hivyo.

Tafsiri ni kwa mujibu wa kamusi za Kiswahili sanifu zilizopo bwerere maktaba na kwenye maduka ya vitabu.

Msimamo ni ule ule watu makini hawachukuliwi kireja reja na tafsiri uchwara za vijiweni.

Rejea kuyaona matusi na waasisi kujiridhisha wanaostahili lawama ni nani.
 

Tapeli yeyote hujisifia kwa utapeli wake. Walisema Nginde - 'kama aikudanganya na kupoteza wakati wako bure, ajue kuwa mambo hayo yatamfika naye."

Waungwana wengine husema malipo ni hapa hapa duniani.
 
Tatizo lugha uliyoitumia kuwasilisha mada mkuu.

Huoni huyo jinsi alivyoeleweka kirahisi?

Kwenye maandiko yoyote huwa kuna disclaimer na scope.

Ukiona umeshindwa kuelewa rejea kujiridhisha disclaimer na scope zilikuwa ni zipi?

Usipoyaelewa mawili hayo hoja kama hii yako sasa unaweza kudhani ni zinga la point.

Karibu kwenye uwanja wa elimu ambako ukishindwa kuelewa usishangae kuwa kumbe tatizo laweza kuwa hata ni lako tu.
 
Ilitakiwa iwe unatoa taarifa voda kua umekosea halaf wao wapige namba ya kule ulikokosea ili kuthibitisha kama ni kweli amepokea kimakosa. Na ikithibitika amepokea kihalali basi yule mtoa taarifa azuiwe kufanya miamala kwa wiki nzima
 
Ilitakiwa iwe unatoa taarifa voda kua umekosea halaf wao wapige namba ya kule ulikokosea ili kuthibitisha kama ni kweli amepokea kimakosa. Na ikithibitika amepokea kihalali basi yule mtoa taarifa azuiwe kufanya miamala kwa wiki nzima
Ilitaka haki bin haki. Utapeli ni utapeli tu hauna tofauti na wizi wa kibaka mwizi wa kuku.
 

USITUMIE MPESA AU TIGO PESA KUPOKEA MALIPO SABABU HAZIKUTENGENEZWA ILI KUFANYA MALIPO, ZINARUHUSU KURUDISHA MUAMALA IWAPO MTUMAJI AMEKOSEA. TUMIA NAMBA MAALUM ZA MALIPO KAMA HIZO KWENYE PICHA, KWENYE MENU YAKO IMEANDIKWA LIPA KWA SIMU NA SIO TUMA PESA. UKIFANYA HIVI HUTATAPELIWA.
 

Msingi wa hoja - inatakikana elimu.

Imefanyanyika tathmini kutambua kiasi gani cha wanajamii kingali gizani huku utapeli huu ukiendelea?

Ni hayo tu ndugu mjumbe.
 
Reactions: Tsh
Msingi wa hoja - inatakikana elimu.

Imefanyanyika tathmini kutambua kiasi gani cha wanajmii kingali gizani huku utapeli huu ukiendelea?

Ni hayo tu ndugu mjumbe.
Ndo elimu hiyo inatolewa na wadau kua mtu asikubali kutumiwa pesa, anatakiwa alipwe sio kutumiwa pesa. Ukitumiwa pesa hujalipwa, umepewa na aliyekupa anaruhusiwa kuirudisha. Ukilipwa ni ya kwako na haiwezi chukuliwa bila ridhaa yako.

Kupewa PESA/kutumiwa PESA njia: MPESA, TIGOPESA, AIRTEL MONEY, NAMBA YA WAKALA.

Kulipwa PESA njia: LIPA NAMBA YA VODA/TIGO.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…