Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 1,679
- 2,123
Kabla ya kuufichua huo utapeli, hebu tuwasikilize kwanza hawa manabii feki:
Nabii XXL: Aisee, hizi sadaka tunazopata hazitoshi kununua ndege, na kutufanya tuishi maisha ya kifahari. Naomba tubuni mbinu ya kuongeza mapato.
Nabii X: Mi nafikiri wakati wa maombezi, tuwe tunawauzia watu chumvi, mafuta, maji na vitambaa, lakini tuwaambie kwamba vitu hivyo vina upako. Watanunua tu.
Nabii XXL: Mh, tukifanya hivyo kabla ya kuwaombea, watatugundua. Katika Biblia Yesu si alisema huduma za kuponya na kutenda miujiza hazipaswi kutolewa kwa malipo?
Nabii X: Mkuu, watu hawana muda wa kusoma Biblia, hawajui hilo Andiko. Nakwambia watanunua tu. Tena tukiwaambia mafuta na chumvi vimetoka Israeli, ndio kabisa, hata tukiwauzia kwa dola watanunua.
Nabii XXL: Hahaa, aisee we una akili. Hebu tuanze haraka kuifanyia kazi hiyo mbinu. Ndani ya mwaka mmoja tu, tutakuwa mabilionea.
================
Nyakati hizi za mwisho manabii wengi wa uongo wametokea na kuwadanganya wengi kama Maandiko yanenavyo(Mt24:11). Na watu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Maneno ya Mungu yako wazi lakini kwakuwa watu hawasomi Biblia wanadanganyika kirahisi.
Ni kweli katika Biblia mafuta na chumvi vimetajwa. Kwa mfano katika kitabu cha Yakobo 5:14 imeandikwa:"Mtu wa kwenu anaumwa? Na awaite wazee wa kanisa, nao watamuombea, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana." Andiko hili linaonyesha kuwa upako wa mafuta ni sehemu ya ibada na uponyaji wa kiroho.
Katika Marko 6:13 imeandikwa pia hivi – "Wakatoa pepo wengi, wakawapaka mafuta wengi waliokuwa wagonjwa, wakawaponya." Andiko hili linaonyesha pia jinsi Mitume walivyotumia mafuta kwa uponyaji.
LAKINI Maandiko hayo hayatuambii kwamba wagonjwa, wenye shida na wanaohitaji baraka wanapaswa kununua bidhaa hizo ili wapone au wabarikiwe. Kwahiyo wauzaji ni matapeli.
Katika Mathayo 10:8, tunasoma kuwa Yesu aliwapa wanafunzi wake mamlaka ya kuponya wagonjwa na kufukuza pepo, lakini aliwaonya wasifanye huduma hiyo kwa kudai malipo.
Mathayo 10:8 – "Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure."
Andiko hilo linaonyesha wazi kuwa karama za Mungu zinapaswa kutolewa bure.
Enyi mnaolifanya Jina la Mungu litukanwe kwa sababu mmewalaghai watu kuwa chumvi na mafuta mnayouza yana upako, kumbe uongo, nawasihi, popote pale mlipo ulimwenguni, badilikeni. La sivyo unabii huu utatimia kwenu:
Mathayo 7:22-23 – "Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu."