Utapeli wa Dawa ya 'HIT' katika kuua Mbu

Naunga mkono hoja. Hii dawa nilianza kuishtukia muda. Bora na wewe umeliona hili. Dawa nzuri ya kupuliza ya mbu ni Rungu. HIT ni mtengenezaji ni MO?
 
Ulifanya mauwaji ya kimbari ya biodiversity mkuu [emoji23]
 
Ni kama Air freshener.. tu

Tunaibiwa sana.
Ni kweli. Hili ni la siku nyingi sana. Sana sana unakuwa kama unawapulizia mbu perfume ili watoke out kuja kunyonya damu wakiwa wananukia vizuri. Vipi Expel siku hizi hamna? Jmabo jingine la kuzingatia ni kununua dawa kutoka vyanzo vinavyoaminika. Binadamu tumekuwa kama wanyama na tuko tayari kutengeneza dawa zenye madhara ili tu kupata fedha. Kama mchina mimi simwamini kabisa.
 
Rungu ni kali sana. Mimi ndiyo dawa ya mbu nayoiamini. Cha ajabu hata zile dawa za kuchoma za blue aka pellets siku hizi hazina ukali tena kama zamani.
Mbona wadau wanazikandia hizo dawa za Rungu?

Zile za kuchoma sas ndio huwa zinawazimisha.. Wanazimia kwa muda wakiamka wanarudi na Hasira na njaa.

Usiombe umeme ukatike maana feni inasaidia.

Dawa nyingi ni za kufukuza tu kaa muda yaan temporary solution.
 
Mbu wame evolve na kuweza kutengeneza usugu dhidi ya hizi dawa. Inatakiwa kununu dawa ya aina tofauti ili kupata matokeo chanya, jaribu kumtumia Ile dawa ya kuchoma inakua kwenye package ya silver .
 
Kweli mkuu wanazimia tu halafu wanaamka. zamani ulikuwa unazoa/unafagia mbu kibao ukifukiza kwa dawa za kuchoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…