Utapeli wa upatu wa kimtandao ni janga sugu Tanzania, Serikali ina la kujifunza

mzeewabarakoa

Member
Joined
Oct 20, 2024
Posts
9
Reaction score
8
Habari za muda huu ndugu zangu kuna jambo linaniwazisha sana hasa juu ya hii mifumo ya upatu maarufu kama Ponzi schemes(kama sijakosea herufi) binafsi sijawahi kushiriki

Ila naona kama serikali inachelewa sana kutambua haya mambo au inafanya makusudi? au kuna baadhi ya watumishi wa serikali huwa wananufahika nayo Kwa namna fulani? ,hivyo wanazipa gape zinufaike huku wao wakipata chochote kitu behind?

Siituhumu serikali kwamba ni wazembe Ila kuna baadhi ya mambo yanafikirisha kidogo,kwamba haya hawayaoni kweli hao wahusika wanaosimamia? maana tafsiri yake usalama wa wananchi kwa njia ya mtandao ni mdogo na wahusika wanaosimamia ni kama wameshindwa wajibu wao ni kama wameshindwa hilo kusimamia, hii haileti picha mzuri Kwa serikali hivyo nashauri vyombo husika kuwa active na wepesi

Hivi akitokea mtu akamtukana raisi mtandaoni huwa inachukua muda gani kukamatwa kuchukiliwa hata za kinidhamu?

Mbona mambo makubwa kama haya yanayoumiza wananchi yanakuja kugunduliwa too late watu wameshaumia? Na hata yanapogundulika wananchi hawarudishiwi pesa zao?

Nakumbuka DECI,Mr. Kuku na nyingine nyingi pamoja na LBL ,watu wamewekeza weee ndio baadaye serikali inakuja kuingilia kati tatizo nini hasa ..anayeelewa zaidi anieleweshe tafadhali maana inanifikirisha sana

Asante
 
Inaonekana TCRA na BOT hakuna kitu wanajua maana hawa jamaa wanaonekana wakitangaza matangazo yao kila kukicha mtandaoni na inachukua muda kweli baadae unakuja kusikia eti wameanza kuwakamata baada ya Wananchi kupoteza fedha wao hawawezi kuzuia kabla ya hao wezi wa Mtandao hawajaanza kuiba.
 
Sema wananchi ndio wajifunze sio serikali wajifunze.
Serikali wanaweza wakawa wanajua ila wana mambo mengi ya kufanya hawawezi kuwa macho muda wote kuzuia usitapeliwe cha msingi inabidi wewe muhusika uwe macho
 
Ni changamoto sana
 
Uko sahihi, ila hayo mambo mengi waliyo nayo Serikali ikiwemo na hili kama jukumu lao, pia namna ya uelewa kwa watu tunatofautiana wakati elimu ikiendelea kutolewa Kwa wananchi pia serikali iboreshe miundombinu yake ya kuzuia haya majanga Kwa njia ya kimtandao
 
Kuna mkono wa vigogo humo maana pesa ndefu sana inakusanywa
 
Sema wananchi ndio wajifunze sio serikali wajifunze.
Serikali wanaweza wakawa wanajua ila wana mambo mengi ya kufanya hawawezi kuwa macho muda wote kuzuia usitapeliwe cha msingi inabidi wewe muhusika uwe macho
Umeombwa Msaada? . Punguza shobo Dada
 
Sio kwamba wanaacha kwanza hela zijae kwenye kibubu halafu ndio wazichukue ? Maana hizo hela huwa zinataifishwa 🐼
 
Project za watu hizo haiwekani watu walewale Ila muda na nyakati tofauti wakawa wanaanzisha kitu kilekile na wakishapiga hela wanakamatwa watu fulani na baada ya hapo hatuoni muendelezo

Mfano Manguruwe, Doctor Kuku n.k

Ina maana hii pyramid huwa inaanzishwa na watu wachache wanafaidika na wengi wanaliwa na mwisho ni kesi

walikikuwepo Deci hadi Leo hii. LbL

Hii ni miradi ya watu na kwanini wakati wa Magufuli hii miradi haikuepo tuseme ilikuwa wapi

Haya mambo nina zaidi ya maika 15 nayasikia na style ni hizi hizi , kamlete na yule kamlete upate hela.
 
Habari za muda huu ndugu zangu kuna jambo linaniwazisha sana hasa juu ya hii mifumo ya upatu maarufu kama Ponzi schemes(kama sijakosea herufi) binafsi sijawahi kushiriki

Ila naona kama serikali inachelewa sana kutambua haya mambo au inafanya makusudi? au kuna baadhi ya watumishi wa serikali huwa wananufahika nayo Kwa namna fulani? ,hivyo wanazipa gape zinufaike huku wao wakipata chochote kitu behind?

Siituhumu serikali kwamba ni wazembe Ila kuna baadhi ya mambo yanafikirisha kidogo,kwamba haya hawayaoni kweli hao wahusika wanaosimamia? maana tafsiri yake usalama wa wananchi kwa njia ya mtandao ni mdogo na wahusika wanaosimamia ni kama wameshindwa wajibu wao ni kama wameshindwa hilo kusimamia, hii haileti picha mzuri Kwa serikali hivyo nashauri vyombo husika kuwa active na wepesi

Hivi akitokea mtu akamtukana raisi mtandaoni huwa inachukua muda gani kukamatwa kuchukiliwa hata za kinidhamu?

Mbona mambo makubwa kama haya yanayoumiza wananchi yanakuja kugunduliwa too late watu wameshaumia? Na hata yanapogundulika wananchi hawarudishiwi pesa zao?

Nakumbuka DECI,Mr. Kuku na nyingine nyingi pamoja na LBL ,watu wamewekeza weee ndio baadaye serikali inakuja kuingilia kati tatizo nini hasa ..anayeelewa zaidi anieleweshe tafadhali maana inanifikirisha sana

Asante
Wananchi wajinga tu. Hata wakiambiwa huu ni utapeli wanasema ni pesa zetu, kwani nani kalalamika kuwa katapeliwa n.k.
Wa kwanza kula wa mwisho kuliwa. Ipi mpya iliyokuja tuwahi mapema?
 
Hizo ni projects za watu na hao watu ndo wanaanzisha hizo project Kwa kubadilisha tittle na muda na tarehe .

Inahitaji akili kuelewa hili maana wao hucheza na Saikolojia ya mtu kwakuwa wanatumia wasanii na baadhi ya Vyombo Vya habari vyenye ushawishi .
 
Mibongo ni mifala sana. Juzi tu hapo Kalynda kawaliza, inakuja nyingine ya aina hiyo hiyo ikiwa imebadili tu jina na inawaliza tena

Mibongo ni mijuaji na mibishi, unaiambia hiyo kitu ni utapeli, hakuna mtu anaweza kukulipa kiasi hicho cha pesa kwa kuangalia video sekunde 10 ila bado inabishana, acha itapeliwe ijufunze.
 
Uko sahihi, ila hayo mambo mengi waliyo nayo Serikali ikiwemo na hili kama jukumu lao, pia namna ya uelewa kwa watu tunatofautiana wakati elimu ikiendelea kutolewa Kwa wananchi pia serikali iboreshe miundombinu yake ya kuzuia haya majanga Kwa njia ya kimtandao
Sikatai kuwa serikali ni jukumu lao lakini wakati huo serikali wanajiandaa kwenda kuwazuia itakuwa tayari ushatapeliwa hasara ni ya nani?
 
Hizo ni projects za watu na hao watu ndo wanaanzisha hizo project Kwa kubadilisha tittle na muda na tarehe .

Inahitaji akili kuelewa hili maana wao hucheza na Saikolojia ya mtu kwakuwa wanatumia wasanii na baadhi ya Vyombo Vya habari vyenye ushawishi .
Tamaa tu. Yah ni same people hiyo lbl ilianzia kenya ilikuwa inaitwa CBL kitu kama hicho ikawapiga pia
 
Halafu ilivyokuwa mijinga eti inakuja kuomba serikali iwasaidie kulinda pesa zao,wangekuwa wanajielewa angalau wakitapeliwa waugulie maumivu kimyakimya iwe funzo kwenye maisha yao ya baadae lakini ndio kwanza inajitokeza hadharani kuilaumu serikali,pesa yako ya kuitafuta mwenyewe unangojea mtu mwingine ndio aje kuwa na uchungu nayo.
 
Umeombwa Msaada? . Punguza shobo Dada
Kwa akili hizi za kuwazawaza misaada kwa nini usitapeliwe?ukitapeliwa jifungie ndani uugulie kimyakimya usiite mtu mwingine aje akusimamie jitambue.
Kwa kujilegeza huko mwisho wa siku utakuja kuomba mtu akulelee mkeo na watoto wako
 
Kwa ujumla mimi sioni matatizo kwa haya makampuni. Haya makampuni mengi hayawaumizi wananchi. Serikali ndio inayowaumiza wananchi. Ksbb mpaka serikali kuifungia hiyo kampuni hakuna mwananchi alietoa malalamiko serikalini kuhusiana na hiyo kampuni.

Mfano hili sakata linaloendelea la LBL. Hakuna mwananchi alieenda serikalini kutoa malalamiko yoyote kuhusiana na LBL kwamba anadhurumiwa.
Bali serikali inasema imeifungia LB L ksbb haijajisajiri B.O.T.

Serikali ilitakiwa Ione wananchi waliowekeza kwa wingi kwenye hiyo LBL. Ilitakiwa ichunguze then kama swala ni usajiri wangeongea na LBL kwa taratibu ili waendelee kujisajiri. Negotiation hiyo inafanyika ili kuwanusuru wananchi waliowekeza humo. Sio kama hivi ghafla tu asubuhi unafungia kampuni ambayo unaona kabisa kuna watu wengi wataumia. Serikali ndio kila kitu kwa wananchi,basi ilitakiwa iwaone hawa waliojitupia humo ili wasalimike. Sio kama hivi shauri yao nani amewaambia wawekeze huko?
 
Back
Top Bottom