Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Nimeona kwa siku za karibuni kuona Waziri au Mawaziri wakifanya kazi ya kukagua ama kuzindua ama kutembelea miradi isiyo chini ya wizara zao. Sasa katika utaratibu huu mpya nilikuwa na Maswali kadhaa ila leo nauliza machache.
Je utaratibu huu hauwezi kuleta migogoro ya chinichini na chuki binafsi miongoni mwa Mawaziri? Mfano ikionekana waziri fulani anafanya kazi ya kuzindua na kukagua miradi mbalimbali ambayo inagusa wizara mbalimbali.au vipi ikionekana waziri fulani amekuwa mbele sana kutoa maelekezo na kujishughulisha sana na mambo ya wizara za wenzake kuliko hata wizara yake?
Vipi ikitokea Waziri fulani yupo wizara fulani ambayo yeye haipendi kivile au hana uzoefu sana na masuala ya wizara hiyo na akaamua kuwa anatumia muda mwingi sana kufanya kazi za wizara nyingine? Yaani mfano waziri ni msomi mzuri sana wa Udaktari na ni bingwa na nguli sana katika eneo hilo, halafu ikatokea ameteuliwa wizara ya michezo au maendeleo ya jamii jinsia na watoto au wizara ya katiba au wizara ya ulinzi.
Hivyo kwa sababu yeye ni daktari bingwa na ana utalaamu wakutosha katika secta ya Afya akaamua muda mwingi na wote kujikita zaidi katika masuala yenye kugusa secta au wizara ya afya.na katika kugusa huko ikaonekana anafanya vizuri sana na yupo na uelewa mpana sana kuliko waziri wa wizara hiyo.
Je waziri wa wizara hiyo atajisikiaje pale atakapoona sifa kutoka kwa watanzania zinakwenda zaidi kwa waziri huyo asiye husika na wizara hiyo? Je hii haiwezi kuleta chuki binafsi miongoni kwa mawaziri hawa? Je hii haiwezi kumvunja moyo waziri wa wizara husika kuona kwamba anaingiliwa sana na yeye kuonekana hafanyi kazi vizuri na kwamba anatakiwa hata ampishe huyo anayepitapita sana katika wizara hiyo?
Je nini mantiki ya kuwa na waziri katika kila wizara? Inakuwaje waziri afanye kazi katika wizara asiyohusika nayo? Je hii inamaanisha kuwa wizara zingine hazina kazi na majukumu mengi mpaka kumfanya waziri kukosa kazi za kufanya na kuanza kufanya kazi za wizara zingine? Kama ni hivyo kwanini wizara zisizo na majukumu makubwa mpaka mawaziri wao kukosa kazi zisifutwe au kuunganishwa na wizara zingine?
Je vipi kama maelekezo yakawa yanatofautiana? Yaani leo waziri huyu anatoa maelekezo fulani halafu wiki ijayo mwingine anakuja kutoa maelekezo mengine? Vipi kama maelekezo ya waziri fulani asiye wa wizara hiyo akatoa maelekezo yaliyokinyume na utaratibu? Mfano waziri akamfukuza mkandarasi site halafu baadaye mkandarasi akafungua kesi na kushinda na kutakiwa kulipwa mabilioni ya pesa kama fidia.nani atabeba lawama? Nani atawajibika? Italeta picha gani?
Kama mawaziri sasa wanauhuru wa kujitanua uwanja mzima na kucheza namba zote .sasa nafasi ya waziri Mkuu inakuwa ipoje? Vipi naibu waziri Mkuu nafasi yake? Ngoja niishie hapa mara moja nitarejea baadaye kidogo.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.