Utaratibu mzima wa kufungia ndoa kanisani ni uhuni tu, kanisa limepora mamlaka yasiyowausu ili kuzitawala ndoa

Mwafrika ulimwambia ukweli anasema ni ujinga, badala ya kutoa hoja zake ili kufifisha huo ukweli anaishia kusema kwa jazba eti ni ujinga. Ndio maana Wazungu wanatudharau, walituletea dini zao tukakubali kama mazuzu bila kuhoji.
 
Ndo mnavyodanganyikaga? Hivi kama ni upana wa elimu ya dini waisrael ndo wangekuwa wakuletetea hilo suala ! Wew upana wa dini zilizoanza kwa migogoro ya madaraka ndo ziwe na upana wa elimu? Hivi ungezaliwa na familia ya kikristu ungetetea dhehebu gani hapa? Je hao Wachina ambao hawataki kutawaliwa na tamaduni za mashariki ya kati unaona walivyo na heshima tena na akili panaa. Toka nje ya boksi
 
Mkuu natamani nianzishe uzi niorodheshe ukakasi uliopo kwenye dini mbalimbali ikiwemo uislamu,ukatoliki,usabato,n.k lakini nashikwa na uvivu kwa sababu nina uhakika majibu yatakayotolewa yatasababisha ukakasi zaidi badala ya kunitoa kwenye utata. Labda niunganishwe na waasisi wa hizo dini(kama bado wapo hai). Niwaulize mbele ya waumini wao.

Sent from my 2201116TG using JamiiForums mobile app
 
Kwani umelazimishwa kuoa kanisani?
 
Siku utakapoamua kuwa mfuasi wa Mungu badala ya kuwa mfuasi wa Dini ndio kidogo lugha zetu zinaweza kulandana lakini Kwa sasa hatuwezi kufikia muafaka.

Sent from my 2201116TG using JamiiForums mobile app
 
Hata Mimi nimelifikiria sana suala la kufunga Ndoa kanisani Mkuu.

1. Mimi ni Mtoto wa Askofu KKKT.
Na Mzee wangu anewahi kuwa mkuu wa kanisa. KKKT.

2. Utaratibu wa kibiblia na Ndoa wakufungishwa na Taasisi za kidini ni kama DINI/ kanisa limehodhi Mamlaka ya ki Ukoo, kifamilia na kimila.

Lakini kanisa ndio linalowalea Wana ndoa kabla ya ndoa, Wakati wa kufunga ndoa na Baada ya ndoa.

YAANI linawalea kiroho
kuwafunza ndoa
kupata vyeti vya ndoa
Ustawi wa ndoa.
na Suluhisho ya migogoro yote ya kindoa.

FAMILIA, KOO, NA JAMII KWA UJUMLA VIMESHINDWA KUWALEA VIJANA KIMAADILI. HADI KUPELEKEA DINI KUINGILIA KATI SUALA LA NDOA.

3. Kanisa na Dini ya Dunia imejipa Mamlaka ya kitaasisi.
Kutoa mafunzo ya ndoa.

UISLAMU NI MILA ZA KIARABU, SIO DINI WALA TAASISI YA KI UNGU
MAVAZI.
LUGHA.
VylYAKULA.
NA MTINDO WA KIMAISHA.
NI MILA ZA KIARABU
 
We ukiwa na nafasi lete Uzi itakuwa ni elimu tosha ...usiwe na wasi .
 
Naona unataka ligi tu nachelea kusema huna hoja za msingi Kama uislam ungekuwa unatetereshwa kwa kushindwa kujibu hoja basi dhahiri usingekuwepo mpaka leo hii tunavyozungumza hivyo hakuna kipya utakachouliza kiwe hakijawahi kuulizwa na kujibiwa.
 
Naona unataka ligi tu nachelea kusema huna hoja za msingi Kama uislam ungekuwa unatetereshwa kwa kushindwa kujibu hoja basi dhahiri usingekuwepo mpaka leo hii tunavyozungumza hivyo hakuna kipya utakachouliza kiwe hakijawahi kuulizwa na kujibiwa.
Kudaka watu utotoni ni miongoni mwa mbinu za kujipatia waumini wa kudumu. Ni ngumu kuchomoka kwenye hicho kitanzi. Waasisi wa hizi dini sio wajinga. Ni watu wenye mikakati madhubuti ya kuhakikisha dini zao zinaishi(hazifi) hata kama wao wanakufa.

Sent from my 2201116TG using JamiiForums mobile app
 
Naona unataka ligi tu nachelea kusema huna hoja za msingi Kama uislam ungekuwa unatetereshwa kwa kushindwa kujibu hoja basi dhahiri usingekuwepo mpaka leo hii tunavyozungumza hivyo hakuna kipya utakachouliza kiwe hakijawahi kuulizwa na kujibiwa.
Majibu yanayotolewa ndiyo yanazua utata zaidi. Hivyo kujibiwa sio hoja,hoja ni je,hayo majibu yanajibu kweli au yanazua utata zaidi?

Sent from my 2201116TG using JamiiForums mobile app
 
Hakuna uhusiano wa kukuzwa kuanzia utoto na kuwa muumini wa kudumu nikwambie kitu ambacho hukifaham ni kwamba kuwa nje ya imani ni rahisi Sana kuliko kudumu katika imani.
 
Kama kanisa halijakulazimisha kufunga ndoa kanisani, malalamiko yoyote dhidi ya kanisa ni malalamiko yasiyo na mantiki.

Kwa sababu unalalamikia kitu ambacho hujalazimishwa kufanya.

Unalalamikia pilipili, wakati meza ina vyakula kibao ambavyo havina pilipili.Unaruhusiwa kula.

Kwa nini unalalamikia pilipili ambayo hujalazimishwa kula?

Kwani usipokula pilipili ukaamua kula vyakula vingine utakufa?
 
Eti alichounganisha Mungu asitenganishe binadamu! Binadamu si ndio aliounganisha? Je ikigundulika mmoja ni mchawi tuendelee tu bila talaka? Mimi napiga chini naenda kwenye ndoa ya serikali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…