Utaratibu na gharama za kupata hatimiliki ya nyumba/kiwanja

Namshukuru Jamaa kwa kuwa amejitolea kwa kuandika uzi mzuri tena kwa moyo wake wote. lakini ktk wasomaji 47000 jamaa amepata like 3. pamoja na ya kwangu kweli nimejifunza kitu watantania wengi swala kushukuru limewapita kushoto.
 
Wakuu natanguliza shukrani zangu kwenu,
Nilinunua kijishamba huku Kisewe 2004 kwa mtu nae alinunu kwa mwenyeji, sasa hati ya mauziano ina jina lake huyo nilie nunua kwake na sasa hayupo hapa dar, nahitaji kupimiwa eneo langu na hatiamye nipate hati tittle deed,nifanyejee ngd zangu.
cc@ Kiyanga and others
 
Samahani kaka kumradhi,kama hutojali naomba namba yako nikupigie kuna mambo natamani kueleweshwa au nifanyaje ili niskilizwe Kwa ukaribu
 

Ñaomba niulizie hapa na kila mwenye uelewa wa hili naomba anieleweshe.
Iwapo imebaki nyumba ya urithi na hati haijulikani ilipo Kwa maana wazazi waliaga dunia pasi na kutoa taarifa za hati miliki.
Je,mrithi anatakiwa kufata taratibu gani ili aweze kupata hati miliki upya,inachukua muda gani na inagharimu kiasi gani.
Naomba kuwasilisha
 
Kama kiwanja kimepimwa maana yake Plot number na Block number mtakuwa mnaijua, kama taratibu za mirathi mmefanya maana yake mhusika anatakiwa afanye ufuatiliaji ofisi ya ardhi ili muweze kupata hati nyingine japokuwa kiutaratibu mnatakiwa mtangaze kupotea kwa hati kwa siku 30 kwenye gazeti then mnaenda kuomba hati nyingine (ila kabla ya kutangaza hatua zingine za loss report kwa police zifuatwe.

Nashauri uende ofisi ya ardhi kwenye halmashauri uliyopo Kwa ushauri zaidi

Kingine kama hati haionekani mjitahidi kulipa Kodi ya ardhi ili mtu asije akawa ameibadili nyie hamna habari lakini ukilipa Kodi ya ardhi (kama kimepimwa) jina linakuwa linasoma jina la marehemu na huo ni mwanzo mzuri wa kuonyesha umilki wenu na hata mtu akifanya lolote kuhusu hiyo nyumba mnakuwa na receipts zenu zote za Kodi ya kiwanja
 
Ni
Pe namba yako mkuu
 
I
Tafadhali Naomba namba yako kiongozi
Nina mengi yakukuelezea
 
Mkuu ni pm namba yako
 
OK
Nafuatilia hii kitu
 
Mkuu ni pm namba yako
Kama una issue wewe tupia tu hapa ili tuelimishane kwa pamoja ili kama nakueleza kitu kama nakuwa nimekosea mwingine anarekebisha... mie sio mtaalam kivile ile nina share uzoefu kama mmilki wa ardhi.

Huu uzi ni wa miaka 14 iliyopita (tangu 2010) na taratibu pia zimebadilika hivyo sintokupa kitu sahihi sana huko PM lakini hapa inakuwa rahisi kurekebishana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…