Ni hatua ndefu. Kwanza lazima uwe na uthibitisho kuwa hilo eneo la ardhi ni lako. Pili uende wilayani kitengo cha ardhi. Wao watakupa picha yote. Ni lazima waje wapime eneo husika walipeleke wizarani likishakubaliwa watakutengenezea mawe ya pembeni (beacons) yenye namba zao. Baada ya hapo ndio watapeleka waizani ili maandalizi ya hati yaanze. Malipo ya kisheria yapo lakini siwezi kujua ni kiasi gani kwani inategemeana na ukubwa wa eneo na mahali lilipo. Kwa sababu uko nje ya mkoa wa DSM hati utaipata mapema tu!